Mh.Zitto Zuberi Kabwe |
Kambi
rasmi ya upinzani bungeni imesema italazimika kuweka wazi taarifa na
majina ya watu wenye umiliki wa fedha katika benki nchini Uswis
zinazofikia bilioni 315.5 kama serikali haitatoa hizo taarifa.
Waziri
kivuli na msemaji mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni Wizara ya
fedha na uchumi Zitto Kabwe amesema hizo fedha zililipwa na makampuni ya
utafutaji mafuta na gesi kwenye pwani ya mkoa wa Mtwara, kampuni ambazo
zilipewa mikataba kati ya mwaka 2004 na 2006.
Nimemkariri
Zitto akiongea bungeni kwamba “kambi rasmi ya upinzani bungeni imepata
taarifa kuwa mmoja wa viongozi wa juu kabisa wa Tanzania na baadhi ya
mawaziri wa serikali ya awamu zilizopita ni miongoni mwa wamiliki wa
fedha hizi, sehemu kubwa ya fedha zililipwa na kampuni za utafutaji wa
mafuta na gesi katika pwani ya mkoa wa Mtwara zilizopewa mikataba kati
ya mwaka 2004 na 2006, kambi rasmi ya upinzani inaitaka serikali kutoa
taarifa rasmi ya hatua gani ambayo imechukua mara baada ya kutolewa kwa
taarifa kutoka benki ya taifa ya Uswis, tunaitaka serikali kuliambia
taifa hatua itakazochukua kurejesha fedha hizi na nyingine zozote
zilizofichwa ughaibuni”
Kuhusu
ishu ya mjadala kuhusu kampuni ya BAE system ya Uingereza, Mh Zitto
amesema “ukilinganisha fedha iliyorejeshwa kama chenchi ya rada na fedha
ambayo Tanzania iliilipa benki ya Barclays, je chenchi ya rada ilikua
na thamani yoyote kifedha? mjadala wa ununuzi wa rada hauwezi kuisha kwa
kufurahia kurejesha chenchi tu, mjadala huu bado mbichi kabisa kwani
tunataka ukweli mtupu uelezwe kwa umma na kuona taifa lilipata hasara
kiasi gani kwa ufisadi huu wa kimataifa na hatua stahiki za kisheria
kuchukuliwa dhidi ya wote walioliingizia taifa hasara”
Baada
ya Zitto Kabwe kumaliza kuwasilisha, Mbunge wa Simanjiro (CCM)
Christopher Ole Sendeka aliomba mwongozo kwa spika na kusema “tuhuma hii
ni kubwa sana nilitaka kuomba mwongozo wako kwamba nani abebe mzigo
huu, ni Zitto ataje majina ya wanaohusika au serikali iwataje hao
wanaohusika katika utoroshaji wa fedha hizo ambazo zimeenda ughaibuni
ili kila mmoja abebe msalaba wake pale itakapothibitika kwamba fedha za
wananchi wa Tanzania zimepelekwa nje ya nchi bila kufata taratibu za
kisheria”
Source:Millard Ayo
No comments:
Post a Comment