ushauri

Fay Pub

Fay Pub
Fay Pub Sinza,We Rock,it is a good place to be cool and usalama wa kutosha!!Fay Pub ipo Sinza kumekucha,nyuma ya Seven Up kama unaelekea shamool Hotel,, kwa maelekezo piga namba 0715 556453

tangaza

Tuesday, September 11, 2012

KALAPINA WA KIKOSI CHA MIZINGA AIGIZA MOVIE JUU YA MAISHA YA DK.ULIMBOKA.

Kamanda mkuu wa kikosi cha Mizinga, msanii wa Hiphop Kalapina mwishoni mwa mwaka huu ndio amepanga kuitoa na imfikie kila Mtanzania, movie mpya ambayo ameigiza kama kiongozi wa Madaktari Dr Ulimboka ambae siku kadhaa zilizopita alitekwa na kupigwa sana na wasiojulikana.

Pamoja na kwamba kwa sasa kuna stori za chinichini kwamba Dr Ulimboka ameondoka Tanzania kutokana na kuhofia usalama wake, Kalapina anaamini Dr Ulimboka hana haja ya kukimbia nchi kutokana na kuhofia usalama wake.

Namkariri Kalapina akisema “ninachoweza kumshauri Dr Ulimboka asiogope, watu wapo kama anahitaji kupewa ulinzi Kikosi cha mizinga tupo fiti kila idara na tuna kitengo cha kikosi kinaitwa Department of defence (DOD) kitengo cha ulinzi, kuna vijana wamefuzu mafunzo wanaweza kumlinda mtu yoyote, wanakodishwa kwa gharama nafuu tu kama unahitaji walinzi unaweza ukaniona, walinzi wa kulinda kumbi za disco na sehemu nyingine pia, kama anahitaji atapata kwa gharama nafuu”
Kuhusu hiyo movie mpya Kalapina atakayoigiza maisha ya Dr Ulimboka, amesema “nitajaribu kuonyesha tokea anarudi kutoka masomoni, harakati zake mpaka anaanza kazi, harakati za kutetea madaktari wenzake mpaka anapelekea kutekwa na kutupwa msituni, hii yote ni kuionyesha tasnia ya filamu kwamba tuna vitu vingi vya kuonyesha lakini nashangaa zimejaa filamu za ngono na filamu za upotoshaji”



source;Millard Ayo

No comments:

Post a Comment