NI
kivumbi! Kuna madai kwamba, staa wa Bongo asiyechuja, Wema Sepetu
amemfikisha mama yake, Miriam Sepetu kwenye Kituo cha Polisi Kijitonyama
‘Mabatini’, Dar kwa madai ya kwenda nyumbani kwake na kufanya vurugu
zilizosababisha kuharibika kwa samani mbalimbali...
Kwa mujibu wa chanzo chetu, ishu hiyo ilijiri usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita, nyumbani kwa Wema, Kijitonyama, jijini Dar.
Mbali
na mama mtu, wengine waliofikishwa kituoni hapo ni dada mkubwa wa Wema
aitwaye Nuru na kijana aliyefahamika kwa jina moja la Bestizo ambaye
inasemekana ni mshirika mkubwa wa Diamond kwenye masuala ya mtandao wa
msanii huyo.
“Wema
alikuwa nyumbani kwake usiku huo, watuhumiwa hao wakamzukia na kuanza
kumchapa makofi ya ‘kelbu’ ambapo katika mshikemshike huo, baadhi ya
vitu vilivunjika na kumtia hasara staa huyo,” kilisema chanzo.
Haikujulikana
mara moja ni kitu gani kilisababisha mama mzazi huyo, dada mtu na
kijana asiyekuwa ndugu kwenda kwa Wema na kutenda kosa hilo.
Wema
alikwenda polisi na kuandikisha maelezo ambayo yameingizwa kwenye
jalada lenye kumbukumbu; KJN/RB/2755/2013 SHAMBULIO, KUHARIBU MALI.
No comments:
Post a Comment