ushauri

Fay Pub

Fay Pub
Fay Pub Sinza,We Rock,it is a good place to be cool and usalama wa kutosha!!Fay Pub ipo Sinza kumekucha,nyuma ya Seven Up kama unaelekea shamool Hotel,, kwa maelekezo piga namba 0715 556453

tangaza

Wednesday, September 12, 2012

KALAPINA AFUNGUKA KWAMBA PROF.JAY ANAPOTEA KWENYE RAMANI YA MUZIKI.

Msanii wa hiphop Kalapina wa kikosi cha Mizinga amekubali kutaja majina ya wasanii wa hiphop anaosikiliza muziki wao kwa sasa hapa Tanzania.

Namkariri akisema “Tanzania mimi nasikiliza wasanii wote niangalie vitu wanavyovifanya lakini wasanii wengi hawako real wanafake, sasa hivi nimekua nikiwasikiliza wadogo zangu Lunduno, Nash Mc, Fid Q, Mansu Lee, Rado… mzee mwenzangu Profesa J amepotea sasa hivi, nilikua namsikiliza lakini sasa hivi amepotea”



“Profesa J amefikia hatua anafanya video za dada zetu wako uchi kabisa na ule ni udhalilishaji wa kijinsia kama atabisha si udhalilishaji, achukue video awachukue dada zake na mama zake wadogo awavalishe vichupi na sidiria tutaona kweli yeye ni mmagharibi lakini kama anachukua dada za watu huu ni udhalilishaji wa kijinsia mi napinga mambo kama yale, tusifikie huko sasa hivi huwezi kufanya video kali mpaka uweke wanawake wako uchi Tanzania” – Kalapina

Source;Millard Ayo

UNAMJUA R.O.M.A??HUYU HAPA.

Anaitwa Ibrahimu mwenyeji wa Tanga aliekulia Dar,

ROMA ni kifupi cha Rhymes Of Magic Attraction
Yeye ni mtoto wa mwisho(kitinda mimba) kutoka katika familia ya watoto 5.

Kwa imani,Yes ni kweli kwamba yeye ni mkristo wa madhehebu ya Roman Catholic
Hivi sasa yeye ndio anashikilia tuzo ya Kilimanjaro ya  msanii bora wa Hip Hop nchini Tanzania.

sOURCE; BongoCelebrity

KILICHOFIKIWA NA WAANDISHI BAADA YA MAANDAMANO.

Jukwaa la Wahariri Tanzania pamoja na waandishi wa habari waliungana na kufanya maandamano kuanzia mkao makuu ya kituo cha Television cha Channel Ten mpaka kwenye viwanja vya Jangwani Dar es salaam september 11 kupinga mauaji ya mwandishi wa habari Daudi Mwangosi alieuwawa kwa kulipukiwa na bomu akiwa mikononi mwa polisi Iringa wakati polisi walipokua wakiwatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na maendeleo.

Mjumbe wa jukwaa la wahariri kutoka Zanzibar Masoud Sanani kwenye maandamano hayo Jangwani  alitangaza maazimio yaliyofikiwa na washiriki wa maandamano hayo, namkariri akisema “kwa siku 40 hizi za maombolezo tusiandike habari ya polisi, polisi hata akifanya kitu gani tusiandike, wataandika kwenye gazeti lao la polisi wanalo”


sOURCE;Millard Ayo

VODACOM YADHAMINI LIGI KUU KWA MIAKA 3.

Vodacom na TFF zasaini mkataba wa udhamini wa ligi kuu kwa miaka mitatu
Klabu ya Simba Sports Club ndio bingwa mtetezi.

Msimu wa ligi kuanza Septemba 15, na kushirikisha timu 14.

Polisi Morogoro, Tanzania Prisons na Mgambo JKT ni timu mpya katika ligi.


Dar es Salaam, 11 Septemba 2012. Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) leo limeingia katika mkataba wa udhamini kutoka kwa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, wakati maandalizi ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania yakielekea ukingoni.


Kampuni ya Vodacom imekuwa mdhamini wa ligi kuu kwa miaka mitano iliyopita, na sasa imeingia mkataba mpya wa udhamini kwa miaka mitatu na TFF, mkataba utakao liwezesha shirikisho hilo kupoea fedha za udhamini kwa miaka mitatu.


