Swali kwenye kichwa cha habari linajieleza. Nani zaidi kati ya Ali
Kiba na Diamond? Tunaposema zaidi tuangalie mambo kadhaa;
muziki,uimbaji,umiliki wa jukwaa,management (kwa maana jinsi msanii
anavyojiongoza au kuongozwa na yeyote aliye nyuma yake), mafanikio ndani
na nje ya nchi, likability yaani jinsi anavyokubalika au hata
kujikubali yeye mwenyewe.Hapo tunaweza kuongeza muonekano…msanii hana
budi kujiweka vizuri..ni kioo
Pages
Search This Blog
ushauri
Fay Pub
tangaza
Thursday, August 30, 2012
Wednesday, August 29, 2012
CHADEMA YACHANGIA WAFIWA MORO.
KATIBU
mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk. Wilbroad, Slaa
jana
alilazimika kuendesha shughuli ya kuomba msaada wa fedha kutoka
kwa watu waliofurika kwenye mkutano wa chama hicho mjini Morogoro ili
kuwachangia wafiwa na walioathirika na vurugu zilizoanzishwa na polisi
dhidi ya wafuasi wa chama hicho.Akifafanua, alisema zitatumika kuwasaidia majeruhi wawili waliopigwa risasi na polisi jana ambao wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.
Pia fedha hizo zitapekwa kwa familia ya marehemu Ally Zolla anayesemekana aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi wakati wa vurugu hizo.
Mmiongoni mwa watu waliozunguka na bakuli hilo ni pamoja na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika.
Fedha hizo hazikufahamika idadi yake hadi mwandishi wetu anaondoka kwenye viwanja hivyo majira ya saa moja usiku.
Source;Mateja
Thursday, August 23, 2012
CHADEMA WAHUJUMIWA KATIKA KAMPENI ZA M4C ULANGA.
Jitihada za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) za kuwafikia
wanachi ili kunadi sera zake, hususan katika mikutano inayoendelea
katika mkoa wa Morogoro, zilikumbana na vikwazo mbali mbali katika
baadhi ya maeneo, kama inavyoonyesha pichani, mtaro uliochimbwa katika
barabara ya kuingia kijiji cha Namgezi kitongoji cha Kambi ya Keya
jimbo la Ulanga Mashariki, kwa lengo la kuzuia magari yasipite.Picha na
Joseph Senga
News source;Mateja20
MGUUU PANDE VIJANA KUANZA DEPO 2012!!!!NI WA O LEVEL NA A LEVEL 2011-2012
JESHI la polisi Tanzania limetoa ajira 1,446 kwa Vijana wa kidato cha
nne wa mwaka 2011,kidato cha sita mwaka 2012 na vijana walioko kambi za
JKT Mafinga, Mlale, Ruvu, Mgambo Oljoro , Bulombola, Kanembwa, Itende,
Nachingwea na Mgulani.
Kati ya hao 951 ni walio hitimu kidato cha nne na sita mwaka 2011/2012
na 495 kwa Vijana waliokuwa katika Kambi za JKT za JKT Mafinga, Mlale,
Ruvu, Mgambo Oljoro , Bulombola, Kanembwa, Itende, Nachingwea na
Mgulani.
Maelekezo Muhimu:-
1. Vijana wa kidato cha nne wa mwaka 2011,kidato cha sita mwaka 2012 na
vijana walioko JKT Mafinga, Mlale, Ruvu, Mgambo Oljoro , Bulombola,
Kanembwa, Itende, Nachingwea na Mgulani waliochaguliwa kujiunga na Jeshi
la Polisi baada ya mchakato wa usaili uliokamilika hivi karibuni
wanatakiwa kuripoti Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi kati ya tarehe
06/10/2011 na 07/10/2012 kwa ajili ya zoezi la usajili litakaloanza
chuoni hapo tarehe 8.10.2012.
2. Vijana hao wanatakiwa kuripoti tarehe 05/10/2012 kwa Makamanda wa
Polisi wa Mikoa kwa ajili ya kuwaandalia usafiri wa kuwapeleka Chuoni.
3. Vijana wanaotoka katika makambi ya JKT yaliyotajwa hapo juu wataripoti kwa makamanda wa Polisi wa mikoa iliyo karibu nao.
Vijana wa kidato cha nne na sita wataripoti kwa makamanda wa Polisi wa
Mikoa waliojiandikisha wakati wa zoezi la usaili lililoendeshwa mwezi
Julai, 2012.
4. Atakaeamua kuripoti kwa Kamanda wa Polisi ambako hakupangiwa atalazimika kujigharimia usafiri hadi Chuo cha Polisi Moshi
5. Vijana hawa wanatakiwa kufika chuoni wakiwa na mahitaji yafuatayo:
a) Vyeti vyao vyote vya masomo(Academic Certificates/Result slip pamoja
na Leaving certificates) kidato cha Nne/Sita, Vyeti vya kuzaliwa
(Original Birth certificates). Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.
b) Mashuka mawili rangi ya Bluu Bahari (light blue)
c) Chandarua
d) Nguo za michezo(Track suit nyeusi,Tshirt blue na Raba)
e) Pasi ya Mkaa
f) Ndoo moja.1
g) Pesa kidogo ya kujikimu.
6. Kwa mujibu wa kanuni za chuo ni marufuku kufika chuoni na simu ya
mkononi, atakayepatikana na simu atafukuzwa chuoni hapo. Chuo
kitaelekeza na kusaidia kufanya mawasiliano.
