Taarifa kutoka Tunduma mkoani Mbeya
zinadai kuwa hali si shwari katika eneo hilo kutokana na kuzuka kwa
vurugu kubwa zinazodaiwa kusababishwa na masuala ya kiimani ya nani
achinje kati ya mkristo na Muislam .
Mwandishi wetu kutoka Tunduma mkoani Mbeya anaripoti kuwa vurugu hizo zimeanza majira ya saa nne asubuhi kwa makundi ya vijana kuandamana mitaani na kuvutana kuhusu uamuzi wa viongozi wa dini ya kikristo Tunduma kuandika barua kwa mkuu wa wilaya kutaka kuruhusiwa kuchinja wakati wa pasaka.
Ripota wetu anaripoti kuwa kabla ya ijumaa kuu viongozi hao wa dini ya Kikristo walikutana na mkuu wa wilaya ya Momba Abuud Saibea ambae aliwataka kuwasilisha barua rasmi ya kutaka kibali cha kuchinja .
Hata hivyo inaelezwa kuwa vurugu hizo za leo zina mikanganyiko mingi kwani wanaoshiriki katika vurugu hizo ni vijana wapiga debe .....
Vurugu za uchinjaji zilifanyika siku ya Pasaka na hazikuwa na mvutano kwa sababu wakristo walichinja katika bucha zao na waislamu nao walichinja katika mabucha yao ....
Cha kushangaza leo ni baada ya kuibuka kundi la vijana wanaofanya kazi katika stendi na vijiwe mbali mbali ambao ndio walioanzisha vurugu kiasi cha polisi kuingilia kati kwa kutumia mabomu ya machozi na kuwatawanya wananchi waliokuwa wamekusanyika maeneo mbali mbali .
Kutokana na vurugu hizo mpaka wa Tunduma ambao unaingia nchi za kusini mwa Tanzania ulifungwa pamoja na magari yaliyokuwa yakitoka Sumbawanga pia yalizuiwa kuendelea na safari hadi hali hiyo ilipotulia mida ya saa 8 mchana baada ya kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Diwani Athuman kufika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment