ushauri

Fay Pub

Fay Pub
Fay Pub Sinza,We Rock,it is a good place to be cool and usalama wa kutosha!!Fay Pub ipo Sinza kumekucha,nyuma ya Seven Up kama unaelekea shamool Hotel,, kwa maelekezo piga namba 0715 556453

tangaza

Tuesday, September 11, 2012

MKE WA OBAMA MICHELLE OBAMA ATOA SUPPORT KWA MUMEWE BARACK OBAMA KWA UCHAGUZI UJAO.

Mke wa rais wa Marakeni Barack Obama, Michelle Obama amemuunga mkono mumewe katika mkutano mkuu wa chama cha Democratic akiomba rais huyo apewe muda zaidi.

Bibi Obama amekiri kuwa mabadiliko ambayo mumewe Barack Obama aliahidi wakati wa kampeini ya wadhifa wa urais miaka minne iliyopita hayajatwa kikamilifu lakini akawaomba wapiga kura kumpa miaka mingine minne ili kuuimarisha uchumi wa Marekani unaoyumbayumba.

Michelle Obama ndiye aliyekuwa wa kwanza kumtetea mumewe katika siku ya kwanza ya mkutano huo wa siku tatu ambao utakamilika kwa hotuba ya Obama kesho Alhamisi ili kukubali uteuzi wa chama cha Democratic wa kupambana na Mitt Romney katika uchaguzi wa uraisi tarehe sita Novemba.

Bibi Obama alisema "Kama rais, utapata ushauri wa kila aina kutoka kwa watu tofauti, lakini unapohitajika kufanya uamuzi wako kama rais, kinachokuongoza ni maadili na maono yako pamoja na uzoefu wa maisha, mambo yanayokufanya uwe jinsi ulivyo"

Katika kinyang'anyiro ambacho ni kikali kutabiri zikiwa zimebaki wiki tisa kabla ya Wamerakani kupiga kura, Obama anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mgombea wa Republican Mitt Romney kwa sababu ya kudorora uchumi pamoja na asilimia 8.3 ya ukosefu wa ajira.
 


Source;Machibya

KALAPINA WA KIKOSI CHA MIZINGA AIGIZA MOVIE JUU YA MAISHA YA DK.ULIMBOKA.

Kamanda mkuu wa kikosi cha Mizinga, msanii wa Hiphop Kalapina mwishoni mwa mwaka huu ndio amepanga kuitoa na imfikie kila Mtanzania, movie mpya ambayo ameigiza kama kiongozi wa Madaktari Dr Ulimboka ambae siku kadhaa zilizopita alitekwa na kupigwa sana na wasiojulikana.

Pamoja na kwamba kwa sasa kuna stori za chinichini kwamba Dr Ulimboka ameondoka Tanzania kutokana na kuhofia usalama wake, Kalapina anaamini Dr Ulimboka hana haja ya kukimbia nchi kutokana na kuhofia usalama wake.

Namkariri Kalapina akisema “ninachoweza kumshauri Dr Ulimboka asiogope, watu wapo kama anahitaji kupewa ulinzi Kikosi cha mizinga tupo fiti kila idara na tuna kitengo cha kikosi kinaitwa Department of defence (DOD) kitengo cha ulinzi, kuna vijana wamefuzu mafunzo wanaweza kumlinda mtu yoyote, wanakodishwa kwa gharama nafuu tu kama unahitaji walinzi unaweza ukaniona, walinzi wa kulinda kumbi za disco na sehemu nyingine pia, kama anahitaji atapata kwa gharama nafuu”
Kuhusu hiyo movie mpya Kalapina atakayoigiza maisha ya Dr Ulimboka, amesema “nitajaribu kuonyesha tokea anarudi kutoka masomoni, harakati zake mpaka anaanza kazi, harakati za kutetea madaktari wenzake mpaka anapelekea kutekwa na kutupwa msituni, hii yote ni kuionyesha tasnia ya filamu kwamba tuna vitu vingi vya kuonyesha lakini nashangaa zimejaa filamu za ngono na filamu za upotoshaji”



source;Millard Ayo

NMB NA MPANGO WA FINANCIAL FITNESS KUSAIDIA ELIMU YA TANZANIA.

Benki ya NMB imewafikia wanafunzi 45,000 wa shule za msingi katika mpango wake wa kukuza uelewa wa maswala ya kifedha uitwao NMB Financial Fitness. Mpango huo ulioanzishwa mwezi Mei mwaka huu, una lengo la kuwahamasisha wanafunzi kujiwekea akiba kwa kutumia huduma za kibenki wanapokua wakubwa. 

Akizungumza katika utambulisho huo, mwanafunzi wa shule ya Liwale iliyopo mkoani Lindi Idrissa Ndumbaro aliishukuru benki ya NMB kwa elimu hiyo ambayo baadae itamwezesha kuwa na uelewa wa matumizi mazuri ya fedha pamoja na kujiwekea akiba.


Source;Mjengwa

MAGESE AWAKALISHA WAMAREKANI HADI MBUNIFU WA MICHELLE OBAMA.

Mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Happines Millen Magese ameshiriki Wiki ya Mitindo ya Mavazi ya New York nchini Marekani juzi. 