7. Hakikisha jina lako liko kwenye orodha hii. Jeshi la Polisi
halitahusika na gharama zozote kwa atakaye kiuka maagizo haya.
Source;Mateja20
KILIMO KWANZA KUIKOMBOA TANZANIA RAIS AWA MFANO WA KUIGWA.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa na
mjukuu wao Aziza Ridhiwani (3) katika ghala ya mahindi yaliyovunwa
kwenye shamba lao kijijini Msoga, nje kidogo ya mji mdogo wa Chalinze,
Mkoa wa Pwani. Rais Kikwete ni mkulima na mfugaji kijijini hapo na
ameonesha kufurahishwa sana na mavuno makubwa ya mahindi shambani kwake.
Hii katika kutekeleza kwa vitendo sera ya Serikali ya kuendeleza kwa
ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya sekta ya kilimo katika Tanzania.
Source;Mateja20
BILA MILLIONI KUMI SIFANYI MOVIE NA MTU- ROSE NDAUKA
Msanii Rose Ndauka ni mmoja kati nyota wanaofanya vizuri kwenye tasnia
ya filamu bongo, ambapo amedai kuwa baada ya kushiriki kwenye filamu
nyingi na kuonesha uwezo wake sasa kama kuna mtu anayehitaji kumtumia
ndani ya kazi yake basi lazima awe na shilingi milioni 10 cash mbali na
hapa itakuwa ngumu kushiriki.
Kiwango cha fedha cha msanii huyo inaonyesha kuwa anajua thamani yake
kama msanii mkubwa anayehitaji kuwa lulu ndani ya tasnia hiyo. Baadhi ya
filamu alizowahi kung’arisha mwanadada huyu ni pamoja na ‘Because of
You’, ‘Love Me Or Love Me Not’ na nyingine nyingi.
Rose alifunguka na kudai kuwa kwa upande wake haoni sababu ya kuficha na
kuendelea kuumia, na ndiyo maana ameamua kuweka wazi ishu hiyo kuwa
hachezi filamu ya mtu bila muafaka wa kiwango cha fedha alichokitaja.
“Inatakiwa tufikie kipindi wasanii tujue thamani yetu kwani wapo baadhi
ya wasanii wengine wana majina makubwa lakini wanafanya filamu kwa bei
za chini, lakini siwezi kulaumu kwani kila mtu anafanya kwa mipango
yake,” alidai.
Source;Mateja20
Wednesday, August 22, 2012
LIKE FATHER LIKE SON KUMBE NA BABA YAKE KANUMBA MKALI KWA UIGIZAJI NEXT MONTH KUIGIZA MOVIE KUMUENZI KANUMBA.
Imefahamika kwamba baadhi ya
wanafamilia wa Marehemu Steven Kanumba mkoani Shinyanga wameshakamilisha
mipango ya kucheza movie yao ya kwanza toka watangaze kuanza kuigiza.
Kambini wanaingia tarehe 30
August 2012, movie wanaanza kucheza tarehe 3 septemba inaitwa Nasikia
kuitwa ambapo watakaocheza ni mdogo wake Kanumba kwa upande wa baba
aitwae Mjanaheri pamoja na baba mzazi ambapo itachezwa hukohuko
Shinyanga.
Movie imetungwa na Mwalimu
Emanuel Yahewa ambae ni ndio msimamizi wa kikundi cha Taisee art
kilichopo chini ya kanisa la AICT Kambarage ambapo Marehemu ndipo
alikua anaimbia kwaya, alijifunzia gitaa na uigizaji hapo hapo.
Mwanzilishi wa kikundi hicho
chenye watu 39 ni Mjanaheri Kanumba ambae amesema movie itakua
imekamilika ndani ya mwezi mmoja, kampuni inayoitengeneza ni RJ ya Ray
Vicent Kigosi lakini director ni Magulu ambae alikua Director wa Kanumba
kwa miaka saba lakini kampuni ya Kanumba haitohusika hata kidogo na
utengenezaji wa movie hiyo, baba mzazi wa Marehemu Kanumba atashiriki
kucheza pia kama kiongozi wa sungusungu.
Stori yake haihusiani sana na
maisha ya Kanumba japo mwishoni mwa hiyo movie kuna baadhi ya vitu vyake
vitahusishwa, zikiwemo nyimbo na sehemu kidogo ya maisha yake.
Source;Millard Ayo
Saturday, August 18, 2012
WEMA AHUSIKA BIFU LA BOB JUNIOUR NA DIAMOND PLATNUMZ.
Ikiwa ni siku chache tu toka diamond abadilishe jina kuepuka makuu na
Bob junior bado choko choko za vijana hawa zinazidi kupamba moto. jioni
ya jana habari zilizopatikana ni kwamba Bob junior ametangaza kuwa
Diamond ameshuka kimuziki hivyo ameamua kutembea na Wema sepetu ili
kurudisha jina lake.. baya zaidi amesema kuwa huyo Wema sepetu ni malaya
tu so Diamond hajapata lolote... Kisanga kikazidi zaidi baada ya Wema
sepetu kujibu shutuma za Bob junior katika kipindi cha movie leo
kinachorushwa cloudfm kila asubuhi, Wema anasema" kwanza who is
sharobaro??? kwanza hata mazoea naye sina.. why bifu zake za kuime na
Diamond aniingize na mimi msichana? au ana wivu na mimi alikuwa anamtaka
yeye diamond??
Source;Martin Kadinda
PUSH MOBILE KUSAIDIA WASANII WA TANZANIA KUENJOY JASHO LAO.
KAMPUNI ya Push Mobile Limited imeahidi kuboresha kazi za
wanamuziki pamoja na asilimia ya malipo yanayotokana na milio na miito
ya simu.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Freddie Manento katika mkutano na wanamuziki na wadau wa muziki uliofanyika kwenye hotel ya Serena.
Manento alisema hayo baada ya kuweka bayana mchakato mzima wa mfumo wa biashara ya muziki Tanzania katika mkutano uliohudhuria na wasanii zaidi ya 80 wa muziki wa aina tofauti ikiwa kama injili, bongo fleva, muziki wa dansi, taarab na reggae, hip hop na watayarishaji mbali mbali (producers).
Alisema kuwa kwa sasa Push Mobile inatoa wastani wa asilimia 20 mpaka 40 kwa mwanamuziki pamoja na wadau wao . Alisema kuwa kiwango hicho hutolewa baada ya wao kupokea kutoka kwa mitandao ya simu kati ya asilimia 35 mpaka 60.
“Lengo letu ni kuona wanamuziki wanafaidika na kazi zao hasa kupitia milio na miito ya simu, biashara ambayo kwa sasa imewaingizia kipato kikubwa wanamuziki baada ya kuanguka kwa soko la mauzo ya albamu e na kutopata kipato chochote kutoka kwenye redio na televisheni kama ilivyoelezwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano , Sayansi na Teknolojia wakati anajibu hoja ya Mbunge wa Chadema, Zitto Kabwe,” alisema Manento.
Alisema kuwa asilimia ngapi wataongeza, itatokana na majadiliano na kampuni za mitandao ya simu na hata kama kampuni hizo zitakataa kuongeza ili kuwafaidisha wasanii, wao wataongeza tu.
Alifafanua kuwa kampuni yao imekuwa ikiingia gharama kubwa za kiuendeshaji katika kupromoti nyimbo za wasanii ili kuweza kupata soko.
“Tunatumia si chini ya milioni 25 kwa mwezi kwa ajili ya kuandaa matangazo na kudhamini vipindi katika redio na televisheni kwa ajili ya kupromoti nyimbo za wasanii ili kuweza kupata masoko, pia tunatumia zaidi ya million 7 kwa kazi ya kutengeneza nyimbo ili ziwezwe kuingizwa katika mifumo mbali mbali ya simu za mikononi,” alisema.
Kuhusiana na kuchelewa kwa malipo ya wanamuziki, Manento alisema kuwa tatizo hilo linatokana na ucheleweshwaji wa wadau husika kufanya malipo kwa wakati.
“Push imejitahidi kuondoa tatizo hilo kwa kuwalipa wanamuziki kwa fedha zake huku ikiendelea kudai kutoka kwa wadau husika ambao mara nyingine ukaa miezi sita bila kutulipa, ni changamoto kwetu, lakini tumejitahidi kufikia malengo na kutatua matatizo kwa wasanii, japo changamoto ni kubwa, nawaomba wanamuziki kuelewa tatizo hilo, ” alisema.
Akizungumza katika mkutano huo mtayarishaji maarufu wa muziki nchini, John Water Sharizo au Man Water aliipongeza Push Mobile kwa jitihada zake za kuinua kipato kwa wanamuziki kwani zamani walikuwa wananyonywa sana katika mauzo ya albamu.
Man Water alisema kuwa ni jukumu la Push Mobile ambayo inafanya kazi na wanamuziki wengi hapa nchini kuhakikisha kuwa wateja wake wanapata faida na kazi zao kwani wao ndiyo wameingia mikataba na wanamuziki na wala siyo makampuni ya simu.
Alisema kuwa wanashukuru kwa kipato kilichopo kwani hapo awali walikuwa wanachapisha CD au kaseti 200 na kuuzwa mwaka mzima bila kupata mrahaba kinyume na sasa.
Wanamuziki mbali mbali walihudhuria mkutano huo walifuraishwa sana kwani waliweza kuweka hadharani kero zao mbali mbali na kujibiwa na mkurugenzi huyo na kuridhishwa.

M4C MWANZO MWISHO KILOSA VYAMA VINGINE VYAHAHA>
Moja ya Mikutano ya hadhara ya CHADEMA almaarufu kama M4C uliofanyika RUAHA KILOMBERO katika viwanja vya MANYASINI. |
Vuguvugu
la M4C linaloongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA
limeonekana kutikisa Chama cha Wananchi CUF wilayani Kilosa ambapo mbali
ya wanachama wengi wa CUF kujiunga CHADEMA pia Mjumbe wa Mkutano Mkuu
CUF Taifa, Bwana Wille Lemi alijitoa rasmi CUF na kukabidhiwa kadi na
Kiongozi wa upinzani nchini ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk
Wilbroad Slaa.
Katika mkutano huo, Dk Slaa aliwataka wananchi wa vyama vyote kuunganisha nguvu kwa pamoja chini ya vuguvugu la M4C ili kuhakikisha katika uchaguzi mkuu ujao wananchi wanapata serikali itakayojali maslahi yao chini ya CHADEMA.
