Baada ya kupata maelezo ya Diamond jana akiiwalaumu
producers wa AM Records kwa kuvujisha wimbo wake huo mpya na ‘Ukimwona’,
Manecky alianza kwa kusema kuwa yeye sio producer
aliyeutengeneza wimbo huo bali ni mdogo wake anaeitwa Bob Maneck, na kwamba
yeye hafahamu makubaliano kati ya Bob Maneck na Diamond kwa kuwa walifanya
wimbo huo bila kumshirikisha yeye.
Alipoulizwa ni kwa nini nyimbo nyingi za Diamond anazofanya
AM Records zinakuwa na matatizo yakiwemo kuvuja akafunguka,
“Nafanya kazi na wasanii wengi lakini kwa nini always nyimbo
za Diamond tu ndo zinakuwa zinavuja, sasa we unadhani ni mimi au ni yeye ndiye
anavujisha nyimbo zake, wewe kama ni mtu mzima na unaakili fikiria mara mbili
halafu utalijua. Kwa sababu so far tunafanya project nyingi, Diamond kwani ni
nani? Ni msanii kama wasanii wengine, tunafanya kazi na wasanii wengi kutoka
nje na ndani ya Tanzania hii, lakini why always nyimbo zake ndo zinavuja. Sasa
matatizo mengine sio yangu mimi ni yake yeye mwenyewe. Kwa sababu nyimbo
tunazofanya lazima achukue anachukua demo.” Alisema Maneck.
Producer huyo ambae ni mshindi wa tuzo za Kili aliendelea
kufuka na kutoa mfano hai wa kuvuja kwa wimbo wa Diamond ambao sasa hivi ni hit
kuwa ilivujishwa na yeye mwenyewe na sio AM Records.
“ kwa mfano ile nini ‘moyo unanidundadunda’(Ukimwona)
alichukua yeye mwenyewe demo, ushanielewa, imehit sawa maclub ina-bang ila ile
ni demo, nyimbo ambayo haiko finalised, mimi ni producer nashangaa kuona nyimbo
ni demo, kwani hamna music department za kuweza kujua hii nyimbo iko mixed au
la? Lakini nyimbo zinabang!..sio kosa langu mimi ni lake yeye kwa sababu yeye
anachukua demo,muda mwingine mimi nachukua blame ambazo yeye.... mbona hakuna
msanii mwingine anayelalamika mimi natoa nyimbo zake, ni yeye tu kila siku
WHY!aagrh..”
Bob alikiri kuwa Diamond aliwafuata pale studio akilalamika
kuhusu wimbo wake kuvuja.
“Kwa sababu mimi
sikujua, alikuja studio ndo akanambia eeh bwana mi nimesikia ngoma ile,
mnachofanya sio poa. Mi nikamwambia wewe ndo unanambia kuwa nyimbo iko mtaani,
lakini nikaja kuthibitisha kuwa kweli nyimbo iliyoko mtaani ni ile version ya
kwanza kabisa, na hapa wanaohusika ni mimi na ManeckY hakuna mtu mwingine yeyote
ambae anaweza kufanya wimbo uka-leak..ila siwezi kusema chochote kwa sababu
sijajua bado, siwezi kusema chochote mimi sasa hivi.”
No comments:
Post a Comment