Kuna kipindi wimbi la stori za wasanii Tanzania kutumia uchawi lilipita sana bongo mpaka wasanii wakubwa wakajitokeza kukemea.
Sasa kama ulidhani Tanzania ndio inaweza kuwa nchi pekee afrika Mashariki wasanii wake kutumia juju, utakua umepotea…
Michael Ross anashare
experience yake na sisi, akiamini kwamba uchawi kwenye muziki wa Uganda
upo pia na watu wanautumia, lakini haamini kama uchawi unaweza
kumsaidia.
Kwa miaka yote tisa anasema
amefanya muziki na ametengeneza mkwanja na ametengeneza hits bila
kujaribu kutumia uchawi, ndio maana haoni umuhimu wa kutumia uchawi
ambapo kwenye line ya mwisho, mkali huyu kutoka 256 amesema hata kama
msanii atatumia juju nyumbani kwao halitoweza kumsaidia kimataifa.
No comments:
Post a Comment