ushauri

Fay Pub

Fay Pub
Fay Pub Sinza,We Rock,it is a good place to be cool and usalama wa kutosha!!Fay Pub ipo Sinza kumekucha,nyuma ya Seven Up kama unaelekea shamool Hotel,, kwa maelekezo piga namba 0715 556453

tangaza

Saturday, May 25, 2013

DOWNLOAD HII

Ni vizuri kuusupport mziki mzuri wa kitanzania tena kutoka kwa vijana wadogo walioamua kujiariri  wenyewe basi fanya hiviii ponyeza HAPA kuudownload mziki mtamu namzuri toka kwa kijana wa BUKOBA mwenye maskani yake Arusha muite EDger Method thenn utuoe sisi feedback tujue tunausukuma vipi mzuziki huu wa kibongo mbelee.

Sunday, May 12, 2013

ngoma mpya kabisa kutoka kwa mwanamuziki wa kizazi kipya, C-Low

Ni ngoma mpya kabisa kutoka kwa mwanamuziki wa kizazi kipya, C-Low akiwa amemshirikisha mwanamuziki Yard Bash pamoja na mwanadada Tammy kwenye ngoma "SIDE B" ...
SIDE B ni mdundo wa ngoma ambao umefanywa na producer Nahreel pamoja na Mr. Thomas wakati video imetengenezwa na Director 2.5D pamoja na Wyclif kutoka kampuni ya Touch Of Art Vision Pro Creative Minds ...
Enjoy both the Audio and Video ...FOLLOW LINK BELOW


http://t.co/CW7YAoVzl4

Thursday, May 9, 2013

PONda aHUKUMIWa KIFUNGO CHa MWaKa MMOJa NJE.

Makahama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar Es Salaam leo imemuhukumu Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda kifungo cha nje cha mwaka mmoja, huku washtakiwa wengine wote 49 wakiachiwa huru.
 

BUKUKU APATA MCHUMBA MPYA

MWIMBAJI wa Muziki wa Injili , Bahati Lusako Bukuku amefunguka kuwa amepata mchumba lakini tatizo linabaki kuwa mume wake wa zamani, Daniel Basila ambaye anasuasua kumpa talaka yake

Akizungumza  jijini Dar juzikati, staa huyo anayetamba na wimbo wake wa Dunia Haina Huruma aliweka wazi kwamba hivi karibuni Mungu amemjalia kupata mchumba ambaye anahofia kumwanika kwa kuwa anabanwa na kifungo cha ndoa yake ya kwanza aliyofunga na Basila.
 Bahati alisema kuwa kifuatacho inabidi adai talaka yake kwa nguvu zote hata ikiwezekana kufikishana polisi ili aondokane na kifungo cha ndoa hiyo na aanze mipango ya ndoa kwa kuwa hataki kumtendea Mungu dhambi.

Alisema kuwa, mara nyingi amekuwa akimkumbusha mumewe huyo wa zamani kuhusu talaka lakini amekuwa akimwambia asikonde talaka yake ipo hivyo avute subira.

Bukuku aliolewa na Daniel na kufanikiwa kupata mtoto mmoja ambaye alifariki dunia mwaka 2006 kabla staa huyo kutengana na mumewe.

Prezzo IN dSM

Mshindi namba mbili wa BBA 2012 CMB Prezzo ameanza kupata nguvu ya kuendelea na kazi yake kubwa ya siku zote ambayo ni muziki.
May 4, 2013 Prezzo amekubali na kutekeleza mwaliko wa ku cheza kwenye Pool Party Dar es Salaam Tanzania akiambatana na wasanii wengine kama Avril na Kelmah kutoka Kenya, pamoja na Mwana FA kutoka Tanzania.



Bado haijatimia miezi mitatu toka Mnigeria Goldie ambae alikua mpenzi wa Prezzo afariki dunia ambapo kwenye Exclusive interview, Prezzo alisema machungu aliyonayo bado hayampi nafasi ajisikie kuwa karibu na mwanamke yeyote kimapenzi.
 

Monday, May 6, 2013

Ommy Dimpoz KUACHIA MZIGO MPYA NA AVRIL PIA SIKIA UWEZEKANO WA KUWAPO MAHUSIANO YA KIMAPENZI KATI YA DIAMOND PLATNUMZ NA AVRIL.

Kwa wale woote ambao wamekuwa wakisubiri kwa hamu ile ngoma ya bi dada Avril kutoka Kenya na Bongo's finest Ommy Dimpoz  ambayo ilikuwa izinduliwe mwishoni mwa mwezi uliopita kama ilivyokuwa imetangazwa, story ni kwamba mipango haikuenda kama ilivyowekwa hasa kutokana na kupishana sana kwa ratiba za wasanii hawa wawili, ikizingatiwa pia kuwa kwa sasa Dimpoz yupo nnje ya nchi kikazi.
Avril ambaye kwa sasa yupo hapa Bongo amesema kuwa, ngoma hii bado haijakamilika kabisa, na kuna mambo kadhaa ya kugusa kwa upande wa mastering ili iwe katika kiwango chake, na pia kwa mujibu wake, Jina la ngoma hii huenda likawa ni 'Hellow Baby'.

