Mke
wa rais wa Marakeni Barack Obama, Michelle Obama amemuunga mkono mumewe
katika mkutano mkuu wa chama cha Democratic akiomba rais huyo apewe
muda zaidi.
Bibi Obama amekiri kuwa
mabadiliko ambayo mumewe Barack Obama aliahidi wakati wa kampeini ya
wadhifa wa urais miaka minne iliyopita hayajatwa kikamilifu lakini
akawaomba wapiga kura kumpa miaka mingine minne ili kuuimarisha uchumi
wa Marekani unaoyumbayumba.
Michelle Obama ndiye aliyekuwa
wa kwanza kumtetea mumewe katika siku ya kwanza ya mkutano huo wa siku
tatu ambao utakamilika kwa hotuba ya Obama kesho Alhamisi ili kukubali
uteuzi wa chama cha Democratic wa kupambana na Mitt Romney katika
uchaguzi wa uraisi tarehe sita Novemba.
Bibi Obama alisema "Kama rais,
utapata ushauri wa kila aina kutoka kwa watu tofauti, lakini
unapohitajika kufanya uamuzi wako kama rais, kinachokuongoza ni maadili
na maono yako pamoja na uzoefu wa maisha, mambo yanayokufanya uwe jinsi
ulivyo"
Katika kinyang'anyiro ambacho
ni kikali kutabiri zikiwa zimebaki wiki tisa kabla ya Wamerakani kupiga
kura, Obama anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mgombea wa
Republican Mitt Romney kwa sababu ya kudorora uchumi pamoja na asilimia
8.3 ya ukosefu wa ajira.
Source;Machibya
No comments:
Post a Comment