KUNDI
la burudani ya muziki wa kizazi kipya la ‘Mtanashati’ linatarajia
kufanya uzinduzi wake mpya katika Ukumbi wa Club Billicanas, uliopo
katikati ya Jiji la Dar es salaam, eneo la Posta.
Akizungumzia
uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa ‘Mtanashati Entertainment’ Ostaz
Juma na musoma, alisema tayari maandalizi ya uzinduzi huo yamekamila na
kuongeza kuwa kinachosubiriwa ni muda ili kuwadhihirishia kile
kilichokusudiwa.
Alisema
katika uzinduzi huo utakaotumika pia kwa ajili ya kuwatambulisha upya
wasanii wote watano wanaounda kundi hilo wakati huu ambao wanaendelea
kujihimarisha kimuziki ambapo pia amewaomba wapenzi wa burudani
kujitokeza kwa wingi kushuhudia uzinduzi huo.
Alisema
katika kupamba siku hiyo, ukiacha burudani kutoka kwa wasanii hao, pia
kutashushwa disco la nguvu hadi kunapokucha na maarufu ‘DJ Ibra’ huku
akisisitiza kuwa ‘usiku wa leo utakuwa moto wa kuotea mbali’.
“Baada
ya Mtanashati kuporomosha burudani wiki iliyopita katika ukumbi wa
Maisha Club, wiki hii kazi inahamia Billicanas’ bila shaka watu wote
walioudhuria burudani ya pale Maisha wanakumbukumbu nzuri juu ya
burudani ya nguvu iliyofanywa na Dogo Janja na PNC, burudani ya leo ni
zaidi ya ile ya Maisha” alisisitiza Ostaz Juma na musoma.
Alisema
katika uzinduzi huo, kundi hilo litapiga nyimbo mbalimbali zikiwemo
mpya pamoja na zile zinazoendelea kutamba katika vituo mbalimbali vya
redio na televisheni 'Ya Moyoni' 'Checherumba' ‘watasubiri’ na
zinginezo zikitarajiwa kutumbuizwa katika uzinduzi huo.
Mtanashati ni kundi linaloundwa na wasanii watano
ambao ni Dogo Janja, Amazon, Y-Fil, PNC, Happy Balice ndani ya familia
ya ‘Moja ya Muziki’ iliyopewa jina la ‘MTANASHATI ENTERTAINMENT’ chini
ya Mkurugenzi wake Mkuu ‘Ostaz Juma na musoma’ ambaye kwa mujibu wake
malengo makubwa ya kuanzishwa ‘Mtanashati’ kumekusudia mapinduzi
mapya katika tasnia ya Muziki wa Kizazi kipya.
Wakati huo huo habari zilizonifikia sasa hivi kupitia account yamgu ya BBM toka kwa dogo Janja zinasema ustaz Juma na Musoma amepata mtoto wa kiume toka kwa mke wake leo hii majira ya mchana.
Source;Kajuna son & Dogo Janja
No comments:
Post a Comment