ushauri

Fay Pub

Fay Pub
Fay Pub Sinza,We Rock,it is a good place to be cool and usalama wa kutosha!!Fay Pub ipo Sinza kumekucha,nyuma ya Seven Up kama unaelekea shamool Hotel,, kwa maelekezo piga namba 0715 556453

tangaza

Saturday, August 18, 2012

M4C MWANZO MWISHO KILOSA VYAMA VINGINE VYAHAHA>

Moja ya Mikutano ya hadhara ya CHADEMA almaarufu kama M4C uliofanyika RUAHA KILOMBERO katika viwanja vya MANYASINI.
Vuguvugu la M4C linaloongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA limeonekana kutikisa Chama cha Wananchi CUF wilayani Kilosa ambapo mbali ya wanachama wengi wa CUF kujiunga CHADEMA pia Mjumbe wa Mkutano Mkuu CUF Taifa, Bwana Wille Lemi alijitoa rasmi CUF na kukabidhiwa kadi na Kiongozi wa upinzani nchini ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk Wilbroad Slaa.
Katika mkutano huo, Dk Slaa aliwataka wananchi wa vyama vyote kuunganisha nguvu kwa pamoja chini ya vuguvugu la M4C ili kuhakikisha katika uchaguzi mkuu ujao wananchi wanapata serikali itakayojali maslahi yao chini ya CHADEMA.
Dk Slaa pia alishukuru mwitikio wa Wanakilosa kutokana na mkutano huo kufurika umati mkubwa wa watu. Mbali na CUF kupoteza wanachama wengi pia mamia ya wanaCCM walikihama chama chao na kujiunga rasmi CHADEMA kuunganisha nguvu katika vuguvugu la M4C. Idadi ya wanachama wapya waliojiunga CDM katika mkutano wa Kilosa walikuwa zaidi ya elfu moja.
Kilosa ilikuwa ni mojawapo ya maeneo yenye wanachama wengi wa CUF lakini inaonekana ziara ya Dk Slaa imesimika rasmi CHADEMA kama chama kinachopendwa zaidi Kilosa.


Source;Mateja

No comments:

Post a Comment