Msanii Wizkid wa Nigeria ambae
amewahi kuingia kwenye rekodi ya nyimbo zake kuombwa na wanafunzi anazidi kupata mashavu ya staa wa dunia
mwimbaji Chris Brown.
Mara ya mwisho Wizkid alikula
shavu baada ya Chris Brown kumuita kwenye stage na kufanya nae show
kidogo wakati akiwa Ghana wiki kadhaa zilizopita lakini sasa hivi CB
amempa shavu Wizkid kwenye interviw aliyofanyiwa na show kubwa ya
burudani ambayo ina mashabiki mamilioni vijana kutoka sehemu mbalimbali
za dunia ya 106 & Park ya Television ya BET.
CB akizungumzia
Album yake, aliizungumzia staili ya kucheza ya Azonto ambayo anasema
alifundishwa kuicheza na staa wa muziki Wizkid kutoka Nigeria, namkariri
akisema “ni staili inayotaka kufanana kama na ya Michael Jackson,
utaiona kwenye video… vuta subira tu!! nimejifunza kutoka kwa Wizkid,
sitaki kusema nimeianzisha mimi…. nimeitoa kwa Wizkid, ni msanii mkali
wa Nigeria”
No comments:
Post a Comment