ushauri

Fay Pub

Fay Pub
Fay Pub Sinza,We Rock,it is a good place to be cool and usalama wa kutosha!!Fay Pub ipo Sinza kumekucha,nyuma ya Seven Up kama unaelekea shamool Hotel,, kwa maelekezo piga namba 0715 556453

tangaza

Thursday, August 30, 2012

ALI KIBA NA DIAMOND PLATNUMZ NANI MKALI NA KIOO CHA JAMII.


Swali kwenye kichwa cha habari linajieleza. Nani zaidi kati ya Ali Kiba na Diamond? Tunaposema zaidi tuangalie mambo kadhaa; muziki,uimbaji,umiliki wa jukwaa,management (kwa maana jinsi msanii anavyojiongoza au kuongozwa na yeyote aliye nyuma yake), mafanikio ndani na nje ya nchi, likability yaani jinsi anavyokubalika au hata kujikubali yeye mwenyewe.Hapo tunaweza kuongeza muonekano…msanii hana budi kujiweka vizuri..ni kioo

Wednesday, August 29, 2012

CHADEMA YACHANGIA WAFIWA MORO.

KATIBU mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk. Wilbroad, Slaa jana
 alilazimika kuendesha shughuli ya kuomba msaada wa fedha kutoka kwa watu waliofurika kwenye mkutano wa chama hicho mjini Morogoro ili kuwachangia wafiwa na walioathirika na vurugu zilizoanzishwa na polisi dhidi ya wafuasi wa chama hicho.
Akifafanua, alisema zitatumika kuwasaidia majeruhi wawili waliopigwa risasi na polisi jana ambao wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.

Pia fedha hizo zitapekwa kwa familia ya marehemu Ally Zolla anayesemekana aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi wakati wa vurugu hizo.

Mmiongoni mwa watu waliozunguka na bakuli hilo ni pamoja na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika.

Fedha hizo hazikufahamika idadi yake hadi mwandishi wetu anaondoka kwenye viwanja hivyo majira ya saa moja usiku.


Source;Mateja  

Thursday, August 23, 2012

CHADEMA WAHUJUMIWA KATIKA KAMPENI ZA M4C ULANGA.

Jitihada za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) za kuwafikia wanachi ili kunadi sera zake, hususan katika mikutano inayoendelea katika mkoa wa Morogoro, zilikumbana na vikwazo mbali mbali katika baadhi ya maeneo, kama inavyoonyesha pichani, mtaro uliochimbwa katika barabara ya kuingia kijiji cha Namgezi kitongoji cha Kambi ya Keya jimbo la Ulanga Mashariki, kwa lengo la kuzuia magari yasipite.Picha na Joseph Senga
News source;Mateja20

MGUUU PANDE VIJANA KUANZA DEPO 2012!!!!NI WA O LEVEL NA A LEVEL 2011-2012

JESHI la polisi Tanzania limetoa ajira 1,446 kwa Vijana wa kidato cha nne wa mwaka 2011,kidato cha sita mwaka 2012 na vijana walioko kambi za JKT Mafinga, Mlale, Ruvu, Mgambo Oljoro , Bulombola, Kanembwa, Itende, Nachingwea na Mgulani.
Kati ya hao 951 ni walio hitimu kidato cha nne na sita mwaka 2011/2012 na 495 kwa Vijana waliokuwa katika Kambi za JKT za JKT Mafinga, Mlale, Ruvu, Mgambo Oljoro , Bulombola, Kanembwa, Itende, Nachingwea na Mgulani. 
Maelekezo Muhimu:-
1. Vijana wa kidato cha nne wa mwaka 2011,kidato cha sita mwaka 2012 na vijana walioko JKT Mafinga, Mlale, Ruvu, Mgambo Oljoro , Bulombola, Kanembwa, Itende, Nachingwea na Mgulani waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi baada ya mchakato wa usaili uliokamilika hivi karibuni wanatakiwa kuripoti Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi kati ya tarehe 06/10/2011 na 07/10/2012 kwa ajili ya zoezi la usajili litakaloanza chuoni hapo tarehe 8.10.2012.
2. Vijana hao wanatakiwa kuripoti tarehe 05/10/2012 kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa kwa ajili ya kuwaandalia usafiri wa kuwapeleka Chuoni.
3. Vijana wanaotoka katika makambi ya JKT yaliyotajwa hapo juu wataripoti kwa makamanda wa Polisi wa mikoa iliyo karibu nao.
Vijana wa kidato cha nne na sita wataripoti kwa makamanda wa Polisi wa Mikoa waliojiandikisha wakati wa zoezi la usaili lililoendeshwa mwezi Julai, 2012.
4. Atakaeamua kuripoti kwa Kamanda wa Polisi ambako hakupangiwa atalazimika kujigharimia usafiri hadi Chuo cha Polisi Moshi
5. Vijana hawa wanatakiwa kufika chuoni wakiwa na mahitaji yafuatayo:
a) Vyeti vyao vyote vya masomo(Academic Certificates/Result slip pamoja na Leaving certificates) kidato cha Nne/Sita, Vyeti vya kuzaliwa (Original Birth certificates). Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.
b) Mashuka mawili rangi ya Bluu Bahari (light blue)
c) Chandarua
d) Nguo za michezo(Track suit nyeusi,Tshirt blue na Raba)
e) Pasi ya Mkaa
f) Ndoo moja.1
g) Pesa kidogo ya kujikimu.
6. Kwa mujibu wa kanuni za chuo ni marufuku kufika chuoni na simu ya mkononi, atakayepatikana na simu atafukuzwa chuoni hapo. Chuo kitaelekeza na kusaidia kufanya mawasiliano. 
7. Hakikisha jina lako liko kwenye orodha hii. Jeshi la Polisi
halitahusika na gharama zozote kwa atakaye kiuka maagizo haya.
 
