Vodacom na TFF zasaini mkataba wa udhamini wa ligi kuu kwa miaka mitatu
Klabu ya Simba Sports Club ndio bingwa mtetezi.
Msimu wa ligi kuanza Septemba 15, na kushirikisha timu 14.
Polisi Morogoro, Tanzania Prisons na Mgambo JKT ni timu mpya katika ligi.
Klabu ya Simba Sports Club ndio bingwa mtetezi.
Msimu wa ligi kuanza Septemba 15, na kushirikisha timu 14.
Polisi Morogoro, Tanzania Prisons na Mgambo JKT ni timu mpya katika ligi.
Dar es Salaam, 11 Septemba 2012. Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) leo limeingia katika mkataba wa udhamini kutoka kwa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, wakati maandalizi ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania yakielekea ukingoni.
Kampuni ya Vodacom imekuwa mdhamini wa ligi kuu kwa miaka mitano iliyopita, na sasa imeingia mkataba mpya wa udhamini kwa miaka mitatu na TFF, mkataba utakao liwezesha shirikisho hilo kupoea fedha za udhamini kwa miaka mitatu.
Ligi kuu ya Vodacom itaanza tarehe 15 ya mwezi huu, ikitarajia kushuhudia michezo 182 ikichezwa katika viwanja mbalimbali na kushirikisha timu 14, zikiwemo timu za Dar es Salaam Young Africans, Kagera Sugar na Simba Sports Club ambaye ndie bingwa mtetetzi wa kombe hilo.
source;Mateja20
No comments:
Post a Comment