Ligi kuu ya Vodacom itaanza tarehe 15 ya mwezi huu, ikitarajia kushuhudia michezo 182 ikichezwa katika viwanja mbalimbali na kushirikisha timu 14, zikiwemo timu za Dar es Salaam Young Africans, Kagera Sugar na Simba Sports Club ambaye ndie bingwa mtetetzi wa kombe hilo. 


source;Mateja20 

Tuesday, September 11, 2012

STEVE WA RnB AREJEA BONGO TOKA ULAYA ALIKOKAA KWA MIEZI 6.


MSANII Steve R&B ambaye alitamba na ngoma kibao ikiwemo ‘One Love’, aliyomshirikisha Baby Boy, sasa amefunguka na kuzungumza na blog hii, kuwa kitu kilichomfanya kuwa kimya ni kutokana na safari ndefu aliyokuwa nayo ya kimuziki nchi za Ulaya iliyodumu kwa takribani miezi sita.


Steve
alisema kuwa katika safari hiyo alifanya show katika nchi nyingi kama Germany, Italy, Australia na Swaziland, ambako kote alifanya makamuzi ya hatari kwa ajili ya katangaza jina lake pamoja na taifa lake kwa ujumla.


Hata hivyo alisema kuwa anaamini mashabiki wake watakuwa wamemisi vitu vyake, na katika hilo anadai kuwa sasa amekuja na staili mpya ujio kwa ajili ya kuonesha kile alikifanya nje kwa miezi hiyo sita.


Aliongeza kuwa baada ya kurudi kuna ngoma ambayo ameshaifanya na inakaribia kwenda sokoni ambayo inakwenda kwa jina la
‘Radio’ ambayo ndani yake anapatikana Ommy Dimpoz.

“Mashabiki wangu wanaweza kusema nilikuwa kimya sana, kama unavyojua kila mtu anazungumza analojua, lakini ukweli ni kwamba nilikuwa kimya kwa sababu nilikuwa Ulaya ambapo nilienda kwa ajili ya show,”
alisema.

Source;DarTalk

BENJAMINI WA MAMBO JAMBO KURELEASE NGOMA MPYA BY THE NAME OF SKENDO.

MSANII anayepagawisha mashabiki wengi kutokana na sauti yake ‘Benjamini wa Mambo Jambo’, ameiambia blog hii, kuwa anatarajia kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Skendo’, ambayo itazungumzia namna watu wanavyitengenezea skendo kwa lengo la kujipatia umaarufu usiyo na maana.

Alisema kuwa ngoma hiyo inakuja hivi soon na ipo katika mtiririko mzuri wa mashairi pamoja na ujumbe wake, kitu ambacho kinaashiria kuwa itafanya vizuri kwani kwa upande wake si msanii ambaye anatoa ngoma kila baada ya wiki mbili.


Msanii huyo aliwahi kutamba sana na ngoma ya yake ya 
‘My Friend’, ambayo inazungumzia mambo mengi ya maisha na njisi ndugu yako anavyoweza kukumaliza kwa ajili ya pesa au kutaka kuwa juu ya yako.


“Mimi si msanii ambaye anatoa ngoma kila baada ya wiki kwani najua kusoma alama za nyakati hivyo napokuwa kimya huwa natafakari ni namna gani naweza kutoa kitu kizuri kwa ajili ya mashabiki wangu,”
alisema.

Hata hivyo sasa msanii huyo ana kampuni yake ya kutengeneza video inayoitwa
Promo Only ambapo pia matarajiao yake ni kuwa na kampuni kubwa zaidi ya atakayoipa jina la B.M.L, ambayo itahusika zaidi na video pamoja na audio.



Source;DarTalk

MKE WA OBAMA MICHELLE OBAMA ATOA SUPPORT KWA MUMEWE BARACK OBAMA KWA UCHAGUZI UJAO.

Mke wa rais wa Marakeni Barack Obama, Michelle Obama amemuunga mkono mumewe katika mkutano mkuu wa chama cha Democratic akiomba rais huyo apewe muda zaidi.