Source;Mateja20

KILIMO KWANZA KUIKOMBOA TANZANIA RAIS AWA MFANO WA KUIGWA.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa na mjukuu wao Aziza Ridhiwani (3) katika ghala ya mahindi yaliyovunwa kwenye shamba lao kijijini Msoga, nje kidogo ya mji mdogo wa Chalinze, Mkoa wa Pwani. Rais Kikwete ni mkulima na mfugaji kijijini hapo na ameonesha kufurahishwa sana na mavuno makubwa ya mahindi shambani kwake. Hii katika kutekeleza kwa vitendo sera ya Serikali ya kuendeleza kwa ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya sekta ya kilimo katika Tanzania.
 
Source;Mateja20

BILA MILLIONI KUMI SIFANYI MOVIE NA MTU- ROSE NDAUKA



Msanii Rose Ndauka ni mmoja kati nyota wanaofanya vizuri kwenye tasnia ya filamu bongo, ambapo amedai kuwa baada ya kushiriki kwenye filamu nyingi na kuonesha uwezo wake sasa kama kuna mtu anayehitaji kumtumia ndani ya kazi yake basi lazima awe na shilingi milioni 10 cash mbali na hapa itakuwa ngumu kushiriki.
Kiwango cha fedha cha msanii huyo inaonyesha kuwa anajua thamani yake kama msanii mkubwa anayehitaji kuwa lulu ndani ya tasnia hiyo. Baadhi ya filamu alizowahi kung’arisha mwanadada huyu ni pamoja na ‘Because of You’, ‘Love Me Or Love Me Not’ na nyingine nyingi.
Rose alifunguka na kudai kuwa kwa upande wake haoni sababu ya kuficha na kuendelea kuumia, na ndiyo maana ameamua kuweka wazi ishu hiyo kuwa hachezi filamu ya mtu bila muafaka wa kiwango cha fedha alichokitaja.
“Inatakiwa tufikie kipindi wasanii tujue thamani yetu kwani wapo baadhi ya wasanii wengine wana majina makubwa lakini wanafanya filamu kwa bei za chini, lakini siwezi kulaumu kwani kila mtu anafanya kwa mipango yake,” alidai.
Source;Mateja20

Wednesday, August 22, 2012

LIKE FATHER LIKE SON KUMBE NA BABA YAKE KANUMBA MKALI KWA UIGIZAJI NEXT MONTH KUIGIZA MOVIE KUMUENZI KANUMBA.

Imefahamika kwamba baadhi ya wanafamilia wa Marehemu Steven Kanumba mkoani Shinyanga wameshakamilisha mipango ya kucheza movie yao ya kwanza toka watangaze kuanza kuigiza.
Kambini wanaingia tarehe 30 August 2012, movie wanaanza kucheza tarehe 3 septemba inaitwa Nasikia kuitwa ambapo watakaocheza ni mdogo wake Kanumba kwa upande wa baba aitwae Mjanaheri pamoja na baba mzazi ambapo itachezwa hukohuko Shinyanga.
Movie imetungwa na Mwalimu Emanuel Yahewa ambae ni ndio msimamizi wa kikundi cha Taisee art kilichopo chini ya kanisa la AICT Kambarage  ambapo Marehemu ndipo alikua anaimbia kwaya, alijifunzia gitaa na uigizaji hapo hapo.
Nyumbani kwa kina Kanumba Shinyanga.
Mwanzilishi wa kikundi hicho chenye watu 39 ni Mjanaheri Kanumba ambae amesema movie itakua imekamilika ndani ya mwezi mmoja, kampuni inayoitengeneza ni RJ ya Ray Vicent Kigosi lakini director ni Magulu ambae alikua Director wa Kanumba kwa miaka saba lakini kampuni ya Kanumba haitohusika hata kidogo na utengenezaji wa movie hiyo, baba mzazi wa Marehemu Kanumba atashiriki kucheza pia kama kiongozi wa sungusungu.
Stori yake haihusiani sana na maisha ya Kanumba japo mwishoni mwa hiyo movie kuna baadhi ya vitu vyake vitahusishwa, zikiwemo nyimbo na sehemu kidogo ya maisha yake.
.

Source;Millard Ayo

Saturday, August 18, 2012

WEMA AHUSIKA BIFU LA BOB JUNIOUR NA DIAMOND PLATNUMZ.

