ushauri

Fay Pub

Fay Pub
Fay Pub Sinza,We Rock,it is a good place to be cool and usalama wa kutosha!!Fay Pub ipo Sinza kumekucha,nyuma ya Seven Up kama unaelekea shamool Hotel,, kwa maelekezo piga namba 0715 556453

tangaza

Wednesday, August 22, 2012

LIKE FATHER LIKE SON KUMBE NA BABA YAKE KANUMBA MKALI KWA UIGIZAJI NEXT MONTH KUIGIZA MOVIE KUMUENZI KANUMBA.

Imefahamika kwamba baadhi ya wanafamilia wa Marehemu Steven Kanumba mkoani Shinyanga wameshakamilisha mipango ya kucheza movie yao ya kwanza toka watangaze kuanza kuigiza.
Kambini wanaingia tarehe 30 August 2012, movie wanaanza kucheza tarehe 3 septemba inaitwa Nasikia kuitwa ambapo watakaocheza ni mdogo wake Kanumba kwa upande wa baba aitwae Mjanaheri pamoja na baba mzazi ambapo itachezwa hukohuko Shinyanga.
Movie imetungwa na Mwalimu Emanuel Yahewa ambae ni ndio msimamizi wa kikundi cha Taisee art kilichopo chini ya kanisa la AICT Kambarage  ambapo Marehemu ndipo alikua anaimbia kwaya, alijifunzia gitaa na uigizaji hapo hapo.
Nyumbani kwa kina Kanumba Shinyanga.
Mwanzilishi wa kikundi hicho chenye watu 39 ni Mjanaheri Kanumba ambae amesema movie itakua imekamilika ndani ya mwezi mmoja, kampuni inayoitengeneza ni RJ ya Ray Vicent Kigosi lakini director ni Magulu ambae alikua Director wa Kanumba kwa miaka saba lakini kampuni ya Kanumba haitohusika hata kidogo na utengenezaji wa movie hiyo, baba mzazi wa Marehemu Kanumba atashiriki kucheza pia kama kiongozi wa sungusungu.
Stori yake haihusiani sana na maisha ya Kanumba japo mwishoni mwa hiyo movie kuna baadhi ya vitu vyake vitahusishwa, zikiwemo nyimbo na sehemu kidogo ya maisha yake.
.

Source;Millard Ayo

No comments:

Post a Comment