Bibi Obama amekiri kuwa mabadiliko ambayo mumewe Barack Obama aliahidi wakati wa kampeini ya wadhifa wa urais miaka minne iliyopita hayajatwa kikamilifu lakini akawaomba wapiga kura kumpa miaka mingine minne ili kuuimarisha uchumi wa Marekani unaoyumbayumba.

Michelle Obama ndiye aliyekuwa wa kwanza kumtetea mumewe katika siku ya kwanza ya mkutano huo wa siku tatu ambao utakamilika kwa hotuba ya Obama kesho Alhamisi ili kukubali uteuzi wa chama cha Democratic wa kupambana na Mitt Romney katika uchaguzi wa uraisi tarehe sita Novemba.

Bibi Obama alisema "Kama rais, utapata ushauri wa kila aina kutoka kwa watu tofauti, lakini unapohitajika kufanya uamuzi wako kama rais, kinachokuongoza ni maadili na maono yako pamoja na uzoefu wa maisha, mambo yanayokufanya uwe jinsi ulivyo"

Katika kinyang'anyiro ambacho ni kikali kutabiri zikiwa zimebaki wiki tisa kabla ya Wamerakani kupiga kura, Obama anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mgombea wa Republican Mitt Romney kwa sababu ya kudorora uchumi pamoja na asilimia 8.3 ya ukosefu wa ajira.
 


Source;Machibya

KALAPINA WA KIKOSI CHA MIZINGA AIGIZA MOVIE JUU YA MAISHA YA DK.ULIMBOKA.

Kamanda mkuu wa kikosi cha Mizinga, msanii wa Hiphop Kalapina mwishoni mwa mwaka huu ndio amepanga kuitoa na imfikie kila Mtanzania, movie mpya ambayo ameigiza kama kiongozi wa Madaktari Dr Ulimboka ambae siku kadhaa zilizopita alitekwa na kupigwa sana na wasiojulikana.

Pamoja na kwamba kwa sasa kuna stori za chinichini kwamba Dr Ulimboka ameondoka Tanzania kutokana na kuhofia usalama wake, Kalapina anaamini Dr Ulimboka hana haja ya kukimbia nchi kutokana na kuhofia usalama wake.

Namkariri Kalapina akisema “ninachoweza kumshauri Dr Ulimboka asiogope, watu wapo kama anahitaji kupewa ulinzi Kikosi cha mizinga tupo fiti kila idara na tuna kitengo cha kikosi kinaitwa Department of defence (DOD) kitengo cha ulinzi, kuna vijana wamefuzu mafunzo wanaweza kumlinda mtu yoyote, wanakodishwa kwa gharama nafuu tu kama unahitaji walinzi unaweza ukaniona, walinzi wa kulinda kumbi za disco na sehemu nyingine pia, kama anahitaji atapata kwa gharama nafuu”
Kuhusu hiyo movie mpya Kalapina atakayoigiza maisha ya Dr Ulimboka, amesema “nitajaribu kuonyesha tokea anarudi kutoka masomoni, harakati zake mpaka anaanza kazi, harakati za kutetea madaktari wenzake mpaka anapelekea kutekwa na kutupwa msituni, hii yote ni kuionyesha tasnia ya filamu kwamba tuna vitu vingi vya kuonyesha lakini nashangaa zimejaa filamu za ngono na filamu za upotoshaji”



source;Millard Ayo

NMB NA MPANGO WA FINANCIAL FITNESS KUSAIDIA ELIMU YA TANZANIA.

Benki ya NMB imewafikia wanafunzi 45,000 wa shule za msingi katika mpango wake wa kukuza uelewa wa maswala ya kifedha uitwao NMB Financial Fitness. Mpango huo ulioanzishwa mwezi Mei mwaka huu, una lengo la kuwahamasisha wanafunzi kujiwekea akiba kwa kutumia huduma za kibenki wanapokua wakubwa. 

Akizungumza katika utambulisho huo, mwanafunzi wa shule ya Liwale iliyopo mkoani Lindi Idrissa Ndumbaro aliishukuru benki ya NMB kwa elimu hiyo ambayo baadae itamwezesha kuwa na uelewa wa matumizi mazuri ya fedha pamoja na kujiwekea akiba.


Source;Mjengwa

MAGESE AWAKALISHA WAMAREKANI HADI MBUNIFU WA MICHELLE OBAMA.

Mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Happines Millen Magese ameshiriki Wiki ya Mitindo ya Mavazi ya New York nchini Marekani juzi. 

Onyesho hilo lilishuhudiwa na nyota wakubwa kama mwanasoka David Beckham huku wabunifu wakubwa duniani wakishiriki kuonyesha mitindo yao ya mavazi kama Tommy Hilfiger, Carolina Herrera, Michael Kors, Ralph Lauren na mwanamama Tracy Reese, ambaye gauni lake lilivaliwa na mke wa rais wa Marekani, Michelle Obama katika Kongamano la Kitaifa Chama cha Democratic. Mwanamitindo maarufu Naomi Campbell pia alipita stejini kuonyesha mitindo.


Source;Straika

Monday, September 10, 2012

MARAFIKI ZANGU WA FACEBOOK WENYE BIRTHDAYZ ZAO LEO.

Friendship is not something that is written on paper, because paper can be torn. It is neither something that can be written on a rock, for even a rock can break. But it is written on the heart of a person, and it stays there forever. Birthday wishes and blessings are coming your way, my friend!

Godwin Zephrin
sOURCE:my facebook profile by the name of Fredy Seventeeneleven

Sunday, September 9, 2012

J MARTINS AFATA NYAYO ZA P SQUARE APIGA COLLABO NA PITBULL.



Mpaka sasa Nigeria inaongoza kwa idadi ya vijana wake kufanya kolabo na mastaa wa muziki wa dunia kutokea Marekani pamoja na kupata deals, mfano ni kwa kolabo waliyoifanya P Square na rapper Rick Ross pia kolabo yao na Akon lakini pia Dbanj ambae yuko chini ya lebo ya Kanye West.

Naomba kukufahamisha kwamba kolabo inayofata sasa hivi ni ya Producer/msanii J Martins ambapo tayari ameshairekodi na Cuban American Rapper Pitbull na mpaka sasa jina la kolabo yenyewe halijatajwa.
 
Kingine ambacho unapaswa kufahamu ni kwamba wiki chache zijazo ndio video itafanyika kwenye mji wa Amsterdam ambapo stori kamili ziLISEMA kwamba ni hit ambayo Pitbull amelenga kupanua zaidi soko lake ambalo kwa sasa ni USA na Latin America na J Martins pia anataka kuvuka boda na kwenda umbali mrefu.

Bado haijawekwa wazi jamaa walikutanaje mpaka akakubaliwa kolabo lakini kolabo hiyo itamsogeza sana J Martins kwa sababu Pitbull ni staa ambae ameshine kwenye nyimbo zake na hata kolabo nyingi alizofanya na wakali kama J.Lo na Ne-yo.

Source;Millard Ayo

DOGO JANJA AKIWA NA CREW NZIMA YA MTANASHATI YA USTAZI JUMA NA MUSOMA KUKAMUA LEO BILLZ KATIKA UZINDUZI WA KUNDI.

KUNDI la burudani ya muziki wa kizazi kipya la ‘Mtanashati’  linatarajia kufanya uzinduzi  wake mpya katika Ukumbi wa Club Billicanas, uliopo katikati ya Jiji la Dar es salaam, eneo la Posta.

Akizungumzia uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa  ‘Mtanashati Entertainment’ Ostaz Juma na musoma, alisema tayari maandalizi ya uzinduzi huo yamekamila na kuongeza kuwa kinachosubiriwa ni muda ili kuwadhihirishia kile kilichokusudiwa.

Alisema katika uzinduzi huo utakaotumika pia kwa ajili ya kuwatambulisha upya wasanii wote watano wanaounda kundi hilo wakati huu ambao wanaendelea kujihimarisha kimuziki ambapo pia amewaomba wapenzi wa burudani kujitokeza kwa wingi kushuhudia uzinduzi huo.

Alisema katika kupamba siku hiyo, ukiacha burudani kutoka kwa wasanii hao, pia kutashushwa  disco la nguvu hadi kunapokucha na maarufu ‘DJ Ibra’ huku akisisitiza kuwa  ‘usiku wa leo utakuwa moto wa kuotea mbali’.

