Msanii wa hiphop Kalapina wa
kikosi cha Mizinga amekubali kutaja majina ya wasanii wa hiphop
anaosikiliza muziki wao kwa sasa hapa Tanzania.
Namkariri akisema “Tanzania
mimi nasikiliza wasanii wote niangalie vitu wanavyovifanya lakini
wasanii wengi hawako real wanafake, sasa hivi nimekua nikiwasikiliza
wadogo zangu Lunduno, Nash Mc, Fid Q, Mansu Lee, Rado… mzee mwenzangu
Profesa J amepotea sasa hivi, nilikua namsikiliza lakini sasa hivi
amepotea”
“Profesa J amefikia hatua
anafanya video za dada zetu wako uchi kabisa na ule ni udhalilishaji wa
kijinsia kama atabisha si udhalilishaji, achukue video awachukue dada
zake na mama zake wadogo awavalishe vichupi na sidiria tutaona kweli
yeye ni mmagharibi lakini kama anachukua dada za watu huu ni
udhalilishaji wa kijinsia mi napinga mambo kama yale, tusifikie huko
sasa hivi huwezi kufanya video kali mpaka uweke wanawake wako uchi
Tanzania” – Kalapina
Source;Millard Ayo
No comments:
Post a Comment