BBC wameandika kwamba watoto wa Rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela Makaziwe na Zenani Mandela,
wameamua kuchukua hatua za kuwaondoa wasaidizi watatu kutoka katika
makampuni anayoyamiliki wakidai kuwa watatu hao hawana haki ya kuwa
kwenye bodi mbili za kampuni hiyo ambazo ni za thamani ya dola milioni
1.1
Kesi hiyo inakuja wakati kuna
wasiwasi kuhusu afya ya Mandela mwenye umri wa miaka 94 ambae aliondoka
hospitali baada ya kutibiwa mapafu akiwa tayari kalazwa hospitali mara
nne katika kipindi cha miaka miwili.
Kumekuwa na mzozo wa chinichini
tangu mwaka 2005 wa kudhibiti pesa zinazotokana na mauzo kwenye jina la
Mandela hususani picha alizokuwa anachora akiwa jela ambapo Makaziwe na
Zenani Mandela waliwasilisha kesi mahakamani wakidai kuwa Bizo ambae ni
Waziri wa nyumba, Tokyo Sexwale na wakili wa zamani wa Mandela, Bally
Chuene, hawakuwahi kuteuliwa kama wamiliki au wakurugenzi wa kampuni ya
Harmonieux Investment Holdings na Magnifique Investment Holdings
kulingana na gazeti la Star.
Bizos akiwa ni wakili
anayeheshimika sana na ambaye pia ni rafiki wa karibu sana wa Mzee
Mandela amesema kuwa watajitetea vikali katika kesi hiyo na kwamba
Watoto wa Mandela walikuwa wanataka kuuza vitu ambavyo havipaswi kuuzwa.
No comments:
Post a Comment