Benki
ya NMB imewafikia wanafunzi 45,000 wa shule za msingi katika mpango
wake wa kukuza uelewa wa maswala ya kifedha uitwao NMB Financial
Fitness. Mpango huo ulioanzishwa mwezi Mei mwaka huu, una lengo la
kuwahamasisha wanafunzi kujiwekea akiba kwa kutumia huduma za kibenki
wanapokua wakubwa.
Akizungumza katika utambulisho huo, mwanafunzi wa
shule ya Liwale iliyopo mkoani Lindi Idrissa Ndumbaro aliishukuru benki
ya NMB kwa elimu hiyo ambayo baadae itamwezesha kuwa na uelewa wa
matumizi mazuri ya fedha pamoja na kujiwekea akiba.
Source;Mjengwa
No comments:
Post a Comment