ushauri

Fay Pub

Fay Pub
Fay Pub Sinza,We Rock,it is a good place to be cool and usalama wa kutosha!!Fay Pub ipo Sinza kumekucha,nyuma ya Seven Up kama unaelekea shamool Hotel,, kwa maelekezo piga namba 0715 556453

tangaza

Monday, September 3, 2012

MWALIMU AACHISHWA KAZI KWA TUHUMA ZA USHOGA.

Uongozi wa Shule ya Sekondari ya Majengo, Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi umeridhia kuacha kazi kwa mwalimu wa kiume wa shule hiyo anayedaiwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Kufuatia hatua hiyo, Bodi ya shule imemlipa mwalimu huyo Endrew Katto, Sh. 2,409,924 kama kiinua mgongo baada ya kuitumikia shule hiyo kwa miaka sita.
Mwalimu Katto aliajiriwa katika shule hiyo Februari Mosi, 2006 hadi Februari Mosi mwaka huu, alipoamua kuandika barua hiyo na kumfungulia kesi Mkuu wa shule hiyo, Bruda Peter Lyimo, kwa madai ya kumtukana kwa maandishi katika kituo kikuu cha polisi Mjini Moshi na kufungua jalada Na. MOS/RB/11709/2012
Alipotakiwa na NIPASHE kueleza sababu za kuandikiwa barua hiyo alisema hawezi kuzungumzia kwa undani kwa kuwa alishamuelekeza wakili wake kuchukua hatua za kisheria
Aidha, mwalimu huyo amewasilisha barua ya kutaka aombwe radhi na kulipwa fidia ya Sh milioni 800 kupitia wakili wake Kipoko & Advocate, akidai kuwa Bodi ya shule imemdhalilisha na kuchafulia jalada la taaluma yake hali inayomsababishia asiajiriwe sehemu yoyote.
Hata hivyo, wakili huyo aliiambia NIPASHE kwa njia ya simu kuwa endapo watamuomba radhi mteja wake na kumlipa gharama na kuridhika hawataenda mahakamani
Kwa mujibu wa barua ya Mkuu wa shule hiyo, Bruda Peter Lyimo ya 18/04/2012 yenye kumbukumbu Na. MSS/PP/AK/189/30 imeeleza kuwa uongozi wa shule umeridhia mwalimu huyo kuacha kazi baada ya kubainika kuwa alikuwa akijihusisha na masuala ya kujamiiana kinyume cha maumbile.
“The school administration received your letter dated 12.04.2012 in which you clearly stated that you will not keep on working at this shool as a teacher after a homosexual scandal was revealed on you” (Utawala wa shule umepokea barua yako ya tarehe 12. 04. 2012 ambayo umeeleza wazi kuwa huwezi kufanyakazi katika shule hii kama mwalimu baada ya kubainika kwa kashfa dhidi yako ya kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja),”
ilisomeka sehemu ya barua hiyo ikimaanisha kuwa kuacha kazi kwa mwalimu huyo kulitokana na kubainika kushiriki suala la ushoga.
Akizungumza na NIPASHE ofisini kwake, Bruda Lyimo alikiri kuandika barua hiyo kwa maelezo kuwa aliiandika akiwa makini kwa kuwa ushahidi upo nakuongeza kuwa Majengo Sekondari ni shule inayoheshimika nchini kwa elimu na malezi bora kwa hiyo sio busara kuendelea kuwa na mwalimu aliyekiri kuwa ni shoga.
Habari zilizolifikia gazeti hili na kuthibitishwa na Mkurugenzi wa Elimu Jimbo Katoliki la Moshi, Padre Wiliamu Ruaichi, zimeeleza kuwa uongozi wa kanisa hilo bado unatafakari hatua iliyochukuliwa na bodi.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments:

Post a Comment