ushauri

Fay Pub

Fay Pub
Fay Pub Sinza,We Rock,it is a good place to be cool and usalama wa kutosha!!Fay Pub ipo Sinza kumekucha,nyuma ya Seven Up kama unaelekea shamool Hotel,, kwa maelekezo piga namba 0715 556453

tangaza

Tuesday, September 11, 2012

MKE WA OBAMA MICHELLE OBAMA ATOA SUPPORT KWA MUMEWE BARACK OBAMA KWA UCHAGUZI UJAO.

Mke wa rais wa Marakeni Barack Obama, Michelle Obama amemuunga mkono mumewe katika mkutano mkuu wa chama cha Democratic akiomba rais huyo apewe muda zaidi.

Bibi Obama amekiri kuwa mabadiliko ambayo mumewe Barack Obama aliahidi wakati wa kampeini ya wadhifa wa urais miaka minne iliyopita hayajatwa kikamilifu lakini akawaomba wapiga kura kumpa miaka mingine minne ili kuuimarisha uchumi wa Marekani unaoyumbayumba.

Michelle Obama ndiye aliyekuwa wa kwanza kumtetea mumewe katika siku ya kwanza ya mkutano huo wa siku tatu ambao utakamilika kwa hotuba ya Obama kesho Alhamisi ili kukubali uteuzi wa chama cha Democratic wa kupambana na Mitt Romney katika uchaguzi wa uraisi tarehe sita Novemba.

Bibi Obama alisema "Kama rais, utapata ushauri wa kila aina kutoka kwa watu tofauti, lakini unapohitajika kufanya uamuzi wako kama rais, kinachokuongoza ni maadili na maono yako pamoja na uzoefu wa maisha, mambo yanayokufanya uwe jinsi ulivyo"

Katika kinyang'anyiro ambacho ni kikali kutabiri zikiwa zimebaki wiki tisa kabla ya Wamerakani kupiga kura, Obama anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mgombea wa Republican Mitt Romney kwa sababu ya kudorora uchumi pamoja na asilimia 8.3 ya ukosefu wa ajira.
 


Source;Machibya

No comments:

Post a Comment