ushauri

Fay Pub

Fay Pub
Fay Pub Sinza,We Rock,it is a good place to be cool and usalama wa kutosha!!Fay Pub ipo Sinza kumekucha,nyuma ya Seven Up kama unaelekea shamool Hotel,, kwa maelekezo piga namba 0715 556453

tangaza

Sunday, September 9, 2012

DOGO JANJA AKIWA NA CREW NZIMA YA MTANASHATI YA USTAZI JUMA NA MUSOMA KUKAMUA LEO BILLZ KATIKA UZINDUZI WA KUNDI.

KUNDI la burudani ya muziki wa kizazi kipya la ‘Mtanashati’  linatarajia kufanya uzinduzi  wake mpya katika Ukumbi wa Club Billicanas, uliopo katikati ya Jiji la Dar es salaam, eneo la Posta.

Akizungumzia uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa  ‘Mtanashati Entertainment’ Ostaz Juma na musoma, alisema tayari maandalizi ya uzinduzi huo yamekamila na kuongeza kuwa kinachosubiriwa ni muda ili kuwadhihirishia kile kilichokusudiwa.

Alisema katika uzinduzi huo utakaotumika pia kwa ajili ya kuwatambulisha upya wasanii wote watano wanaounda kundi hilo wakati huu ambao wanaendelea kujihimarisha kimuziki ambapo pia amewaomba wapenzi wa burudani kujitokeza kwa wingi kushuhudia uzinduzi huo.

Alisema katika kupamba siku hiyo, ukiacha burudani kutoka kwa wasanii hao, pia kutashushwa  disco la nguvu hadi kunapokucha na maarufu ‘DJ Ibra’ huku akisisitiza kuwa  ‘usiku wa leo utakuwa moto wa kuotea mbali’.

“Baada ya Mtanashati kuporomosha burudani wiki iliyopita katika ukumbi wa Maisha Club, wiki hii kazi inahamia Billicanas’ bila shaka watu wote walioudhuria burudani ya pale Maisha wanakumbukumbu nzuri juu ya burudani ya nguvu iliyofanywa na Dogo Janja na PNC, burudani ya leo ni zaidi ya ile ya Maisha” alisisitiza Ostaz Juma na musoma.

Alisema katika uzinduzi huo, kundi hilo litapiga nyimbo mbalimbali zikiwemo mpya pamoja na zile zinazoendelea kutamba katika vituo mbalimbali vya redio na televisheni  'Ya Moyoni' 'Checherumba'  ‘watasubiri’ na zinginezo zikitarajiwa kutumbuizwa katika uzinduzi huo.

Mtanashati ni kundi linaloundwa na wasanii watano  ambao ni Dogo Janja, Amazon, Y-Fil, PNC, Happy Balice ndani ya familia ya ‘Moja ya Muziki’ iliyopewa jina la ‘MTANASHATI ENTERTAINMENT’ chini ya Mkurugenzi wake Mkuu ‘Ostaz Juma na musoma’ ambaye kwa mujibu wake malengo makubwa ya kuanzishwa  ‘Mtanashati’  kumekusudia  mapinduzi mapya katika tasnia  ya Muziki wa Kizazi kipya.
Wakati huo huo habari zilizonifikia sasa hivi kupitia account yamgu ya BBM toka kwa dogo Janja zinasema ustaz Juma na Musoma amepata mtoto wa kiume toka kwa mke wake leo hii majira ya mchana.


Source;Kajuna son & Dogo Janja

No comments:

Post a Comment