Ikiwa ni siku chache tu toka diamond abadilishe jina kuepuka makuu na Bob junior bado choko choko za vijana hawa zinazidi kupamba moto. jioni ya jana habari zilizopatikana ni kwamba Bob junior ametangaza kuwa Diamond ameshuka kimuziki hivyo ameamua kutembea na Wema sepetu ili kurudisha jina lake.. baya zaidi amesema kuwa huyo Wema sepetu ni malaya tu so Diamond hajapata lolote... Kisanga kikazidi zaidi baada ya Wema sepetu kujibu shutuma za Bob junior katika kipindi cha movie leo kinachorushwa cloudfm kila asubuhi, Wema anasema" kwanza who is sharobaro??? kwanza hata mazoea naye sina.. why bifu zake za kuime na Diamond aniingize na mimi msichana? au ana wivu na mimi alikuwa anamtaka yeye diamond??

Source;Martin Kadinda

PUSH MOBILE KUSAIDIA WASANII WA TANZANIA KUENJOY JASHO LAO.

KAMPUNI ya Push Mobile Limited imeahidi kuboresha kazi za wanamuziki pamoja na asilimia ya malipo yanayotokana na milio na miito ya simu.


Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Freddie Manento katika mkutano na wanamuziki na wadau wa muziki uliofanyika kwenye hotel ya Serena.


Manento alisema hayo baada ya kuweka bayana mchakato mzima wa mfumo wa biashara ya muziki Tanzania katika mkutano uliohudhuria na wasanii zaidi ya 80 wa muziki wa aina tofauti ikiwa kama injili, bongo fleva, muziki wa dansi, taarab na reggae, hip hop na watayarishaji mbali mbali (producers).


Alisema kuwa kwa sasa Push Mobile inatoa wastani wa asilimia 20 mpaka 40 kwa mwanamuziki pamoja na wadau wao . Alisema kuwa kiwango hicho hutolewa baada ya wao kupokea kutoka kwa mitandao ya simu kati ya asilimia 35 mpaka 60.


“Lengo letu ni kuona wanamuziki wanafaidika na kazi zao hasa kupitia milio na miito ya simu, biashara ambayo kwa sasa imewaingizia kipato kikubwa wanamuziki baada ya kuanguka kwa soko la mauzo ya albamu e na kutopata kipato chochote kutoka kwenye redio na televisheni kama ilivyoelezwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano , Sayansi na Teknolojia wakati anajibu hoja ya Mbunge wa Chadema, Zitto Kabwe,” alisema Manento.


Alisema kuwa asilimia ngapi wataongeza, itatokana na majadiliano na kampuni za mitandao ya simu na hata kama kampuni hizo zitakataa kuongeza ili kuwafaidisha wasanii, wao wataongeza tu.


Alifafanua kuwa kampuni yao imekuwa ikiingia gharama kubwa za kiuendeshaji katika kupromoti nyimbo za wasanii ili kuweza kupata soko.


“Tunatumia si chini ya milioni 25 kwa mwezi kwa ajili ya kuandaa matangazo na kudhamini vipindi katika redio na televisheni kwa ajili ya kupromoti nyimbo za wasanii ili kuweza kupata masoko, pia tunatumia zaidi ya million 7 kwa kazi ya kutengeneza nyimbo ili ziwezwe kuingizwa katika mifumo mbali mbali ya simu za mikononi,” alisema.


Kuhusiana na kuchelewa kwa malipo ya wanamuziki, Manento alisema kuwa tatizo hilo linatokana na ucheleweshwaji wa wadau husika kufanya malipo kwa wakati.


“Push imejitahidi kuondoa tatizo hilo kwa kuwalipa wanamuziki kwa fedha zake huku ikiendelea kudai kutoka kwa wadau husika ambao mara nyingine ukaa miezi sita bila kutulipa, ni changamoto kwetu, lakini tumejitahidi kufikia malengo na kutatua matatizo kwa wasanii, japo changamoto ni kubwa, nawaomba wanamuziki kuelewa tatizo hilo, ” alisema.


Akizungumza katika mkutano huo mtayarishaji maarufu wa muziki nchini, John Water Sharizo au Man Water aliipongeza Push Mobile kwa jitihada zake za kuinua kipato kwa wanamuziki kwani zamani walikuwa wananyonywa sana katika mauzo ya albamu.


Man Water alisema kuwa ni jukumu la Push Mobile ambayo inafanya kazi na wanamuziki wengi hapa nchini kuhakikisha kuwa wateja wake wanapata faida na kazi zao kwani wao ndiyo wameingia mikataba na wanamuziki na wala siyo makampuni ya simu.


Alisema kuwa wanashukuru kwa kipato kilichopo kwani hapo awali walikuwa wanachapisha CD au kaseti 200 na kuuzwa mwaka mzima bila kupata mrahaba kinyume na sasa.


Wanamuziki mbali mbali walihudhuria mkutano huo walifuraishwa sana kwani waliweza kuweka hadharani kero zao mbali mbali na kujibiwa na mkurugenzi huyo na kuridhishwa.

