ushauri

Fay Pub

Fay Pub
Fay Pub Sinza,We Rock,it is a good place to be cool and usalama wa kutosha!!Fay Pub ipo Sinza kumekucha,nyuma ya Seven Up kama unaelekea shamool Hotel,, kwa maelekezo piga namba 0715 556453

tangaza

Sunday, October 28, 2012

AFANDE SELE AZIDISHA MACHUNGU YA KUGOMBEA UBUNGE BAADA YA NAIBU WAZIRI WA ELIMU MH.PHILIP MULUGO KUCHAPIA HUKO SAUZI.

Baada ya Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi Philip Mulugo kuomba radhi kwa wote waliomfikiria vingine baada ya kuzungumza kwenye mkutano Afrika Kusini kwamba Tanzania ni muungano wa Pemba na Zimbabwe msanii wa bongofleva Afande Sele ametoa maoni yake.
Sele ambae ameahidi kugombea ubunge wa Morogoro mjini 2015 huku akisisitiza kwamba atakua kwenye chama pinzani na sio CCM namkariri akisema “ni jambo lisilofikirika licha ya dhamana ya uwaziri aliyonayo muheshimiwa Waziri inasikitisha, kitu kibaya ni kwamba yeye ni naibu Waziri wa elimu na hilo swala linahusiana na maswala ya kitaaluma, nchi imepata uhuru mwaka gani, imeingia kwenye muungano mwaka gani, imeungana na nchi gani”
“Inasikitisha kwa sababu ni waziri halafu ni Waziri wa Elimu na swala lenyewe linahusiana na swala la kielimu, kama waziri mwenye dhamana ya elimu anashindwa kutambua basi ndio maana wanasema kwamba mtandao mzima wa serikali yetu basi mara nyingi haufanyi kile ambacho watu wanategemea kwamba kingefanywa vizuri, ndio maana inasainiwa mikataba mibovu kwa sababu mtu anawekwa kwenye  nafasi ambazo hakustahili kuwepo” – Afande Sele



Source;Millard ayo

No comments:

Post a Comment