ushauri

Fay Pub

Fay Pub
Fay Pub Sinza,We Rock,it is a good place to be cool and usalama wa kutosha!!Fay Pub ipo Sinza kumekucha,nyuma ya Seven Up kama unaelekea shamool Hotel,, kwa maelekezo piga namba 0715 556453

tangaza

Monday, September 3, 2012

NAMNA HII ELIMU TANZANIA ITABOREKA.

WAKUU wa shule za sekondari nchini wametakiwa kuacha tabia ya kusajili wanafunzi ambao hawajapata nafasi ya kuchaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari, kwa kigezo cha kuziba nafasi ya wale waliochaguliwa na kushindwa kuripoti kwa muda mwafaka.
Badala yake wafuate taratibu na kanuni za Wizara ya Elimu  na Mafunzo ya Ufundi katika kusaili wanafunzi.
Viongozi hao waliopewa dhamana ya kusimamia taratibu za kuhakiki wanafunzi wanaojiunga na elimu hiyo, walipewa onyo hilo juzi mjini Kibaha, katika mkutano wa wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania.
Onyo hilo lilitolewa na Mwakilishi wa Mkaguzi Mkuu wa Shule za Sekondari katika Kanda ya Mashariki, Paulo Moshi, ambaye alisema vitendo hivyo vinapingana na sheria za nchi.
Alisema kuwa kitendo cha baadhi ya wakuu wa shule za sekondari kuwasajili kinyemela wanafunzi ambao hawakuchaguliwa, kinarudisha nyuma maendeleo ya elimu.
Alisema hiyo inatokana na ukweli kwamba baadhi ya wanafunzi hao wanakuwa wanaingia katika shule za sekondari, huku wakiwa hawana sifa inayostahiki.
“Napenda kuwasihi juu ya hili kuwa hiki ni kitendo ambacho kinarudisha nyuma maendeleo ya nchi hasa katika nyanja ya elimu, naomba tujirekebishe kama kutakuwa na wanafunzi wanaoshindwa kuripoti kwa muda mwafaka kwa sababu mbalimbali, basi tutumie kanuni zetu zilizowekwa na Wizara ya Elimu,”alisema Moshi.

Alisema katika kuwaingiza wanafunzi wasiokuwa na sifa kunasababisha matokeo mabaya  ya mitihani.

Source;Natafutashule.com

No comments:

Post a Comment