M4C MWANZO MWISHO KILOSA VYAMA VINGINE VYAHAHA>

Moja ya Mikutano ya hadhara ya CHADEMA almaarufu kama M4C uliofanyika RUAHA KILOMBERO katika viwanja vya MANYASINI.
Vuguvugu la M4C linaloongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA limeonekana kutikisa Chama cha Wananchi CUF wilayani Kilosa ambapo mbali ya wanachama wengi wa CUF kujiunga CHADEMA pia Mjumbe wa Mkutano Mkuu CUF Taifa, Bwana Wille Lemi alijitoa rasmi CUF na kukabidhiwa kadi na Kiongozi wa upinzani nchini ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk Wilbroad Slaa.
Katika mkutano huo, Dk Slaa aliwataka wananchi wa vyama vyote kuunganisha nguvu kwa pamoja chini ya vuguvugu la M4C ili kuhakikisha katika uchaguzi mkuu ujao wananchi wanapata serikali itakayojali maslahi yao chini ya CHADEMA.
Dk Slaa pia alishukuru mwitikio wa Wanakilosa kutokana na mkutano huo kufurika umati mkubwa wa watu. Mbali na CUF kupoteza wanachama wengi pia mamia ya wanaCCM walikihama chama chao na kujiunga rasmi CHADEMA kuunganisha nguvu katika vuguvugu la M4C. Idadi ya wanachama wapya waliojiunga CDM katika mkutano wa Kilosa walikuwa zaidi ya elfu moja.
Kilosa ilikuwa ni mojawapo ya maeneo yenye wanachama wengi wa CUF lakini inaonekana ziara ya Dk Slaa imesimika rasmi CHADEMA kama chama kinachopendwa zaidi Kilosa.


Source;Mateja

Friday, August 17, 2012

AIRTEL TANZANIA KUKIMBIZA KOTEKOTE.


Airtel Tanzania, imeendeleza dhamira yake katika kuboresha elimu kwa kuchezesha droo iliyochagua shule za sekondari 93 zitakazo faidika na mradi wa vitabu wa Airtel wa kusaidia jamii unaojulikana kama Airte shule yetu kwa mwaka 2012 -2013 Akiongea katika mkutano na vyombo vya Habari Mkurugenzi wa Airtel Kitengo cha Mawasiliano Bi, Beatrice Singano Mallya alisema "Mwaka huu.


Airtel tunaendelea na dhamira yetu ya kusaidia elimu kwa kuzipatia vitabu shule za sekondari 93, Mradi huu utafaidisha shule 3 kutoka katika kila mkoa Tanzania bara na visiwani.

Shule 93 zilizo chaguliwa leo ni matokeo ya droo iliyochezeshwa na kuzichagua shule hizo kutoka shule 3,000 zilizopendekezwa na Wizara ya Elimu Tanzania kuwa ni shule ambazo zina uhitaji mkubwa wa vitabu na kushauri ziingie katika mpango wa kusaidia jamii wa Airtel shule
yetu.

"Toka tulivyooanza mradi huu wa Vitabu miaka saba iliyopita tumeweza kuzifikia zaidi ya shule 1000 za sekondari zilizopo Tanzania bara na visiwani kwa kutoa msaada sawa kwa mikoa yote na kuwafikia wanafunzi katika kila kona ya Tanzania.

Mwaka huu vitabu tunavyogawa vinakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 110, hivyo kila shule iliyopatikana kwenye droo hii watapata Vitabu alisema Mallya.

Bi Mallya aliongeza kwa kusema "tumefanya kazi kwa pamoja na Mamlaka ya elimu na Wizara ya Elimu Tanzania kwa kuhakikisha kwamba mahitaji ya vitabu kwa shule zote zitakazoingia kwenye Mradi huu wa Shule yetu tunayatimiza kwa kuwapatia vitabu vya mitaala ya masomo yao kama ilivyopendekezwa na Wizara"

"Airtel Tanzania imekuwa mstari wa mbele kwa kutoa misaada mbalimbali ili kuisaidia jamii hapa Tanzania hasa kwa kuchangia sekta ya elimu kwa kuwapatia vitendea kazi vikiwemo Vitabu kwa wanafunzi wa shule za sekondari.

Mwaka jana pia Airtel ilisaidia Vitabu vyenye thamani ya zaidi ya milioni 104 tsh kwa shule za sekondari kwa kupitia droo iliyohusisha jumla ya shule 502" alisema Bi, Mallya.

Nae Afisa Mkuu Mwandamizi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bw Masozi Nyirenda aliongea kwa Niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ulimu (TEA) alisema "Mamlaka ya Elimu Tanzania tunawashukuru sana Airtel kwa dhamira yenu ya kusaidia jamii kwa kuinua kiwango cha elimu hapa nchini " Mradi wa Airtel Shule Yetu ni mradi mzuri sana kwa jamii yetu kwa kuinua kiwango cha elimu na maisha ya watanzania"

Tunaamini elimu ndio ufunguo wa maisha hivyo watanzania wote pamoja na waalimu mtakaopokea vitabu hivi vya mradi wa Airtel Shule yetu tuvitunze na kuvitumia vizuri ili kuunga mkono jitihada za Airtel katika kusaidia kuinua kiwango cha elimu hapa nchini" aliongeza kwa
kusema Bw. Nyirenda

Mbali na shule 93 za sekondari zitakazofaidika na mradi huu wa vitabu mwaka huu, pia Airtel Tanzania imeshamaliza kukarabati shule ya msingi ya Kiromo iliyopo nje kidogo ya jiji la DSM kando kando na barabara ya bagamoyo ilichaguliwa mwaka jana 2011 huku mipango mingine ya mwaka huu ikiendelea ili kupata shule nyingine itakayofaidika kwa kujengwa na kukarabatiwa na Airtel shule Yetu Airtel bado itaendelea kushirikiana wizara ya elimu kwa wadau wengine kuweza kushiriki katika kuinua kiwango cha elimu hapa Tanzania. 