Onyesho hilo lilishuhudiwa na nyota wakubwa kama mwanasoka David Beckham huku wabunifu wakubwa duniani wakishiriki kuonyesha mitindo yao ya mavazi kama Tommy Hilfiger, Carolina Herrera, Michael Kors, Ralph Lauren na mwanamama Tracy Reese, ambaye gauni lake lilivaliwa na mke wa rais wa Marekani, Michelle Obama katika Kongamano la Kitaifa Chama cha Democratic. Mwanamitindo maarufu Naomi Campbell pia alipita stejini kuonyesha mitindo.


Source;Straika

Monday, September 10, 2012

MARAFIKI ZANGU WA FACEBOOK WENYE BIRTHDAYZ ZAO LEO.

Friendship is not something that is written on paper, because paper can be torn. It is neither something that can be written on a rock, for even a rock can break. But it is written on the heart of a person, and it stays there forever. Birthday wishes and blessings are coming your way, my friend!

Godwin Zephrin
sOURCE:my facebook profile by the name of Fredy Seventeeneleven

Sunday, September 9, 2012

J MARTINS AFATA NYAYO ZA P SQUARE APIGA COLLABO NA PITBULL.



Mpaka sasa Nigeria inaongoza kwa idadi ya vijana wake kufanya kolabo na mastaa wa muziki wa dunia kutokea Marekani pamoja na kupata deals, mfano ni kwa kolabo waliyoifanya P Square na rapper Rick Ross pia kolabo yao na Akon lakini pia Dbanj ambae yuko chini ya lebo ya Kanye West.

Naomba kukufahamisha kwamba kolabo inayofata sasa hivi ni ya Producer/msanii J Martins ambapo tayari ameshairekodi na Cuban American Rapper Pitbull na mpaka sasa jina la kolabo yenyewe halijatajwa.
 
Kingine ambacho unapaswa kufahamu ni kwamba wiki chache zijazo ndio video itafanyika kwenye mji wa Amsterdam ambapo stori kamili ziLISEMA kwamba ni hit ambayo Pitbull amelenga kupanua zaidi soko lake ambalo kwa sasa ni USA na Latin America na J Martins pia anataka kuvuka boda na kwenda umbali mrefu.

Bado haijawekwa wazi jamaa walikutanaje mpaka akakubaliwa kolabo lakini kolabo hiyo itamsogeza sana J Martins kwa sababu Pitbull ni staa ambae ameshine kwenye nyimbo zake na hata kolabo nyingi alizofanya na wakali kama J.Lo na Ne-yo.

Source;Millard Ayo

DOGO JANJA AKIWA NA CREW NZIMA YA MTANASHATI YA USTAZI JUMA NA MUSOMA KUKAMUA LEO BILLZ KATIKA UZINDUZI WA KUNDI.

KUNDI la burudani ya muziki wa kizazi kipya la ‘Mtanashati’  linatarajia kufanya uzinduzi  wake mpya katika Ukumbi wa Club Billicanas, uliopo katikati ya Jiji la Dar es salaam, eneo la Posta.

Akizungumzia uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa  ‘Mtanashati Entertainment’ Ostaz Juma na musoma, alisema tayari maandalizi ya uzinduzi huo yamekamila na kuongeza kuwa kinachosubiriwa ni muda ili kuwadhihirishia kile kilichokusudiwa.

Alisema katika uzinduzi huo utakaotumika pia kwa ajili ya kuwatambulisha upya wasanii wote watano wanaounda kundi hilo wakati huu ambao wanaendelea kujihimarisha kimuziki ambapo pia amewaomba wapenzi wa burudani kujitokeza kwa wingi kushuhudia uzinduzi huo.

Alisema katika kupamba siku hiyo, ukiacha burudani kutoka kwa wasanii hao, pia kutashushwa  disco la nguvu hadi kunapokucha na maarufu ‘DJ Ibra’ huku akisisitiza kuwa  ‘usiku wa leo utakuwa moto wa kuotea mbali’.

“Baada ya Mtanashati kuporomosha burudani wiki iliyopita katika ukumbi wa Maisha Club, wiki hii kazi inahamia Billicanas’ bila shaka watu wote walioudhuria burudani ya pale Maisha wanakumbukumbu nzuri juu ya burudani ya nguvu iliyofanywa na Dogo Janja na PNC, burudani ya leo ni zaidi ya ile ya Maisha” alisisitiza Ostaz Juma na musoma.

Alisema katika uzinduzi huo, kundi hilo litapiga nyimbo mbalimbali zikiwemo mpya pamoja na zile zinazoendelea kutamba katika vituo mbalimbali vya redio na televisheni  'Ya Moyoni' 'Checherumba'  ‘watasubiri’ na zinginezo zikitarajiwa kutumbuizwa katika uzinduzi huo.

Mtanashati ni kundi linaloundwa na wasanii watano  ambao ni Dogo Janja, Amazon, Y-Fil, PNC, Happy Balice ndani ya familia ya ‘Moja ya Muziki’ iliyopewa jina la ‘MTANASHATI ENTERTAINMENT’ chini ya Mkurugenzi wake Mkuu ‘Ostaz Juma na musoma’ ambaye kwa mujibu wake malengo makubwa ya kuanzishwa  ‘Mtanashati’  kumekusudia  mapinduzi mapya katika tasnia  ya Muziki wa Kizazi kipya.
Wakati huo huo habari zilizonifikia sasa hivi kupitia account yamgu ya BBM toka kwa dogo Janja zinasema ustaz Juma na Musoma amepata mtoto wa kiume toka kwa mke wake leo hii majira ya mchana.


Source;Kajuna son & Dogo Janja