ushauri

Fay Pub

Fay Pub
Fay Pub Sinza,We Rock,it is a good place to be cool and usalama wa kutosha!!Fay Pub ipo Sinza kumekucha,nyuma ya Seven Up kama unaelekea shamool Hotel,, kwa maelekezo piga namba 0715 556453

tangaza

Friday, August 17, 2012

LA "MWANAHALISI" LAHOJIWA BUNGENI.

Kwenye kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri mkuu, Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA alisimama na kumuuliza Waziri mkuu.
Namkariri akiuliza “sheria tunayoizungumzia iiyotumika kulihukumu gazeti la Mwanahalisi ni sheria ambayo imelalamikiwa na wadau wengi wa vyombo vya habari kwa muda mrefu  na ni sheria ambayo inaipa Serikali mamlaka ya ziada kuyadhibiti au bila hata kuyasilikiliza au kuvisikiliza vyombo vya habari pale vinapokua pengine vimeandika taarifa ambazo hazitaipendeza Serikali, madam sheria hii ya msingi ndio imekua tatizo kubwa, wewe huamini Muheshimiwa Waziri mkuu kwamba kutumia sheria mbaya ama sheria kandamizi kunyima haki ni msisitizo wa utawala usio bora?

.
Alichojibu Waziri mkuu ni hiki….. “mimi siamini hivyo muheshimiwa Spika kwa sababu sheria ile imetungwa na bunge lako hili tukufu kwa hiyo ilimradi bado ipo inatumika, ni sheria halali, yaliyomo humo ndio mliosema yako halali kwa hiyo sisi tutaendelea kuitumia mpaka hapo itakapokua imerekebishwa”
Kwenye line nyingine Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema serikali haitoogopa vikwazo vyovyote vitakavyowekwa na nchi wahisani kufuatia kuzisimamisha meli zinazotuhumiwa kupeperusha bendera ya Tanzania wakati asili yake ni Iran.


Source;Millard Ayo

No comments:

Post a Comment