Kamanda mkuu wa kikosi cha
Mizinga, msanii wa Hiphop Kalapina mwishoni mwa mwaka huu ndio amepanga
kuitoa na imfikie kila Mtanzania, movie mpya ambayo ameigiza kama
kiongozi wa Madaktari Dr Ulimboka ambae siku kadhaa zilizopita alitekwa
na kupigwa sana na wasiojulikana.
Pamoja na kwamba kwa sasa kuna
stori za chinichini kwamba Dr Ulimboka ameondoka Tanzania kutokana na
kuhofia usalama wake, Kalapina anaamini Dr Ulimboka hana haja ya
kukimbia nchi kutokana na kuhofia usalama wake.
Namkariri Kalapina akisema
“ninachoweza kumshauri Dr Ulimboka asiogope, watu wapo kama anahitaji
kupewa ulinzi Kikosi cha mizinga tupo fiti kila idara na tuna kitengo
cha kikosi kinaitwa Department of defence (DOD) kitengo cha ulinzi, kuna
vijana wamefuzu mafunzo wanaweza kumlinda mtu yoyote, wanakodishwa kwa
gharama nafuu tu kama unahitaji walinzi unaweza ukaniona, walinzi wa
kulinda kumbi za disco na sehemu nyingine pia, kama anahitaji atapata
kwa gharama nafuu”
Kuhusu hiyo movie mpya Kalapina
atakayoigiza maisha ya Dr Ulimboka, amesema “nitajaribu kuonyesha tokea
anarudi kutoka masomoni, harakati zake mpaka anaanza kazi, harakati za
kutetea madaktari wenzake mpaka anapelekea kutekwa na kutupwa msituni,
hii yote ni kuionyesha tasnia ya filamu kwamba tuna vitu vingi vya
kuonyesha lakini nashangaa zimejaa filamu za ngono na filamu za
upotoshaji”
No comments:
Post a Comment