Dk Slaa pia alishukuru mwitikio wa Wanakilosa kutokana na mkutano huo kufurika umati mkubwa wa watu. Mbali na CUF kupoteza wanachama wengi pia mamia ya wanaCCM walikihama chama chao na kujiunga rasmi CHADEMA kuunganisha nguvu katika vuguvugu la M4C. Idadi ya wanachama wapya waliojiunga CDM katika mkutano wa Kilosa walikuwa zaidi ya elfu moja.
Kilosa ilikuwa ni mojawapo ya maeneo yenye wanachama wengi wa CUF lakini inaonekana ziara ya Dk Slaa imesimika rasmi CHADEMA kama chama kinachopendwa zaidi Kilosa.

Friday, August 17, 2012
AIRTEL TANZANIA KUKIMBIZA KOTEKOTE.
Airtel Tanzania, imeendeleza dhamira yake katika kuboresha elimu kwa kuchezesha droo iliyochagua shule za sekondari 93 zitakazo faidika na mradi wa vitabu wa Airtel wa kusaidia jamii unaojulikana kama Airte shule yetu kwa mwaka 2012 -2013 Akiongea katika mkutano na vyombo vya Habari Mkurugenzi wa Airtel Kitengo cha Mawasiliano Bi, Beatrice Singano Mallya alisema "Mwaka huu.
Airtel tunaendelea na dhamira yetu ya kusaidia elimu kwa kuzipatia vitabu shule za sekondari 93, Mradi huu utafaidisha shule 3 kutoka katika kila mkoa Tanzania bara na visiwani.
Shule 93 zilizo chaguliwa leo ni matokeo ya droo iliyochezeshwa na kuzichagua shule hizo kutoka shule 3,000 zilizopendekezwa na Wizara ya Elimu Tanzania kuwa ni shule ambazo zina uhitaji mkubwa wa vitabu na kushauri ziingie katika mpango wa kusaidia jamii wa Airtel shule
yetu.
"Toka tulivyooanza mradi huu wa Vitabu miaka saba iliyopita tumeweza kuzifikia zaidi ya shule 1000 za sekondari zilizopo Tanzania bara na visiwani kwa kutoa msaada sawa kwa mikoa yote na kuwafikia wanafunzi katika kila kona ya Tanzania.
Mwaka huu vitabu tunavyogawa vinakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 110, hivyo kila shule iliyopatikana kwenye droo hii watapata Vitabu alisema Mallya.
Bi Mallya aliongeza kwa kusema "tumefanya kazi kwa pamoja na Mamlaka ya elimu na Wizara ya Elimu Tanzania kwa kuhakikisha kwamba mahitaji ya vitabu kwa shule zote zitakazoingia kwenye Mradi huu wa Shule yetu tunayatimiza kwa kuwapatia vitabu vya mitaala ya masomo yao kama ilivyopendekezwa na Wizara"
"Airtel Tanzania imekuwa mstari wa mbele kwa kutoa misaada mbalimbali ili kuisaidia jamii hapa Tanzania hasa kwa kuchangia sekta ya elimu kwa kuwapatia vitendea kazi vikiwemo Vitabu kwa wanafunzi wa shule za sekondari.
Mwaka jana pia Airtel ilisaidia Vitabu vyenye thamani ya zaidi ya milioni 104 tsh kwa shule za sekondari kwa kupitia droo iliyohusisha jumla ya shule 502" alisema Bi, Mallya.
Nae Afisa Mkuu Mwandamizi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bw Masozi Nyirenda aliongea kwa Niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ulimu (TEA) alisema "Mamlaka ya Elimu Tanzania tunawashukuru sana Airtel kwa dhamira yenu ya kusaidia jamii kwa kuinua kiwango cha elimu hapa nchini " Mradi wa Airtel Shule Yetu ni mradi mzuri sana kwa jamii yetu kwa kuinua kiwango cha elimu na maisha ya watanzania"
Tunaamini elimu ndio ufunguo wa maisha hivyo watanzania wote pamoja na waalimu mtakaopokea vitabu hivi vya mradi wa Airtel Shule yetu tuvitunze na kuvitumia vizuri ili kuunga mkono jitihada za Airtel katika kusaidia kuinua kiwango cha elimu hapa nchini" aliongeza kwa
kusema Bw. Nyirenda
Mbali na shule 93 za sekondari zitakazofaidika na mradi huu wa vitabu mwaka huu, pia Airtel Tanzania imeshamaliza kukarabati shule ya msingi ya Kiromo iliyopo nje kidogo ya jiji la DSM kando kando na barabara ya bagamoyo ilichaguliwa mwaka jana 2011 huku mipango mingine ya mwaka huu ikiendelea ili kupata shule nyingine itakayofaidika kwa kujengwa na kukarabatiwa na Airtel shule Yetu Airtel bado itaendelea kushirikiana wizara ya elimu kwa wadau wengine kuweza kushiriki katika kuinua kiwango cha elimu hapa Tanzania.
Source;Mateja
MOPAO MOKONZI a.k.a KOFII OLOMIDE MATATANI.
Stori kutoka Kinshasa Congo DRC
zimetoa uthibitisho kwamba mwanamuziki maarufu ambae jina lake lina
uzito ndani na nje ya Afrika Koffi Olomide, amehukumiwa kwenda jela kwa
miaka mitatu au kulipa faini.
