Imefahamika kwamba baadhi ya
wanafamilia wa Marehemu Steven Kanumba mkoani Shinyanga wameshakamilisha
mipango ya kucheza movie yao ya kwanza toka watangaze kuanza kuigiza.
Kambini wanaingia tarehe 30
August 2012, movie wanaanza kucheza tarehe 3 septemba inaitwa Nasikia
kuitwa ambapo watakaocheza ni mdogo wake Kanumba kwa upande wa baba
aitwae Mjanaheri pamoja na baba mzazi ambapo itachezwa hukohuko
Shinyanga.
Movie imetungwa na Mwalimu
Emanuel Yahewa ambae ni ndio msimamizi wa kikundi cha Taisee art
kilichopo chini ya kanisa la AICT Kambarage ambapo Marehemu ndipo
alikua anaimbia kwaya, alijifunzia gitaa na uigizaji hapo hapo.
Mwanzilishi wa kikundi hicho
chenye watu 39 ni Mjanaheri Kanumba ambae amesema movie itakua
imekamilika ndani ya mwezi mmoja, kampuni inayoitengeneza ni RJ ya Ray
Vicent Kigosi lakini director ni Magulu ambae alikua Director wa Kanumba
kwa miaka saba lakini kampuni ya Kanumba haitohusika hata kidogo na
utengenezaji wa movie hiyo, baba mzazi wa Marehemu Kanumba atashiriki
kucheza pia kama kiongozi wa sungusungu.
Stori yake haihusiani sana na
maisha ya Kanumba japo mwishoni mwa hiyo movie kuna baadhi ya vitu vyake
vitahusishwa, zikiwemo nyimbo na sehemu kidogo ya maisha yake.
Source;Millard Ayo
No comments:
Post a Comment