Jana
Usiku ndani ya maisha club palikuwa na show kubwa ya Usiku Wa Wasafi
ila haikwenda kama ilivyo pangwa na msafi Diamond.Watu waliingia club
hio mapema na tayari kwa show kali kutoka kwa Diamond. Show ilianza saa
saba na nusu na baada ya dakika chache za Diamond kwenye stage fujo
zilianza, Kundi kubwa la vijana wasiojulikana walianzan kutukana watu,
kurusha chupa na viti, kupigana na kupora vitu vya thamani kutoka kwa
mashabiki wa Diamond. Chupa zilipoanza kurushwa kwenye stage ,moja
ilimpata Diamond mkononi na nyingine ilimjeruhi Bestizo Mkononi.Bestizo
ni Camera Men na Social Media Personal Wa Diamond kupitia
Thisisdiamond.com. Diamond alishuka kwenye stage na kwenda kwenye chumba
cha mapumziko mpaka fujo zilipotulizwa.
Chid
Benz aliongea na watu na kusema sio kitu kizuri kufanya fujo kwenye
onyesho la msanii kama Diamond.Kwani kama una chuki na Diamond mfate
mtaani na sio kwenye show yake kwani unaweza kuleta matatizo kwa
mashabiki wasio na hatia. Pia Chid Benz alimtuliza Diamond na kumuomba
apande kwenye stage kumaliza show na kuburudisha fans waliolipa na kuja
kumuona mtu wao.
Vitu
vya thamani kama Cheni,Pete na Camera ya Bestizo ya ThisisDiamond
iliporwa kwenye fujo hizo. Inasemekana Diamond na Uongozi wa maisha
ulipata taarifa kuhusu uwezekano wa fujo hizi kutokea na hatua
zilifanyika kuweka usalama zaidi ila vijana hawa walikuwa wengi na ndio
sababu ya show ya Diamond Kuharibika.
sOURCE;SAm Misago
No comments:
Post a Comment