Kilichomfanya apigwe hizo nyundo ni fujo alizozifanya akiwa kwenye hoteli moja maarufu Congo DRC pamoja na kumpiga meneja wake.
Nimemsikia mwandishi wa DW
kutoka Congo akisema Koffi alikua akitetewa na zaidi ya mawakili 15
ambapo mamia ya mashabiki wake walihudhuria Mahakamani kusikiliza
kitatokea nini kwenye kesi yake August 16 2012.
kabla ya kufikishwa Mahakamani
Koffi alikamatwa na polisi August 15 jioni muda mfupi tu baada ya
kufanya fujo hizo na kuwekwa kwenye rumande ya mahakama ndogo Kinshasa
kutokana na makosa aliyofanya hotelini ikiwa ni pamoja na kumpiga meneja
wake ambae amekua akiishi Ulaya.
Mwandishi wa DW amesema ugomvi
huo umetokana na Koffi kumdai meneja huyo euro elfu sita ambapo
mashahidi kwenye eneo la tukio wamekiri kwamba Koffi alimpiga ngumi
meneja wake pamoja na kuvunja mlango wa hoteli.
Hata hivyo meneja huyo
aliwasilisha Mahakamani hoja ya kuondoa mashtaka yake dhidi ya Koffi na
kupendekeza kuwepo kwa maridhiano kati yao lakini majaji walilipiga
chini hilo ombi lake.
Baadhi ya wananchi waliotoa
maoni kuhusu hiyo kesi ya Koffi wameunga mkono adhabu hiyo na kusema
amezidisha, Ulaya ni yeye na kwengine ni yeye, mwingine amesema ni safi
kwa sababu hii sio mara ya kwanza kwa yeye kutenda kosa.
Kutokana na adhabu hiyo
kiongozi wa mawakili wanaomtetea Koffi amesema wamepanga kukata rufaa
lakini wanasubiri maoni ya Koffi mwenyewe......Source;Millard Ayo
BANK YA KCB MOROGORO YATOA MSAADA WA MADAWATI.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya madawati hayo, Meneja wa KCB Tawi la Morogoro Carlos Msigwa alisema kuwa lengo la msaada huo lilikuwa kusaidia upungufu wa madawati katika shule hiyo na hivyo kuwawezesha wanafunzi kusoma vizuri
Meneja huo alisema kuwa Benki ya KCB inatambua umuhimu wa elimu bora katika maendeleo ya taifa na ndiyo maana haikusita kuelekeza msaada huo katika sekta ya elimu.
Akipokea msaada huo, diwani wa kata ya Mkundi Emelda Chambo aliishukuru Banki ya KCB kwa kutoa msaada na kusema kuwa utakuwa chachu kubwa katika maendeleo ya elimu katika shule hiyo ambayo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa madawati.
Tuaishukuru sana KCB kwani wamekuwa kama walezi kwa shule yetu. Hii ni mara ya tatu kupokea msaada baada ya ule wa miti ya kivuli pamoja na vitabu.Tunaahidi kuyatunza madawati haya ili mtakaporudi tena myakute katika hali nzuri.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Philemon Kibuja shule hiyo yenye wanafunzi 400 imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo ukosefu mkubwa wa madawati.
“Mimi ndiyo mwalimu mkuu na mwalimu pekee katika shule hii. Nafundisha kuanzia darasa la kwanza hadi la saba. Shule hii kabla ya kupata msaada huu kutoka KCB haikuwa na dawati hata moja. Wanafunzi walilazimika kukaa chini, kwenye magogo na kwenye mabenchi,’ alisema
Mwalimu huyo aliishukuru Benki ya KCB na kuomba serikali pamoja na makampuni binafsi kuidia shule hiyo ambayo wanafunzi wengi wanatoka katika jamii za wafugaji.
“Shule hii yenye wanafunzi 400 ina madarasa matatu tu na mwalimu ni mimi peke yangu. Pamoja na jitihada kubwa ya kuomba msaada serikalini, serikali haijaweza kutusaidia. Tunaomba mashirika mbalimbali kujitikeza kutusaidia,” alisema
LA "MWANAHALISI" LAHOJIWA BUNGENI.
Kwenye kipindi cha maswali ya
papo kwa papo kwa Waziri mkuu, Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na
Maendeleo CHADEMA alisimama na kumuuliza Waziri mkuu.
Namkariri akiuliza “sheria
tunayoizungumzia iiyotumika kulihukumu gazeti la Mwanahalisi ni sheria
ambayo imelalamikiwa na wadau wengi wa vyombo vya habari kwa muda mrefu
na ni sheria ambayo inaipa Serikali mamlaka ya ziada kuyadhibiti au
bila hata kuyasilikiliza au kuvisikiliza vyombo vya habari pale
vinapokua pengine vimeandika taarifa ambazo hazitaipendeza Serikali,
madam sheria hii ya msingi ndio imekua tatizo kubwa, wewe huamini
Muheshimiwa Waziri mkuu kwamba kutumia sheria mbaya ama sheria kandamizi
kunyima haki ni msisitizo wa utawala usio bora?