“Baada ya Mtanashati kuporomosha burudani wiki iliyopita katika ukumbi wa Maisha Club, wiki hii kazi inahamia Billicanas’ bila shaka watu wote walioudhuria burudani ya pale Maisha wanakumbukumbu nzuri juu ya burudani ya nguvu iliyofanywa na Dogo Janja na PNC, burudani ya leo ni zaidi ya ile ya Maisha” alisisitiza Ostaz Juma na musoma.

Alisema katika uzinduzi huo, kundi hilo litapiga nyimbo mbalimbali zikiwemo mpya pamoja na zile zinazoendelea kutamba katika vituo mbalimbali vya redio na televisheni  'Ya Moyoni' 'Checherumba'  ‘watasubiri’ na zinginezo zikitarajiwa kutumbuizwa katika uzinduzi huo.

Mtanashati ni kundi linaloundwa na wasanii watano  ambao ni Dogo Janja, Amazon, Y-Fil, PNC, Happy Balice ndani ya familia ya ‘Moja ya Muziki’ iliyopewa jina la ‘MTANASHATI ENTERTAINMENT’ chini ya Mkurugenzi wake Mkuu ‘Ostaz Juma na musoma’ ambaye kwa mujibu wake malengo makubwa ya kuanzishwa  ‘Mtanashati’  kumekusudia  mapinduzi mapya katika tasnia  ya Muziki wa Kizazi kipya.
Wakati huo huo habari zilizonifikia sasa hivi kupitia account yamgu ya BBM toka kwa dogo Janja zinasema ustaz Juma na Musoma amepata mtoto wa kiume toka kwa mke wake leo hii majira ya mchana.


Source;Kajuna son & Dogo Janja

WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARY ZA MOROGORO JIANDAENI KWA BATA ZA MWSHO KABLA YA NECTA.

Next level barber shop wanakuletea bonge la party ya mwisho before necta yaani ni full kurelease STRESS

Shavu kubwa limetoka kwa mratibu wa party hiyo Mchopi S Nyaa......namba 0654603503 kwa maswai na booking mcheck kihivo hapo.

MWASITI KUREKODI NGOMA MPYA KWA PRODUCER MMAREKANI.

Mwasiti ambae kwa sasa anafanya vizuri sana na pini lake MAPITO, ametoa info kuwa kwa sasa amefanya ngoma na producer mkubwa marekani anaeitwa Hakeem.

Producer Hakeem ameshatengeneza ngoma ya Akon (i wanna be with you),ngoma ya Youssundou na nyingine kibao."Nimefanya nae ngoma mbili moja ikizungumzia wanawake na matatizo yanayowakuta, ila ya pili ipo kibongo fleva zaidi, nimefurahi sana na naiheshimu sana kazi yangu." amesema Mwasiti.



Source;Dj Fetty

FID AWAFUNGUA MACHO WATANZANIA BAADA YA ORIJINO KOMEDI KUMDIS.

Siku tatu baada ya Fid Q kutuhumiwa na orijino komedi kwa kukopy na kupesti wimbo wake wa danger kutoka kwa msanii wa marekani,leo hii amezungumza na kusema kuwa jamaa aliechana kwenye beat hiyo ni mwizi.

"ametuibia sisi yaani mimi na producer choba..mwanzoni aliomba kuitumia lakini alishindwa kuilipia akaingia mitini.. ndio maana ni msanii ambae hapatikani twitter, facebook na wala hana website na yeyote atakaekuwa na info zake atuambie maana wenyewe tunamtafuta"


 Fid Q hakuishia hapo aliendelea na kusema kuwa, tusione mtu mweupe tukadhani yeye ndio originator wa kitu flani...na kuzungumzia kuhusu wimbo wake wa sihitaji marafiki kuridiwa na mmarekani anaeitwa Benjamin kutoka Filladelfia Marekani, ambae ameomba kufanya hivyo...




