KATIBU
mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk. Wilbroad, Slaa
jana
alilazimika kuendesha shughuli ya kuomba msaada wa fedha kutoka
kwa watu waliofurika kwenye mkutano wa chama hicho mjini Morogoro ili
kuwachangia wafiwa na walioathirika na vurugu zilizoanzishwa na polisi
dhidi ya wafuasi wa chama hicho.Akifafanua, alisema zitatumika kuwasaidia majeruhi wawili waliopigwa risasi na polisi jana ambao wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.
Pia fedha hizo zitapekwa kwa familia ya marehemu Ally Zolla anayesemekana aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi wakati wa vurugu hizo.
Mmiongoni mwa watu waliozunguka na bakuli hilo ni pamoja na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika.
Fedha hizo hazikufahamika idadi yake hadi mwandishi wetu anaondoka kwenye viwanja hivyo majira ya saa moja usiku.
Source;Mateja
No comments:
Post a Comment