Stori kutoka Kinshasa Congo DRC
zimetoa uthibitisho kwamba mwanamuziki maarufu ambae jina lake lina
uzito ndani na nje ya Afrika Koffi Olomide, amehukumiwa kwenda jela kwa
miaka mitatu au kulipa faini.
Kilichomfanya apigwe hizo nyundo ni fujo alizozifanya akiwa kwenye hoteli moja maarufu Congo DRC pamoja na kumpiga meneja wake.
Nimemsikia mwandishi wa DW
kutoka Congo akisema Koffi alikua akitetewa na zaidi ya mawakili 15
ambapo mamia ya mashabiki wake walihudhuria Mahakamani kusikiliza
kitatokea nini kwenye kesi yake August 16 2012.
kabla ya kufikishwa Mahakamani
Koffi alikamatwa na polisi August 15 jioni muda mfupi tu baada ya
kufanya fujo hizo na kuwekwa kwenye rumande ya mahakama ndogo Kinshasa
kutokana na makosa aliyofanya hotelini ikiwa ni pamoja na kumpiga meneja
wake ambae amekua akiishi Ulaya.
Mwandishi wa DW amesema ugomvi
huo umetokana na Koffi kumdai meneja huyo euro elfu sita ambapo
mashahidi kwenye eneo la tukio wamekiri kwamba Koffi alimpiga ngumi
meneja wake pamoja na kuvunja mlango wa hoteli.
Hata hivyo meneja huyo
aliwasilisha Mahakamani hoja ya kuondoa mashtaka yake dhidi ya Koffi na
kupendekeza kuwepo kwa maridhiano kati yao lakini majaji walilipiga
chini hilo ombi lake.
Baadhi ya wananchi waliotoa
maoni kuhusu hiyo kesi ya Koffi wameunga mkono adhabu hiyo na kusema
amezidisha, Ulaya ni yeye na kwengine ni yeye, mwingine amesema ni safi
kwa sababu hii sio mara ya kwanza kwa yeye kutenda kosa.
Kutokana na adhabu hiyo
kiongozi wa mawakili wanaomtetea Koffi amesema wamepanga kukata rufaa
lakini wanasubiri maoni ya Koffi mwenyewe......Source;Millard Ayo
No comments:
Post a Comment