Kwenye kipindi cha maswali ya
papo kwa papo kwa Waziri mkuu, Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na
Maendeleo CHADEMA alisimama na kumuuliza Waziri mkuu.
Namkariri akiuliza “sheria
tunayoizungumzia iiyotumika kulihukumu gazeti la Mwanahalisi ni sheria
ambayo imelalamikiwa na wadau wengi wa vyombo vya habari kwa muda mrefu
na ni sheria ambayo inaipa Serikali mamlaka ya ziada kuyadhibiti au
bila hata kuyasilikiliza au kuvisikiliza vyombo vya habari pale
vinapokua pengine vimeandika taarifa ambazo hazitaipendeza Serikali,
madam sheria hii ya msingi ndio imekua tatizo kubwa, wewe huamini
Muheshimiwa Waziri mkuu kwamba kutumia sheria mbaya ama sheria kandamizi
kunyima haki ni msisitizo wa utawala usio bora?
Alichojibu Waziri mkuu ni
hiki….. “mimi siamini hivyo muheshimiwa Spika kwa sababu sheria ile
imetungwa na bunge lako hili tukufu kwa hiyo ilimradi bado ipo
inatumika, ni sheria halali, yaliyomo humo ndio mliosema yako halali kwa
hiyo sisi tutaendelea kuitumia mpaka hapo itakapokua imerekebishwa”
Kwenye line nyingine Waziri
Mkuu Mizengo Pinda amesema serikali haitoogopa vikwazo vyovyote
vitakavyowekwa na nchi wahisani kufuatia kuzisimamisha meli
zinazotuhumiwa kupeperusha bendera ya Tanzania wakati asili yake ni Iran.
Source;Millard Ayo
No comments:
Post a Comment