Msanii Rose Ndauka ni mmoja kati nyota wanaofanya vizuri kwenye tasnia
ya filamu bongo, ambapo amedai kuwa baada ya kushiriki kwenye filamu
nyingi na kuonesha uwezo wake sasa kama kuna mtu anayehitaji kumtumia
ndani ya kazi yake basi lazima awe na shilingi milioni 10 cash mbali na
hapa itakuwa ngumu kushiriki.
Kiwango cha fedha cha msanii huyo inaonyesha kuwa anajua thamani yake
kama msanii mkubwa anayehitaji kuwa lulu ndani ya tasnia hiyo. Baadhi ya
filamu alizowahi kung’arisha mwanadada huyu ni pamoja na ‘Because of
You’, ‘Love Me Or Love Me Not’ na nyingine nyingi.
Rose alifunguka na kudai kuwa kwa upande wake haoni sababu ya kuficha na
kuendelea kuumia, na ndiyo maana ameamua kuweka wazi ishu hiyo kuwa
hachezi filamu ya mtu bila muafaka wa kiwango cha fedha alichokitaja.
“Inatakiwa tufikie kipindi wasanii tujue thamani yetu kwani wapo baadhi
ya wasanii wengine wana majina makubwa lakini wanafanya filamu kwa bei
za chini, lakini siwezi kulaumu kwani kila mtu anafanya kwa mipango
yake,” alidai.
Source;Mateja20
No comments:
Post a Comment