MSANII anayepagawisha mashabiki wengi kutokana na sauti yake ‘Benjamini wa Mambo Jambo’, ameiambia blog hii, kuwa anatarajia kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Skendo’, ambayo itazungumzia namna watu wanavyitengenezea skendo kwa lengo la kujipatia umaarufu usiyo na maana.
Alisema kuwa ngoma hiyo inakuja hivi soon na ipo katika mtiririko mzuri wa mashairi pamoja na ujumbe wake, kitu ambacho kinaashiria kuwa itafanya vizuri kwani kwa upande wake si msanii ambaye anatoa ngoma kila baada ya wiki mbili.
Msanii huyo aliwahi kutamba sana na ngoma ya yake ya ‘My Friend’, ambayo inazungumzia mambo mengi ya maisha na njisi ndugu yako anavyoweza kukumaliza kwa ajili ya pesa au kutaka kuwa juu ya yako.
“Mimi si msanii ambaye anatoa ngoma kila baada ya wiki kwani najua kusoma alama za nyakati hivyo napokuwa kimya huwa natafakari ni namna gani naweza kutoa kitu kizuri kwa ajili ya mashabiki wangu,” alisema.
Hata hivyo sasa msanii huyo ana kampuni yake ya kutengeneza video inayoitwa Promo Only ambapo pia matarajiao yake ni kuwa na kampuni kubwa zaidi ya atakayoipa jina la B.M.L, ambayo itahusika zaidi na video pamoja na audio.
Source;DarTalk
No comments:
Post a Comment