ushauri

Fay Pub

Fay Pub
Fay Pub Sinza,We Rock,it is a good place to be cool and usalama wa kutosha!!Fay Pub ipo Sinza kumekucha,nyuma ya Seven Up kama unaelekea shamool Hotel,, kwa maelekezo piga namba 0715 556453

tangaza

Thursday, September 6, 2012

OMMY DIMPOZ KUZINDUA VIDEO YA BAADAE JUMAPILI SEPT 9


MSANII wa Muziki wa Kizazi kipya anaetamba na nyimbo zake mbili za Nai Nai na Baadaye, na mshindi wa Tuzo mbili za Kili Music Award 2012, Ommy Dimpoz anataraji kuzindua Video yake mpya ya Baadaye katika ukumbi wa Club Maisha Septemba 9,2012 jijini Dar es Salaam.
 
Akizungumza na Blog hii, Meneja wa Msanii huyo, Mbaruku Issa ‘Mubenga’ alisema kuwa maandalizi yote yamekamilika na show itakuwa ya uhakika naya kuvutia.

Mubenga amesema Omy Dimpozy ameifanyia shooting video yake hiyo nchini Afrika Kusini.
 
Aidha Mubenga amesema kuwa kazi ya utayarishaji wa video hiyo ulifanywa na Adam Juma wa Visual Lab ambaye ndiye walisafiri nae hadi Africa Kusini na wameshoot kwenye maeneo mazuri na ya kifahari yaliyopo nchini humo ambapo ameona utofauti mkubwa katika kufanya video nje na nyumbani.
 
“Kazi hii ni ya uhakika ambayo tunaizidua Jumapili hii na Video hiyo imefanyika Johannesburg mitaa ya Sendton na nikatika location kali na za uhakika,”alisema Mubenga. 
 
Amesema wasanii kadhaa watasindikiza uzinduzi huo akiwepo Chegge Chigunda, Suma Mnazareth na Nas 3 siku hiyo katika uzinduzi wa video hiyo mpya na Ommy Dimpoz nae atakuwa katika muonekano tofauti si Dimpoz waliye mzoea.
 
Pia Meneja huyo wa Ommy Dimpoz amesema akiwa nchini Afrika kusini Dimpoz alimshirikisha Model ambaye amekuwa akifanya kazi na wasanii wengi wakali wa Muziki nchini humo anaejulikana kwa jina la Tully Tshabalala. 
 
“Wimbo ni mkali na mashabiki wanaukubali vilivyo na tunaomba mashabiki wa Bongo Fleva wakae tayari kwa video hiyo mpya itakayoanza sasa kuchezwa katika vituo vya Televisheni nchini na kumbi za burudani baada ya uzinduzi huo,” alisema Mubenga.

Mubenga amewakata wakazi wa jiji la Dar es Salaam ambao ni mashabiki na wapenzi wa muziki wa kizazi kipya kujitokeza kwa wingi kumpa support Dimpoz katika uzinduzi huo wa aina yake katika Club Maisha Oysterbay jijini la Dar es Salaam jumapili.
 
Source;burudan.blogspot.com

No comments:

Post a Comment