 Ngoma hii inabeba story ya wapenzi wawili ambao umbali umekuwa ni changamoto kubwa katika mapenzi yao.
On the other hand, kwa wale watu kibao ambao walikuwa na hamu ya kusikia Mwanadada huyu anazungumziaje mahusiano yake na Diamond, Hii ni nukuu fupi kutoka katika maelezo yake, 'Diamond and I are just proffessional friends'.


KAMA YOU LIKE GOOd MUSIC BASI FANYA HIVIIII!!!

Sasa unaweza kumpigia kura SHEDDY CLEVER kuwa producer bora wa mwaka 2012~2013 anaechipukia.Tuma BF5 kwenda namba 15345 au  ingia www.kilitimetz.com umuwezeshe SHEDDY CLEVER. 





Nyimbo alizo fanya kwa mwaka 2012 ni MARRY ME wa RICH MAVOKO, ZILIPENDWA ya MATONYA, MTOTO AMEKUA wa PASHA, YATAKWISHA wa BEN POL na LINNAH na nyingine nyingiii, Muwezeshe Dogo Achukue Mzigo huo kwani kwa kazi alizofanya hakika anastahili, Tunaomba Support Yenu.

Powered by www.citybangz.blogspot.com

Friday, May 3, 2013

BREAKING NEEEWS!!! KIJANA AJITUPA TOKA GHOROFA YA 9 MPAKA CHINI KARIAKOO.

Muda si mrefu huyu kaka kajirusha toka ghorofa ya 9 concord hotel kariakoo akaangukia kwenye hiyo taxi chanzo hata hakijulikani kapatwa na nini, ni mfanya biashara anaitwa Shirima kakimbizwa hosp.

MATOKEO YA FORM 4 YAFUTWA MITIHANI KUSAHIHISHWA TENA.

TAARIFA  KUTOKA BUNGENI MUDA HUU AMBAPO WAZIRI LUKUVI  AMETANGAZA KURUDIWA UPYA KUSAHISHWA KWA MITIHANI YA KIDATO CHA NNE KWA MWAKA 2012,

HII IMETOKANA NA MAPENDEKEZO YALIYO TOLEWA NA TUME ILIYO UNDWA KUCHUNGUZA TATIZO LA WANAFUNZI WENGI KUFELI KATIKA HUO MTIHANI,PIA AMESITISHA KUANZA KUTUMIKA KWA VIWANGO VIPYA VYA UFAULU.

ALICHOKISEMA Gadna G JUU YA WOSIA WA LAdY JAYdEE

Ipi ni Kauli yako juu ya Wosia wa Lady Jay Dee...?

Gadna G: Ni maneno  ambayo yametoka moyoni mwake na  ni maneno  mbayo anajitetea kama msanii,  mimi kama Meneja ukiacha pia kama  mke wangu naendelea kumsapot kwa kile ambacho anaona ni sawa, basi mimi nitaendelea kumsaport  na kujaribu kuzungumza na Lady Jay Dee, mara nyingi anasema tu kwamba  watu wasifikilie ni swala la wimbo kupigwa au kutokupigwa, hayo ni mambo ya kawaida lakini wafikirie tu kwamba huyu mtu anaongea kutokana experience yake aliyokuwa nayo na wale watu.
Baada ya mwaka 2003 kuacha kufanya kazi kwenye management yao ya Smooth Vibe, yalitokea mambo mengi hapa katikati  ila hakusema lakini siku za hivi siku za karibuni kuna mengine ambayo yametokea, ndio akaona hapana nisipo sema nitazidi kukandamizwa na matokeo yake nitakufa kisabuni.




Hii ni kama vita mmejipangaje..?
Gadna G: Unapoamua kusema ukweli swala la kujipanga mara mbili huwa halipo, ni kwamba unasema ukweli watu wasikie  naukizungumzia uhasama watu watauliza juu ya uhasama  lakini ulikuwepo tayari kwahiyo tu watu wanajua kwa sasa kwa kuwa jdee ameamuwa kuongea lakini tu hawajui tu kwamba jdee alikuwa na matatizo na wale watu tangu kipindi cha nyuma sababu wale watu wanafumo dume ya kufanya kazi na alipoachananao aliona kama wanamfatilia  kulekule ambapo yeye alipo 


Nini mlikiona kama chokochoko...?
Gadna G: Unajua kwa mfano unaweza kumuomba mtu maji akakwambia sina, ukayaona yale  pale ukamwambia niuzie akakuuzia ila bado alivyokuuzia  akaona kama unafaidi, mwisho  akakwambia yameisha nenda sehemu nyingine, ukaenda sehemu nyingine na ukayapata bure, akaona umepata akaamua kukufata kulekule na akakukuta unakunywa maji kwenye grasi kisha akakuputa, sasa hapo inabidi useme hapa unavyofanya sio sawa ndo hicho anachofanya Jay Dee sasa hivi.