Source;Mateja

MOPAO MOKONZI a.k.a KOFII OLOMIDE MATATANI.

Stori kutoka Kinshasa Congo DRC zimetoa uthibitisho kwamba mwanamuziki maarufu ambae jina lake lina uzito ndani na nje ya Afrika Koffi Olomide, amehukumiwa kwenda jela kwa miaka mitatu au kulipa faini.
Kilichomfanya apigwe hizo nyundo ni fujo alizozifanya akiwa kwenye hoteli moja maarufu Congo DRC pamoja na kumpiga meneja wake.
Nimemsikia mwandishi wa DW kutoka Congo akisema Koffi alikua akitetewa na zaidi ya mawakili 15 ambapo mamia ya mashabiki wake walihudhuria Mahakamani kusikiliza kitatokea nini kwenye kesi yake August 16 2012.
kabla  ya kufikishwa Mahakamani Koffi alikamatwa na polisi August 15 jioni muda mfupi tu baada ya kufanya fujo hizo na kuwekwa kwenye rumande ya mahakama ndogo Kinshasa kutokana na makosa aliyofanya hotelini ikiwa ni pamoja na kumpiga meneja wake ambae amekua akiishi Ulaya.
Mwandishi wa DW amesema ugomvi huo umetokana na Koffi kumdai meneja huyo euro elfu sita ambapo mashahidi kwenye eneo la tukio wamekiri kwamba Koffi alimpiga ngumi meneja wake pamoja na kuvunja mlango wa hoteli.
Hata hivyo meneja huyo aliwasilisha Mahakamani hoja ya kuondoa mashtaka yake dhidi ya Koffi na kupendekeza kuwepo kwa maridhiano kati yao lakini majaji walilipiga chini hilo ombi lake.
Baadhi ya wananchi waliotoa maoni kuhusu hiyo kesi ya Koffi wameunga mkono adhabu hiyo na kusema amezidisha, Ulaya ni yeye na kwengine ni yeye, mwingine amesema ni safi kwa sababu hii sio mara ya kwanza kwa yeye kutenda kosa.
Kutokana na adhabu hiyo kiongozi wa mawakili wanaomtetea Koffi amesema wamepanga kukata rufaa lakini wanasubiri maoni ya Koffi mwenyewe......


Source;Millard Ayo

BANK YA KCB MOROGORO YATOA MSAADA WA MADAWATI.

BENKI ya KCB Tanzania imetoa msaada wa madawati 80 yenye thamani ya shilingi milioni nne na laki nane (4.8m) kwa shule ya msingi Ujirani iliyopo katika kata ya Mkundi manispaa ya Morogoro.


Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya madawati hayo, Meneja wa KCB Tawi la Morogoro Carlos Msigwa alisema kuwa lengo la msaada huo lilikuwa kusaidia upungufu wa madawati katika shule hiyo na hivyo kuwawezesha wanafunzi kusoma vizuri


Meneja huo alisema kuwa Benki ya KCB inatambua umuhimu wa elimu bora katika maendeleo ya taifa na ndiyo maana haikusita kuelekeza msaada huo katika sekta ya elimu.


Akipokea msaada huo, diwani wa kata ya Mkundi Emelda Chambo aliishukuru Banki ya KCB kwa kutoa msaada na kusema kuwa utakuwa chachu kubwa katika maendeleo ya elimu katika shule hiyo ambayo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa madawati.


Tuaishukuru sana KCB kwani wamekuwa kama walezi kwa shule yetu. Hii ni mara ya tatu kupokea msaada baada ya ule wa miti ya kivuli pamoja na vitabu.Tunaahidi kuyatunza madawati haya ili mtakaporudi tena myakute katika hali nzuri.


Mwalimu mkuu wa shule hiyo Philemon Kibuja shule hiyo yenye wanafunzi 400 imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo ukosefu mkubwa wa madawati.


“Mimi ndiyo mwalimu mkuu na mwalimu pekee katika shule hii. Nafundisha kuanzia darasa la kwanza hadi la saba. Shule hii kabla ya kupata msaada huu kutoka KCB haikuwa na dawati hata moja. Wanafunzi walilazimika kukaa chini, kwenye magogo na kwenye mabenchi,’ alisema


Mwalimu huyo aliishukuru Benki ya KCB na kuomba serikali pamoja na makampuni binafsi kuidia shule hiyo ambayo wanafunzi wengi wanatoka katika jamii za wafugaji.


“Shule hii yenye wanafunzi 400 ina madarasa matatu tu na mwalimu ni mimi peke yangu. Pamoja na jitihada kubwa ya kuomba msaada serikalini, serikali haijaweza kutusaidia. Tunaomba mashirika mbalimbali kujitikeza kutusaidia,” alisema

LA "MWANAHALISI" LAHOJIWA BUNGENI.

