Mpaka sasa Nigeria inaongoza
kwa idadi ya vijana wake kufanya kolabo na mastaa wa muziki wa dunia
kutokea Marekani pamoja na kupata deals, mfano ni kwa kolabo
waliyoifanya P Square na rapper Rick Ross pia kolabo yao na Akon lakini
pia Dbanj ambae yuko chini ya lebo ya Kanye West.
Naomba kukufahamisha kwamba
kolabo inayofata sasa hivi ni ya Producer/msanii J Martins ambapo tayari
ameshairekodi na Cuban American Rapper Pitbull na mpaka sasa jina la
kolabo yenyewe halijatajwa.
Kingine ambacho unapaswa
kufahamu ni kwamba wiki chache zijazo ndio video itafanyika kwenye mji
wa Amsterdam ambapo stori kamili ziLISEMA kwamba ni hit ambayo Pitbull
amelenga kupanua zaidi soko lake ambalo kwa sasa ni USA na Latin
America na J Martins pia anataka kuvuka boda na kwenda umbali mrefu.
Bado haijawekwa wazi jamaa
walikutanaje mpaka akakubaliwa kolabo lakini kolabo hiyo itamsogeza sana
J Martins kwa sababu Pitbull ni staa ambae ameshine kwenye nyimbo zake
na hata kolabo nyingi alizofanya na wakali kama J.Lo na Ne-yo.
Source;Millard Ayo
No comments:
Post a Comment