Alichojibu Waziri mkuu ni
hiki….. “mimi siamini hivyo muheshimiwa Spika kwa sababu sheria ile
imetungwa na bunge lako hili tukufu kwa hiyo ilimradi bado ipo
inatumika, ni sheria halali, yaliyomo humo ndio mliosema yako halali kwa
hiyo sisi tutaendelea kuitumia mpaka hapo itakapokua imerekebishwa”
Kwenye line nyingine Waziri
Mkuu Mizengo Pinda amesema serikali haitoogopa vikwazo vyovyote
vitakavyowekwa na nchi wahisani kufuatia kuzisimamisha meli
zinazotuhumiwa kupeperusha bendera ya Tanzania wakati asili yake ni Iran.
Source;Millard Ayo
Thursday, August 16, 2012
BIG UP MUSEVENI NAMNA HII MOTISHA INAKUA.
Baada ya kurudi home, Maelfu ya
waganda wamempokea Stephen Kiprotich mshindi wa medali ya dhahabu
kwenye riadha ya Olympic 2012 ambapo ameifanya Uganda itangazwe mshindi
wa medali hiyo baada ya miaka 40.
Kiprotich ambae ni askari
magereza alieshinda kwenye mbio za wanaume jumapili iliyopita ndani ya
Olypic 2012, amezawadiwa cheki ya dola za kimarekani elfu 80 ambazo
zimetolewa na Rais Yoweri Museveni ambae pia amempandisha cheo mara tisa
kwenye kazi yake ya uaskari Magereza.
Standard Media wameripoti
kwamba mzigo ulikua mzito manake watu walipanga foleni kumpokea Stephen
huko Entebbe akiwa amebebwa kwenye gari ambalo lilikua na plate namba
iliyoandikwa UG GOLD.
Watu walikua wengi mpaka
waliziba njia ambapo magari yaliyokua kwenye msafara yalikosa pa kupita
wakati yakielekea ikulukumpeleka Stephen kunywa chai asubuhi na Rais
Museveni.
Baada ya Kiprotich kupewa cheki
yake ya dola elfu 80, alimuomba rais Museveni kuwajengea wazazi wake
nyumba kaskazini mashariki mwa Uganda ambapo rais Museveni amekubali
kujenga hiyo nyumba ya vyumba vitatu.
Stephen Kiprotich |
Kwenye line nyingine ni kwamba
rais Museven ameahidi kwamba katika muda ujao, mwanamichezo yoyote wa
Uganda atakaeshinda medali ya kimataifa, atakua analipwa shilingi
shilingi milioni moja za Uganda kila mwezi.
Source;Millard Ayo
UNYAMA NA UKATILI WANAOFANYIWA WASICHANA.
MWANAFUNZI wa darasa la saba Shule ya Msingi Hogolo, wa umri wa miaka 14 (jina limehifadhiwa) ambaye ni Mkazi wa Mtaa wa Ikulu Kijiji cha Hogolo wilayani Kongwa, mkoani Dodoma ameuawa kwa kunyongwa na kuzikwa kwenye shimo nyuma ya nyumba yao karibu na choo baada ya kubakwa.
Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa chanzo cha mauaji hayo yaliyofanyika Jumamosi iliyopita ni wivu wa kimapenzi kwani marehemu enzi za uhai wake, anadaiwa alikuwa amevunja uhusiano na mpenzi wake wa muda mrefu, Heri Aboubakar na kuanzisha uhusiano mpya na Wilfredy Muhaha maarufu Kabo.
Hata hivyo bado haijafahamika muuaji halisi wa marehemu huyo licha ya polisi kuwashikilia watu kadhaa kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo akiwemo mpenzi wake wa sasa, Muhaha.
Mbali na Muhaha wengine wanaoshikiliwa Polisi ni Ashad Jafari ambaye ni mkulima na mkazi wa Mtaa wa Nyerere Hogolo ambaye ni rafiki wa marehemu na Rino Mazoea, mkulima na mkazi wa Ikulu Hogolo wilayani Kongwa ambaye ni kaka wa marehemu.
Kamanda Zelothe Steven alisema wanamtafuta Aboubakar ambaye amekimbia kijijini hapo na hajulikani alipo mpaka sasa. Katika tukio hilo, kaka wa marehemu ambaye pia anashikiliwa Polisi, katika maelezo yake ya awali alidai kusikia purukushani zikitokea usiku wa tukio hilo la mauaji lakini hakutoka usiku huo kushuhudia nini kinaendelea.
Marehemu alikuwa akiishi na babu na bibi yake hapo kijijini na siku ya tukio , walezi hao, walikuwa wameondoka kwenda katika vijiji vya jirani, ambapo bibi yake alikuwa amekwenda Kongwa kwa ajili ya kujengea makaburi na babu yake alikwenda Kijiji cha Banyi Banyi kutembelea wagonjwa.
SOurce;HABARI LEO
UPINZANI WAFUNGUKIA MABILLIONI YA VIGOGO "HUU SI WIZI"(USWISSI)
Mh.Zitto Zuberi Kabwe |
Kambi
rasmi ya upinzani bungeni imesema italazimika kuweka wazi taarifa na
majina ya watu wenye umiliki wa fedha katika benki nchini Uswis
zinazofikia bilioni 315.5 kama serikali haitatoa hizo taarifa.
Waziri
kivuli na msemaji mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni Wizara ya
fedha na uchumi Zitto Kabwe amesema hizo fedha zililipwa na makampuni ya
utafutaji mafuta na gesi kwenye pwani ya mkoa wa Mtwara, kampuni ambazo
zilipewa mikataba kati ya mwaka 2004 na 2006.