Kwenye kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri mkuu, Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA alisimama na kumuuliza Waziri mkuu.
Namkariri akiuliza “sheria tunayoizungumzia iiyotumika kulihukumu gazeti la Mwanahalisi ni sheria ambayo imelalamikiwa na wadau wengi wa vyombo vya habari kwa muda mrefu  na ni sheria ambayo inaipa Serikali mamlaka ya ziada kuyadhibiti au bila hata kuyasilikiliza au kuvisikiliza vyombo vya habari pale vinapokua pengine vimeandika taarifa ambazo hazitaipendeza Serikali, madam sheria hii ya msingi ndio imekua tatizo kubwa, wewe huamini Muheshimiwa Waziri mkuu kwamba kutumia sheria mbaya ama sheria kandamizi kunyima haki ni msisitizo wa utawala usio bora?

.
Alichojibu Waziri mkuu ni hiki….. “mimi siamini hivyo muheshimiwa Spika kwa sababu sheria ile imetungwa na bunge lako hili tukufu kwa hiyo ilimradi bado ipo inatumika, ni sheria halali, yaliyomo humo ndio mliosema yako halali kwa hiyo sisi tutaendelea kuitumia mpaka hapo itakapokua imerekebishwa”
Kwenye line nyingine Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema serikali haitoogopa vikwazo vyovyote vitakavyowekwa na nchi wahisani kufuatia kuzisimamisha meli zinazotuhumiwa kupeperusha bendera ya Tanzania wakati asili yake ni Iran.


Source;Millard Ayo

Thursday, August 16, 2012

BIG UP MUSEVENI NAMNA HII MOTISHA INAKUA.

Baada ya kurudi home, Maelfu ya waganda wamempokea Stephen Kiprotich mshindi wa medali ya dhahabu kwenye riadha ya Olympic 2012 ambapo ameifanya Uganda itangazwe mshindi wa medali hiyo baada ya miaka 40.
Kiprotich ambae ni askari magereza alieshinda kwenye mbio za wanaume jumapili iliyopita ndani ya Olypic 2012, amezawadiwa cheki ya dola za kimarekani elfu 80 ambazo zimetolewa na Rais Yoweri Museveni ambae pia amempandisha cheo mara tisa kwenye kazi yake ya uaskari Magereza.
Standard Media wameripoti kwamba mzigo ulikua mzito manake watu walipanga foleni kumpokea Stephen huko Entebbe akiwa amebebwa kwenye gari ambalo lilikua na plate namba iliyoandikwa UG GOLD.

           Hii ndio nyumba aliyokua akiishi Stephen.
Watu walikua wengi mpaka waliziba njia ambapo magari yaliyokua kwenye msafara yalikosa pa kupita wakati yakielekea ikulukumpeleka Stephen kunywa chai asubuhi na Rais Museveni.
Baada ya Kiprotich kupewa cheki yake ya dola elfu 80, alimuomba rais Museveni kuwajengea wazazi wake nyumba kaskazini mashariki mwa Uganda ambapo rais Museveni amekubali kujenga hiyo nyumba ya vyumba vitatu.
Stephen Kiprotich
Kwenye line nyingine ni kwamba rais Museven ameahidi kwamba katika muda ujao, mwanamichezo yoyote wa Uganda atakaeshinda medali ya kimataifa, atakua analipwa shilingi shilingi milioni moja za Uganda kila mwezi.

Source;Millard Ayo

UNYAMA NA UKATILI WANAOFANYIWA WASICHANA.


MWANAFUNZI wa darasa la saba Shule ya Msingi Hogolo, wa umri wa miaka 14 (jina limehifadhiwa) ambaye ni Mkazi wa Mtaa wa Ikulu Kijiji cha Hogolo wilayani Kongwa, mkoani Dodoma ameuawa kwa kunyongwa na kuzikwa kwenye shimo nyuma ya nyumba yao karibu na choo baada ya kubakwa.
Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa chanzo cha mauaji hayo yaliyofanyika Jumamosi iliyopita ni wivu wa kimapenzi kwani marehemu enzi za uhai wake, anadaiwa alikuwa amevunja uhusiano na mpenzi wake wa muda mrefu, Heri Aboubakar na kuanzisha uhusiano mpya na Wilfredy Muhaha maarufu Kabo.
Hata hivyo bado haijafahamika muuaji halisi wa marehemu huyo licha ya polisi kuwashikilia watu kadhaa kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo akiwemo mpenzi wake wa sasa, Muhaha.
Mbali na Muhaha wengine wanaoshikiliwa Polisi ni Ashad Jafari ambaye ni mkulima na mkazi wa Mtaa wa Nyerere Hogolo ambaye ni rafiki wa marehemu na Rino Mazoea, mkulima na mkazi wa Ikulu Hogolo wilayani Kongwa ambaye ni kaka wa marehemu.
Kamanda Zelothe Steven alisema wanamtafuta Aboubakar ambaye amekimbia kijijini hapo na hajulikani alipo mpaka sasa. Katika tukio hilo, kaka wa marehemu ambaye pia anashikiliwa Polisi, katika maelezo yake ya awali alidai kusikia purukushani zikitokea usiku wa tukio hilo la mauaji lakini hakutoka usiku huo kushuhudia nini kinaendelea.
Marehemu alikuwa akiishi na babu na bibi yake hapo kijijini na siku ya tukio , walezi hao, walikuwa wameondoka kwenda katika vijiji vya jirani, ambapo bibi yake alikuwa amekwenda Kongwa kwa ajili ya kujengea makaburi na babu yake alikwenda Kijiji cha Banyi Banyi kutembelea wagonjwa. 



