Mwanamitindo wa kimataifa wa
Tanzania, Happines Millen Magese ameshiriki Wiki ya Mitindo ya Mavazi ya
New York nchini Marekani juzi.
Onyesho hilo lilishuhudiwa na nyota
wakubwa kama mwanasoka David Beckham huku wabunifu wakubwa duniani
wakishiriki kuonyesha mitindo yao ya mavazi kama Tommy Hilfiger,
Carolina Herrera, Michael Kors, Ralph Lauren na mwanamama Tracy Reese,
ambaye gauni lake lilivaliwa na mke wa rais wa Marekani, Michelle Obama
katika Kongamano la Kitaifa Chama cha Democratic. Mwanamitindo maarufu
Naomi Campbell pia alipita stejini kuonyesha mitindo.
Source;Straika
No comments:
Post a Comment