Source;Dj Fetty

MARAFIKI ZANGU WA FACEBOOK WENYE BIRTHDAYZ ZAO LEO

I'm so blessed 2 have a friend like u this comes with many loving thoughts & warm wishes i send 2o may ur day be filled with laughter on this ur special day & may the finest things in life always come ur way happy birthday!
Colman Kibo
 With lots of love, this message comes 2 say u're wished the joys u so deserve especially 2day..... & may the days that lie ahead be extra-nice 1, 2o, filled with all the happiness thought 2 come 2 u. !! happy birthday !!
Leah Enock
Source;My facebook account by the name of Fredy Seventeeneleven

P SQUARE KUSHTAKIWA KWA KUMZINGUA MAY DEE WA CHOP MY MONEY.

Unakumbuka ile kolabo ya P Square na Akon inaitwa Chop my money ambayo ilimfanya May D kuwa staa zaidi baada ya kuongezwa kuwa mtu wa nne kusikika kwenye hiyo single?
kama hufahamu May D ni msanii wa Nigeria ambae alisainiwa kuwa chini ya lebo inayomilikiwa na P Square (Square Records) ambapo ni siku kadhaa zimepita toka lebo hiyo itangaze kwamba haimuhitaji tena na wala hayuko tena chini yao.

Leo mtandao wa Naijag umeripoti kwamba May D ambae alitimuliwa na lebo hiyo wiki kadhaa zilizopita yuko kwenye hatua za mwisho za mazungumzo na wanasheria wake ili awashitaki P Square kwa kuvunja mkataba kiholela.

May D anasema taarifa za kutimuliwa kwake alizipata kwenye blogs na magazeti kama walivyopata watu wengine na kwamba hakupewa taarifa zozote za kiofisi kama inavyopaswa, hiyo ndio sababu inayomfanya awashitaki P Square akiwemo kaka yao mkubwa Jude Okoye ambae ndio alitangaza kuuvunja mkataba wa May D.



Source;Millard Ayo

Saturday, September 8, 2012

KARDINALI RUGAMBWA KUZIKWA TENA KANISA KUU LA BUKOBA.

Kanisa katoliki nchini dayosisi ya Bukoba mkoani Kagera, wanajiandaa kuzika upya masalia ya mwili wa aliyekuwa askofu wa dayosisi hiyo Kardinali Laurean Rugambwa, aliyefariki mnamo mwaka 1997 katika kanisa kuu la Bukoba.

Maziko ya Kadinali Rugambwa yamepangwa kufanyika siku ya oktoba 6 mwaka huu. Mwili wa askofu huyo wa kwanza nchini na Kardinali wa kwanza mweusi barani Afrika umezikwa katika kanisa la kwanza mkoani Kagera lililopo Kashozi kutokana na kwamba kanisa kuu la Bukoba ambalo marehemu aliagiza kuzikiwa ndani yake lilikuwa katika matengenezo makubwa.

 Akizungumza katika kipindi cha Baragumu Channel ten na baadaye kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Askofu msaidizi wa Jimbo la Bukoba Askofu Methodius Kilaini , amesema wanataka kumzika kardinali Rugambwa kwa heshima tena katika kanisa alilopenda kuzikiwa kutokana na kukamilika kwake, lakini kabla ya kuzikwa humo kutatanguliwa na ibada mbalimbali ikiwa sehemu alikozaliwa, alikobatizwa, sherehe zitakazoambatana na kusherehekea miaka 100 ya kuzaliwa kwa kardinali Rugambwa tarehe 7 mwezi Octoba.

 "tuna alika watu wengi kuhudhuria kwenye tukio hili..., na pia tunakaribisha michango itakayowezesha kuwa na kitu cha kumkumbuka marehemu kwa mchango wake.... alisema askofu Kilaini. Naye mmoja wa wajumbe wa kamati ya maandalizi ya kufanikisha tukio hilo , James Rugemalira, alimwelezea Kardinali Rugambwa kama mtu aliyetoa mchango mkubwa kwenye jamii ya watanzania, kuanzia kwenye nyanja za elimu, afya na kiroho.

 Marehemu Kardinali Rugambwa ana mambo mengi ya kukumbukwa na jamii ya watanzania hususani watu wa mkoa wa Kagera hasa kwa juhudi zake za kupeleka elimu mkoani humo kwa kuagiza ujengwaji wa shule za msingi na sekondari ikiwemo shule ya kwanza ya wasichana ya Rugambwa ambayo ujenzi wake ulikuwa ni mafanikio ya marehemu huyo kuomba msaada wa ujenzi wa shule hiyo alipohutubia bunge la Ujerumani akiwa mwafrika wa kwanza.