SOurce;HABARI LEO

UPINZANI WAFUNGUKIA MABILLIONI YA VIGOGO "HUU SI WIZI"(USWISSI)

Mh.Zitto Zuberi Kabwe
Kambi rasmi ya upinzani bungeni imesema italazimika kuweka wazi taarifa na majina ya watu wenye umiliki wa fedha katika benki nchini Uswis zinazofikia bilioni 315.5 kama serikali haitatoa hizo taarifa.
Waziri kivuli na msemaji mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni Wizara ya fedha na uchumi Zitto Kabwe amesema hizo fedha zililipwa na makampuni ya utafutaji mafuta na gesi kwenye pwani ya mkoa wa Mtwara, kampuni ambazo zilipewa mikataba kati ya mwaka 2004 na 2006.
Nimemkariri Zitto akiongea bungeni kwamba “kambi rasmi ya upinzani bungeni imepata taarifa kuwa mmoja wa viongozi wa juu kabisa wa Tanzania na baadhi ya mawaziri wa serikali ya awamu zilizopita ni miongoni mwa wamiliki wa fedha hizi, sehemu kubwa ya fedha zililipwa na kampuni za utafutaji wa mafuta na gesi katika pwani ya mkoa wa Mtwara zilizopewa mikataba kati ya mwaka 2004 na 2006, kambi rasmi ya upinzani inaitaka serikali kutoa taarifa rasmi ya hatua gani ambayo imechukua mara baada ya kutolewa kwa taarifa kutoka benki ya taifa ya Uswis, tunaitaka serikali kuliambia taifa hatua itakazochukua kurejesha fedha hizi na nyingine zozote zilizofichwa ughaibuni”
Kuhusu ishu ya mjadala kuhusu kampuni ya BAE system ya Uingereza, Mh Zitto amesema “ukilinganisha fedha iliyorejeshwa kama chenchi ya rada na fedha ambayo Tanzania iliilipa benki ya Barclays, je chenchi ya rada ilikua na thamani yoyote kifedha? mjadala wa ununuzi wa rada hauwezi kuisha kwa kufurahia kurejesha chenchi tu, mjadala huu bado mbichi kabisa kwani tunataka ukweli mtupu uelezwe kwa umma na kuona taifa lilipata hasara kiasi gani kwa ufisadi huu wa kimataifa na hatua stahiki za kisheria kuchukuliwa dhidi ya wote walioliingizia taifa hasara”
Baada ya Zitto Kabwe kumaliza kuwasilisha, Mbunge wa Simanjiro (CCM) Christopher Ole Sendeka aliomba mwongozo kwa spika na kusema “tuhuma hii ni kubwa sana nilitaka kuomba mwongozo wako kwamba nani abebe mzigo huu, ni Zitto ataje majina ya wanaohusika au serikali iwataje hao wanaohusika katika utoroshaji wa fedha hizo ambazo zimeenda ughaibuni ili kila mmoja abebe msalaba wake pale itakapothibitika kwamba fedha za wananchi wa Tanzania zimepelekwa nje ya nchi bila kufata taratibu za kisheria”


Source:Millard Ayo
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitoa wosia kwa wanafunzi 20 waliofanya vizuri katika mitihani ya kidato cha sita kwa mwaka 2012 bungeni leo mjini Dodoma. Wanafunzi hao 10 wasichana na 10 wavulana wamepewa cheti , kopyuta ya pakato (laptop) na fedha taslimu shilingi laki mbili kwa kila mmoja. WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amewataka wanafunzi wote nchini kuwa na nidhamu , kujituma na kufuata maelekezo vizuri ya walimu wao na kuepuka makundi mabaya ili kuweza kupata mafanikio katika masomo yao.

Aidha Waziri Mkuu Pinda amewaasa wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani wa kuhitimu kidato cha sita wa mwaka huu kutumia uhuru vizuri watakaoupata kwenye maisha ya vyuo vya elimu ya juu bila kurudi nyuma katika maendeleo ya masomo yao.

Kauli hiyo ilitolewa leo na Waziri Mkuu, Pinda Bungeni mjini Dodoma kabla ya kuwatunuku vyeti vya kuwapongeza wanafunzi hao 19 kati 20 waliofanya vizuri katika mtihani huo,kutoka shule mbalimbali nchini, ambapo mmoja wao, Jamal Juma yuko nje ya nchi.

Wanafunzi hao ambao wote walipata ufaulu wa daraja la kwanza katika mtihani huo, saba kati yao wanatoka katika shule ya wasichana ya Marian, watatu Mzumbe, wawili Fedha na wengine wawili Kibaha. Waliobakia mmoja mmoja anatoka Kilakala, Ufundi Ifunda, Tabora girls, Tabora boys, Minaki na Mpwapwa.
Mmefanya vizuri. Mnastahili ! Hongereni Sana. Tunataka ufaulu wenu uwe mzuri zaidi kwa vile sasa ninyi mnakweda kujenga weledi. Mnakuwa wataalamu wa fani Fulani. Tumieni muda wenu kujifunza zaidi kutafuta maarifa zaidi na kuvumbua mambo makubwa zaidi yatakayowasaidia ninyi wenywe na jamii kwa ujumla kujiletea maendeleo alisema Waziri Mkuu Pinda.

