Uongozi wa Shule ya Sekondari ya Majengo, Manispaa ya Moshi mkoani
Kilimanjaro inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi umeridhia
kuacha kazi kwa mwalimu wa kiume wa shule hiyo anayedaiwa kujihusisha na
mapenzi ya jinsia moja.
Kufuatia hatua hiyo, Bodi ya shule imemlipa mwalimu huyo Endrew
Katto, Sh. 2,409,924 kama kiinua mgongo baada ya kuitumikia shule hiyo
kwa miaka sita.
Mwalimu Katto aliajiriwa katika shule hiyo Februari Mosi, 2006 hadi
Februari Mosi mwaka huu, alipoamua kuandika barua hiyo na kumfungulia
kesi Mkuu wa shule hiyo, Bruda Peter Lyimo, kwa madai ya kumtukana kwa
maandishi katika kituo kikuu cha polisi Mjini Moshi na kufungua jalada
Na. MOS/RB/11709/2012
Alipotakiwa na NIPASHE kueleza sababu za kuandikiwa barua hiyo
alisema hawezi kuzungumzia kwa undani kwa kuwa alishamuelekeza wakili
wake kuchukua hatua za kisheria
Aidha, mwalimu huyo amewasilisha barua ya kutaka aombwe radhi na
kulipwa fidia ya Sh milioni 800 kupitia wakili wake Kipoko &
Advocate, akidai kuwa Bodi ya shule imemdhalilisha na kuchafulia jalada
la taaluma yake hali inayomsababishia asiajiriwe sehemu yoyote.
Hata hivyo, wakili huyo aliiambia NIPASHE kwa njia ya simu kuwa
endapo watamuomba radhi mteja wake na kumlipa gharama na kuridhika
hawataenda mahakamani
Kwa mujibu wa barua ya Mkuu wa shule hiyo, Bruda Peter Lyimo ya
18/04/2012 yenye kumbukumbu Na. MSS/PP/AK/189/30 imeeleza kuwa uongozi
wa shule umeridhia mwalimu huyo kuacha kazi baada ya kubainika kuwa
alikuwa akijihusisha na masuala ya kujamiiana kinyume cha maumbile.
“The school administration received your letter dated 12.04.2012 in
which you clearly stated that you will not keep on working at this shool
as a teacher after a homosexual scandal was revealed on you” (Utawala
wa shule umepokea barua yako ya tarehe 12. 04. 2012 ambayo umeeleza wazi
kuwa huwezi kufanyakazi katika shule hii kama mwalimu baada ya
kubainika kwa kashfa dhidi yako ya kujihusisha na mapenzi ya jinsia
moja),”
ilisomeka sehemu ya barua hiyo ikimaanisha kuwa kuacha kazi kwa mwalimu huyo kulitokana na kubainika kushiriki suala la ushoga.
Akizungumza na NIPASHE ofisini kwake, Bruda Lyimo alikiri kuandika
barua hiyo kwa maelezo kuwa aliiandika akiwa makini kwa kuwa ushahidi
upo nakuongeza kuwa Majengo Sekondari ni shule inayoheshimika nchini kwa
elimu na malezi bora kwa hiyo sio busara kuendelea kuwa na mwalimu
aliyekiri kuwa ni shoga.
Habari zilizolifikia gazeti hili na kuthibitishwa na Mkurugenzi wa
Elimu Jimbo Katoliki la Moshi, Padre Wiliamu Ruaichi, zimeeleza kuwa
uongozi wa kanisa hilo bado unatafakari hatua iliyochukuliwa na bodi.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
No comments:
Post a Comment