Nimemkariri
Zitto akiongea bungeni kwamba “kambi rasmi ya upinzani bungeni imepata
taarifa kuwa mmoja wa viongozi wa juu kabisa wa Tanzania na baadhi ya
mawaziri wa serikali ya awamu zilizopita ni miongoni mwa wamiliki wa
fedha hizi, sehemu kubwa ya fedha zililipwa na kampuni za utafutaji wa
mafuta na gesi katika pwani ya mkoa wa Mtwara zilizopewa mikataba kati
ya mwaka 2004 na 2006, kambi rasmi ya upinzani inaitaka serikali kutoa
taarifa rasmi ya hatua gani ambayo imechukua mara baada ya kutolewa kwa
taarifa kutoka benki ya taifa ya Uswis, tunaitaka serikali kuliambia
taifa hatua itakazochukua kurejesha fedha hizi na nyingine zozote
zilizofichwa ughaibuni”
Kuhusu
ishu ya mjadala kuhusu kampuni ya BAE system ya Uingereza, Mh Zitto
amesema “ukilinganisha fedha iliyorejeshwa kama chenchi ya rada na fedha
ambayo Tanzania iliilipa benki ya Barclays, je chenchi ya rada ilikua
na thamani yoyote kifedha? mjadala wa ununuzi wa rada hauwezi kuisha kwa
kufurahia kurejesha chenchi tu, mjadala huu bado mbichi kabisa kwani
tunataka ukweli mtupu uelezwe kwa umma na kuona taifa lilipata hasara
kiasi gani kwa ufisadi huu wa kimataifa na hatua stahiki za kisheria
kuchukuliwa dhidi ya wote walioliingizia taifa hasara”
Baada
ya Zitto Kabwe kumaliza kuwasilisha, Mbunge wa Simanjiro (CCM)
Christopher Ole Sendeka aliomba mwongozo kwa spika na kusema “tuhuma hii
ni kubwa sana nilitaka kuomba mwongozo wako kwamba nani abebe mzigo
huu, ni Zitto ataje majina ya wanaohusika au serikali iwataje hao
wanaohusika katika utoroshaji wa fedha hizo ambazo zimeenda ughaibuni
ili kila mmoja abebe msalaba wake pale itakapothibitika kwamba fedha za
wananchi wa Tanzania zimepelekwa nje ya nchi bila kufata taratibu za
kisheria”
Source:Millard Ayo
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akitoa wosia kwa wanafunzi 20 waliofanya vizuri
katika mitihani ya kidato cha sita kwa mwaka 2012 bungeni leo mjini
Dodoma. Wanafunzi hao 10 wasichana na 10 wavulana wamepewa cheti ,
kopyuta ya pakato (laptop) na fedha taslimu shilingi laki mbili kwa kila
mmoja. WAZIRI
Mkuu, Mizengo Pinda amewataka wanafunzi wote nchini kuwa na nidhamu ,
kujituma na kufuata maelekezo vizuri ya walimu wao na kuepuka makundi
mabaya ili kuweza kupata mafanikio katika masomo yao.
Aidha Waziri Mkuu Pinda amewaasa wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani wa kuhitimu kidato cha sita wa mwaka huu kutumia uhuru vizuri watakaoupata kwenye maisha ya vyuo vya elimu ya juu bila kurudi nyuma katika maendeleo ya masomo yao.
Kauli hiyo ilitolewa leo na Waziri Mkuu, Pinda Bungeni mjini Dodoma kabla ya kuwatunuku vyeti vya kuwapongeza wanafunzi hao 19 kati 20 waliofanya vizuri katika mtihani huo,kutoka shule mbalimbali nchini, ambapo mmoja wao, Jamal Juma yuko nje ya nchi.
Wanafunzi hao ambao wote walipata ufaulu wa daraja la kwanza katika mtihani huo, saba kati yao wanatoka katika shule ya wasichana ya Marian, watatu Mzumbe, wawili Fedha na wengine wawili Kibaha. Waliobakia mmoja mmoja anatoka Kilakala, Ufundi Ifunda, Tabora girls, Tabora boys, Minaki na Mpwapwa.
Mmefanya vizuri. Mnastahili ! Hongereni Sana. Tunataka ufaulu wenu uwe mzuri zaidi kwa vile sasa ninyi mnakweda kujenga weledi. Mnakuwa wataalamu wa fani Fulani. Tumieni muda wenu kujifunza zaidi kutafuta maarifa zaidi na kuvumbua mambo makubwa zaidi yatakayowasaidia ninyi wenywe na jamii kwa ujumla kujiletea maendeleo alisema Waziri Mkuu Pinda.
Aliongeza kuwa ni vizuri utaratibu huo wa kuwatambua wanafunzi bora uwe endelevu na ikiwezekana wapatiwe fursa ya kuendelezwa katika vyuo vikuu vya kipekee nje ya nchi hususan kwenye fani zitakazojenga uwezo kwa taifa
Waziri Mkuu alisema kati ya shule 10 ,ambazo wanafunzi hao wanatoka, wawili ni kutoka shule za kata, ambao ni Ester Marcel toka shule ya sekondari ya wasichana ya Olele Kilimanjaro na Brighton Lema toka shule ya sekondari ya Kitangiri, Mwanza.
Napenda niwape pongezi za pekee wanafunzi hawa kwa jihudi kubwa walizozionesha. Kufaulu kwao kunadhihirisha kwamba shule hizi za kata tukiweka bidii kwa kuziwezesha zaidi zitafanya vizuri zaidi kama ilivyo katika shule nyingine.