Aliongeza kuwa ni vizuri utaratibu huo wa kuwatambua wanafunzi bora uwe endelevu na ikiwezekana wapatiwe fursa ya kuendelezwa katika vyuo vikuu vya kipekee nje ya nchi hususan kwenye fani zitakazojenga uwezo kwa taifa

Waziri Mkuu alisema kati ya shule 10 ,ambazo wanafunzi hao wanatoka, wawili ni kutoka shule za kata, ambao ni Ester Marcel toka shule ya sekondari ya wasichana ya Olele Kilimanjaro na Brighton Lema toka shule ya sekondari ya Kitangiri, Mwanza.

Napenda niwape pongezi za pekee wanafunzi hawa kwa jihudi kubwa walizozionesha. Kufaulu kwao kunadhihirisha kwamba shule hizi za kata tukiweka bidii kwa kuziwezesha zaidi zitafanya vizuri zaidi kama ilivyo katika shule nyingine.

Waziri Mkuu pia aliwataka walimu wote nchini kushirikiana na wazazi na serikali kwa pamoja kufundisha watoto kwa bidii ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao kama wanafunzi hao waliotunukiwa vyeti hivyo.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa alisema wanafunzi hao watazawadiwa pakato (laptop) na sh. 200,000, pia kila shule iliyotoa mwanafunzi bora itazawadiwa sh. milioni moja katika hafla maalum itakayofanyika jioni.

Wanafunzi hao wanatoka katika mchepuo wa PCM ambao ni 16 na mmojammoja toka mchepuo wa PGM, CBA, ECA na HKL.

Naye Spika wa Bunge la Jamhuri, Anna Makinda aliwataka wanafunzi hao kuwa makini na makundi kwa kuyasilikiza huku wakitumia akili zao huku akitoa changamoto shule nyingine kujitahidi kufanya vizuri.

Wanafunzi 20 waliofanya vizuri katika mitihani wa kidato cha sita kwa mwaka 2012 wakiwa katika picha ya pamoja nje ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma. Wanafunzi hao 10 wasichana na 10 wavulana wamepewa cheti na Waziri Mkuu, kopyuta ya pakato (laptop) na fedha taslimu shilingi laki mbili kwa kila mmoja.






T.O namba mbili Tanzania Zawadi Mdoe(mwenye t shirt ya kijani),nilibahatika kusoma nae o level.

Waziri Mkuu Mh.Mizengo Pinda
source:Mateja

Wednesday, August 15, 2012

WENJE AFUNGUKA MAGUMASHU ELIMU YA BONGO.



Mbunge wa Nyamagana Mwanza kwa ruhusa ya Chadema na wananchi wa jimbo lake Ezekiah Wenje amewataka wabunge wa bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kuacha unafiki na badala yake waitishe mjadala wa kitaifa kuhusu lugha maalum ya kufundishia kwa shule za msingi.
Namkariri akisema “lugha kwenye primary school ni Kiingereza au kiswahili? mimi nawachallenge acheni unafiki, kama ni Kiswahili iwe Kiswahili kwenye primary School kama ni Kiingereza basi na hizo shule za Serikali zifundishe kiingereza ili wanafunzi wapate hiyo Knowledge ya kiingereza, wanafunzi wa watu masikini pia wapate kama watoto wenu wanavyopata”
Akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya wizara ya Elimu, Wenje amesema wakati wabunge wakipigia debe matumizi ya kiswahili wenyewe pia wamekua wakisomesha watoto wao kwenye shule zinazotumia lugha ya kiingereza
.

source:Millard Ayo

Tuesday, August 14, 2012

KILOMBERO CHADEMA YAFUNGA KAZI.


Add caption


Katibu mkuu wa CHADEMA akiwahutubia wafuasi waliofurika  Ruaha,Kilombero




BIASHARA INAYODHARAULIKA TANZANIA YENYE KIPATO KIKUBWA SANA.


 Utengenezaji wa katuni ama kwa kiswahili VIKARAGOSI ni moja kati ya biashara ambazo zina vipato vikubwa sana ingawaje muamko wake kwa nchi maskini kama Tanzania bado uko chini sana.
Hilo linaweza kujidhihirisha kwa swali moja dogo sana ambalo ni nani kati yetu ambae hajawahi kuiona katuni ya KIRIKOU?! jibu liko wazi kabisa kwamba hakuna ambae hajawahi kuiona sasa jiulize ni shillingi ngapi alipata muandaaji wa katuni hio ukiondoa PIRACY yaani unyonyaji usio halali??

CHADEMA KUWASHA MOTO RUAHA KILOMBERO LEO


Chama cha Demokrasia na Maendeleo leo hii tarehe 14 August wanatarajia kufanya mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya manyasini ambapo Dk.Wilbrod Slaa anatarajiwa kuwahutubia wananchi ikiwa ni pamoja na kupokea wanachama wapya,pia ikiwa ni moja na mikutano ya vugu vugu la mabadiliko yaani M4C ikiwa na kauli mbiu ya VUA GAMBA NA VAA GWANDA>
TUJIKUMBUSHE:
Mapema mwezi wa tano mwaka huu zilizuka vurugu katika uchaguzi mdogo wa kijiji ambao uliwahusisha wanachama wa CCM na CHADEMA.