 Licha ya mambo hayo yote kanisa hilo pia liko mbioni kuanzisha mfuko rasmi wa kumuenzi kardinali huyo mfuko utakaojulikana kwa jina la Kardinali Rugambwa ambao utakuwa maalumu kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali za kijamii.

 Padre Laurean Rugambwa aliwekwa wakfu kuwa Askofu tarehe 10 Februari,1952. Alizaliwa julai 22 1912 na kufariki miaka 15 iliyopita.

Source;kajunason

T.I.D MNYAMA AWA MBOGO BAADA YA KUPEWA MAKAVU NA SHABIKI `AKE KUNAKO MAFACEBONGA.

Top in Dar, TID leo amejikuta akizunguana vibaya na shabiki wake wa kike kwenye Facebook.

Picha lilianza baada ya TID kuandika status inayosema, “Am tha Guy who did tha song KIUNO which is currently the No.1 song in the Country I only do Killer tracks that kill people but I don't kill people..........”


Status hiyo ilimkera msichana aitwaye Happiness ‘Cutegal’ Ignas ambaye aliamua kumpa live TID.


“But stop being arrogant! U luk like a fool b4 pipo! We love ur music bt too rude thus y u NEVER get further! Kama unamfwatilia hata interview TID is rude n too emotional.”


“Don’t get upset she is jus a loozer am the winner keep me posted mnyama mkali, “alijibu TID.


“She doesn't knw me @all she wants to be famous don't worry am not allow them to reach this far,let me block the groupy!”


Majibu ya TID yalimpandisha morali Happiness aliyeamua kufunguka zaidi.



Happiness Cute aliempa makavu T.I.D
“hehehe!! Whatever u talk! Ur a fuck a mean!! A fool callin himself a winner!! Wonders shld neva end! Whaat! Want to be famous?? Hahaha see how zero brain ur! Dnt b twisted hia! It was just a piece of advice, or watever u cal urself! Watch ur smelln mouth!! Nonsense of highest degree."

Aliendelea kufunguka zaidi, “tatizo sio humanity error, TID anajua kuimba, anajua kucheza, anajua kuvaa lakini hajui ku create gud image, hapendi ushauri, 2sipomwambia sisi atamwambia nani? TID angetakiwa kuwa mbali sasa, sio kuwa dominant, y ameanza mziki long bt he stil da xme! Y?? Aache kujisikia bwana.

Ulishamwona T.ID anafanya interview?? As if anaimbia na cash money, as if he has gained!! Unajua kuna mtu waweza mtazama ukamhesabu kwenye mazuri bt kumbe sivyo, TID z arrogant, rude n mean!!!”



sOURCE;Bongoflavatz

KANYE AIMBA SKENDO YA PORNO KIM NA RAY J KWENYE NYIMBO YAKE.

 Kwenye wimbo mpya wa Kanye West unao itwa Clique kuna kipande cha mistari kinachozungumzia skendal kati ya mpenzi wake wa sasa Kim Kardashian na Ray J, Kim na Ray J walikuwa wapenzi zamani na Sex tape yao ilivuja mtandaoni..
Kanye spits:

Break records of Louie

Ate breakfast at Gucci
My girl a superstar all from a home movie
Bow on our arrival the unamerican idols
When them niggas in Paris got em hanging off the Eiffel
Yeah I'm talking business
We talking CIA
I'm talking George Tenet
I seem him the other day
He asked me about my Maybach
Think he had the same
Except mine tinted and his might have been rented
You know white people get money don't spend it
Or maybe they get money, buy business


sOURCE;Bongoflavatz

RAFIKI ZANGU WA FACEBOOK WENYE BIRTHDAYZ ZAO LEO SEPT.8

How do you expect me to remember your birthday, when you never look any older? happy birthday!

Anna Mapunda-Dar
 Its another day 4 u. God picked another petals on your flower, wishing your flowers may bloom for year.

Mise Chikoma-Mbeya
 I send to you warm wishes,that your happiness will be as wonderful as the happiness, you have always given me. wish you happy birthday.



Peter Samson-Arusha
sOURCE:facebook via my account Fredy Seventeeneleven