ushauri

Fay Pub

Fay Pub
Fay Pub Sinza,We Rock,it is a good place to be cool and usalama wa kutosha!!Fay Pub ipo Sinza kumekucha,nyuma ya Seven Up kama unaelekea shamool Hotel,, kwa maelekezo piga namba 0715 556453

tangaza

Thursday, April 18, 2013

NAIBU SPIKA AWAPA WABUNGE WATANO AdHABU YA KUTOHUdHURIA VIKAO VYA BUNGE WABUNGE KWA SIKU TANO.

Naibu Spika wa Bunge JOB NDUGAI amemtoa nje ya Bunge kwa muda wa siku tano Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni TUNDU LISSU kwa madai ya utovu wa nidhamu na kuanzisha majibizano bungeni kitendo kinachokiuka kanuni za bunge.


 Wengine ambao wamepewa adhabu hiyo ya kutohudhuria vikao vya bunge kwa siku tano ni Mbunge wa Mbeya Mjini JOSEPH MBILINYI, Mbunge wa Arusha Mjini GODBLES LEMA, Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji PETER MSIGWA, Mbunge wa Nyamagana EZEKIA WENJE na Mbunge wa Ilemela HIGHNES KIWIA ambao walikuwa wakiwazuia askari wa bunge kumtoa nje LISSU.
Namkariri Naibu Spika akiongea  nje ya bunge akisema “nimemuonya zaidi ya mara kumi kwa jioni ya leo peke yake kwamba demokrasia ya kibunge ni ya kuwapa watu wengine nao nafasi ya kusikika, kila anaesimama anakatishwa yeye kasimama dakika zake zote amekatizwa na kina nani? kinachokosekana kwenye bunge hili ni uvumilivu wa kumsikiliza mwingine, watu wanapenda kumshambulia mwingine lakini hawako tayari kusikiliza wengine wakiwajibu, tunalaumiwa na kila mtu….. hata hatua nilizozichukua ni hatua ndogo tu”
Kabla ya uamuzi wa kutolewa nje ya Viwanja vya bunge haujatolewa, Mbunge wa Iramba Magharibi MWIGULU NCHEMBA ndiye aliyekuwa akichangia Bajeti ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ambapo namkariri hapa akisema “mimi ni ninachokumbuka labda watu wengine kumbukumbu sijua wanakua na hangover gani, kitu ninachokitambua kwamba Rais amekua mtu wa kwanza kukemea jambo la udini, kuna mgombea wa chama kimojawapo alikua anakwenda anaongea na baadhi ya Viongozi wa kidini kama ndio viongozi na mikutano ya ndani ya chama chake, hili linakubalika wapi? wakari CCM inatumia mabalozi, wenyeviti wa tawi…..”
Mbunge wa Longido LEKULE LAIZER ni kama ametabiri kutokea kwa jambo hilo kabla kwani wakati anachangia amepinga vitendo vya vurugu bungeni hali iliyopelekea kuwakumbuka wabunge wa zamani.





CreDits; MillarD Ayo



No comments:

Post a Comment