Hali hii imewaathiri kwa kiasi gani...?
Gadna G: Cha kushukuru Mungu ni  kwamba msanii au hata pia stesheni ya redio inategamea umma wa Watanzania au  hata mashabiki kwa ujumla kwa kuwepo kwake. Jay Dee anapata saport nzuri kutoka  Watanzania, basi ujue hata hajaathirika chochote, na pia tu anaendelea kufanya kazi kwa bidii, ila tu isipokuwa unapoona mtu anafanya madhara ili tu mtu apate athari fulani ndio unasimama kuongea, ndiyo maana tuna Bunge na watu wanasimama, watu wanaongea, watu wanatetea hoja, ndiyo maana yake. Yani lazima mtu usimame useme ukweli kwa unalohisi hili jambo litanipa madhara nisiposema.
 

Kwa Wasanii wengine unawaambiaje...?
Gadna G: Uwoga ni kitu ambacho binadamu tumeumbiwa, wakati mwingine unasaidia wakati mwingine unakudhiru uwoga wako,kwa sababu wanasema adui wa maendeleo yako mwenyewe ni wewe mwenyewe, ndiyo maana uwoga wako unaeza ukasabishwa ukakandamizwa zaidi, ndiyo maana wazee wetu waliweza kusimama na kuikomboa hii nchi kwa sababu walisimama hawakuogopa. Wangeogopa hii leo hii nchi tusingekuwa huru, kwa hiyo kama kuna mtu ana jambo na anaogopa kusema hilo ni jambo la kawaida kuogopa, lakini wakati wa kusema ukifika usiogope kusema ili mradi useme ukweli, basi inatosha....

Kauli yako ya mwisho ni ipi..?
Gadna G: Ni kwamba wanahitaji kujua ukweli na kuambiwa ukweli, mtu yoyote anayejua kitu cha kweli  anaweza kusema sio sawa, utaendelea kukandamizwa. Kauli ya mwisho  ndo hiyo wanahitaji kuambiwa ukweli na  kusikia ukweli  ili kama wanakosea wasiendelee kukosea  wabadilikee….

Mwisho..!

Thursday, May 2, 2013

LIL WAYNE HOI TENA.

 Lil Wayne ni moja ya watu ambao kwa sasa afya zao zinatajwa kuwa katika hatihati hasa baada ya rapa huyu kuzimia kwa mara nyingine siku ya juzi na kupelekwa hospitali ambapo alitoka jana na michongo hii yote ikiwa inafanyika kwa siri kubwa.


Mapema mwezi March Lil Wayne alikiri hadharani kuwa ana ugonjwa wa kifafa kwahiyo kudondoka dondoka kwake ni kitu cha kawaida, na hii ni nukuu ya maneno yake mwenyewe hasa baada ya tukio la mara ya mwisho la kulazwa hospitali kwa wiki nzima akiwa katika wodi ya wagonjwa mahututi.




"The thing is, man, the bad news is, I'm an epileptic, so I'm prone to seizures," he said. "This isn't my first, second, third, fourth, fifth, sixth, seventh seizure. I've had a bunch of seizures; y'all just never hear about it. This time it got real bad because I got three of 'em in a row, and on the third one, my heart rate went down to, like, 30 percent. Basically, I could've died soon. That's why it was so serious. The reason being for the seizures is just plain stress, no rest and overworking myself. That's typical me, though."

Hadi sasa hakuna mtu yoyote kutoka katika timu ya rapa huyu ambaye ameibuka kuzungumzia chochote kutokana na tukio hili.

SCHOLARSHIP!! SCHOLARSHIP!! SCHOLARSHIP!! SCHOLARSHIP!! KAMA UNA NdUGU AU RAFIKI ANAEHITAJI KUJA KUSOMA INIA HII NI MUHIMU SANA SOMA HAPA!!



SCHOLARSHIP
Get admission in 2013 to study Bangalore University, India, for all courses, with 50% scholarship on tution fees.

   TUTION  FEES STRUCTURE
First year; 2000 Dollars
Second year; 1000 Dollars
Third year; 1000  Dollar

ACCOMODATION
  Is 1000 Dollars per year

ACADEMIC QUALIFICATION
  Form 6 starting with one principle or diploma or the  one who have no principle should not have more than one F.

 
TUITION FEES FOR MASTER DEGREE/POST GRADUATE
  First year; 3000 Dollars
 Second year 2000 Dollars

REGARD ADMISSION.
E-mail; kkoverseasedulink@gmail.com
Phone; +919535914895
FOR DETAILS
Call our consultancy in TANZANIA
Phone-0717532818
E mail;fredyse1@hotmail.com