ushauri

Fay Pub

Fay Pub
Fay Pub Sinza,We Rock,it is a good place to be cool and usalama wa kutosha!!Fay Pub ipo Sinza kumekucha,nyuma ya Seven Up kama unaelekea shamool Hotel,, kwa maelekezo piga namba 0715 556453

tangaza

Saturday, September 21, 2013

MEDIA ZINAUA MUZIKI WA DANCE TANZANIA.

Katika miaka ya karibuni muziki wa dance nchini Tanzania umeonekana kupoteza umaarufu uliokuwa nao kipindi cha nyuma huku lawama za matokeo hayo zikielekezwa kwa vyombo vya habari hususan radio na TV zinazodaiwa kuukumbatia zaidi muziki wa bongo fleva na taarab huku zikuaccha muziki wa dance ukipoteza mwelekeo.

Hiyo ni moja ya sababu kubwa zinazotajwa kuchangia kuporomoka kwa muziki huo nchini Tanzania kama zilivyotolewa na baadhi ya wasanii wenyewe.

Upande wa Khalid Chokoraa wa bendi ya Mapacha watatu amesema, ,
“Ni kwamba muziki wa dansi haushuki ila kubwa zaidi ni kwamba media ndio zilikuwa zimeushusha muziki, ila kuna media zingine wana visingizio vyao wengine wanakwambia nyimbo zenu ndefu ukiwauliza mbona taarab ndefu wanakosa majibu, huyu mwingine akasema , nyimbo zenu sijui mnataja majina, sasa hivi nazo vile vile taarab wanataja majina pia mpaka bongo fleva pia wanataja majina”.
Chokoraa amesema baada ya wanamuziki wa dansi kugundua sababu zinazotolewa na media kushindwa kuwasupport katika kazi zao kama awali, sasa wameamua kuanza kufanya kampeni kubwa ya kuweza kuusaidia muziki wa dansi uweze kurudi pale ulipokuwa.

“saivi kuna wadau wengine wameweza kuji organize kumi, ishirini, wanaanzisha chama chao nia na madhumuni kupambana na muziki wa dansi usonge mbele. Sisi hapa wenyewe tuna chama chetu ambacho tumekianzisha kinaitwa Rhumba turn, kimewakusanya viongozi wote wa mabendi, bendi zote nina maanisha bendi zote za Tanzania….nia na madhumuni ni kupigania muziki wa dansi urudi ulipotoka”. Alisema Chokoraa

No comments:

Post a Comment