Waziri Mkuu pia aliwataka walimu wote nchini kushirikiana na wazazi na serikali kwa pamoja kufundisha watoto kwa bidii ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao kama wanafunzi hao waliotunukiwa vyeti hivyo.
Kwa upande wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa alisema wanafunzi hao watazawadiwa pakato (laptop) na sh. 200,000, pia kila shule iliyotoa mwanafunzi bora itazawadiwa sh. milioni moja katika hafla maalum itakayofanyika jioni.
Wanafunzi hao wanatoka katika mchepuo wa PCM ambao ni 16 na mmojammoja toka mchepuo wa PGM, CBA, ECA na HKL.
Naye Spika wa Bunge la Jamhuri, Anna Makinda aliwataka wanafunzi hao kuwa makini na makundi kwa kuyasilikiza huku wakitumia akili zao huku akitoa changamoto shule nyingine kujitahidi kufanya vizuri.
Wanafunzi 20 waliofanya vizuri katika mitihani wa kidato cha sita kwa mwaka 2012 wakiwa katika picha ya pamoja nje ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma. Wanafunzi hao 10 wasichana na 10 wavulana wamepewa cheti na Waziri Mkuu, kopyuta ya pakato (laptop) na fedha taslimu shilingi laki mbili kwa kila mmoja.
source:Mateja

T.O namba mbili Tanzania Zawadi Mdoe(mwenye t shirt ya kijani) | ,nilibahatika kusoma nae o level. |
Waziri Mkuu Mh.Mizengo Pinda |
Wednesday, August 15, 2012
WENJE AFUNGUKA MAGUMASHU ELIMU YA BONGO.
Mbunge wa Nyamagana Mwanza kwa
ruhusa ya Chadema na wananchi wa jimbo lake Ezekiah Wenje amewataka
wabunge wa bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kuacha unafiki na
badala yake waitishe mjadala wa kitaifa kuhusu lugha maalum ya
kufundishia kwa shule za msingi.
Namkariri akisema “lugha kwenye
primary school ni Kiingereza au kiswahili? mimi nawachallenge acheni
unafiki, kama ni Kiswahili iwe Kiswahili kwenye primary School kama ni
Kiingereza basi na hizo shule za Serikali zifundishe kiingereza ili
wanafunzi wapate hiyo Knowledge ya kiingereza, wanafunzi wa watu masikini pia wapate kama watoto wenu wanavyopata”
Akichangia makadirio ya mapato
na matumizi ya wizara ya Elimu, Wenje amesema wakati wabunge wakipigia
debe matumizi ya kiswahili wenyewe pia wamekua wakisomesha watoto wao
kwenye shule zinazotumia lugha ya kiingereza
.
source:Millard Ayo
Mbunge wa Nyamagana Mwanza kwa ruhusa ya Chadema na wananchi wa jimbo lake Ezekiah Wenje amewataka wabunge wa bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kuacha unafiki na badala yake waitishe mjadala wa kitaifa kuhusu lugha maalum ya kufundishia kwa shule za msingi.
Namkariri akisema “lugha kwenye primary school ni Kiingereza au kiswahili? mimi nawachallenge acheni unafiki, kama ni Kiswahili iwe Kiswahili kwenye primary School kama ni Kiingereza basi na hizo shule za Serikali zifundishe kiingereza ili wanafunzi wapate hiyo Knowledge ya kiingereza, wanafunzi wa watu masikini pia wapate kama watoto wenu wanavyopata”
Akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya wizara ya Elimu, Wenje amesema wakati wabunge wakipigia debe matumizi ya kiswahili wenyewe pia wamekua wakisomesha watoto wao kwenye shule zinazotumia lugha ya kiingereza
.
source:Millard Ayo
Tuesday, August 14, 2012
BIASHARA INAYODHARAULIKA TANZANIA YENYE KIPATO KIKUBWA SANA.
Utengenezaji wa katuni ama kwa kiswahili VIKARAGOSI ni moja kati ya biashara ambazo zina vipato vikubwa sana ingawaje muamko wake kwa nchi maskini kama Tanzania bado uko chini sana.
Hilo linaweza kujidhihirisha kwa swali moja dogo sana ambalo ni nani kati yetu ambae hajawahi kuiona katuni ya KIRIKOU?! jibu liko wazi kabisa kwamba hakuna ambae hajawahi kuiona sasa jiulize ni shillingi ngapi alipata muandaaji wa katuni hio ukiondoa PIRACY yaani unyonyaji usio halali??
CHADEMA KUWASHA MOTO RUAHA KILOMBERO LEO
Chama cha Demokrasia na Maendeleo leo hii tarehe 14 August wanatarajia kufanya mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya manyasini ambapo Dk.Wilbrod Slaa anatarajiwa kuwahutubia wananchi ikiwa ni pamoja na kupokea wanachama wapya,pia ikiwa ni moja na mikutano ya vugu vugu la mabadiliko yaani M4C ikiwa na kauli mbiu ya VUA GAMBA NA VAA GWANDA>
TUJIKUMBUSHE:
Mapema mwezi wa tano mwaka huu zilizuka vurugu katika uchaguzi mdogo wa kijiji ambao uliwahusisha wanachama wa CCM na CHADEMA.
Subscribe to:
Posts (Atom)