Siku
yake ya kwanza ofisini kama Papa mtakatifu wa kanisa Katoliki, Papa
Francis 1 tayari anaanza kazi. Papa anatarajiwa kuwateua
wafanyakazi
wakuu watakaohudumu katika Vatican chini ya uongozi wake. Ameanza siku
yake kwa maombi ya kibinafsi katika hekalu ya mtakatifu Maria Maggiore
mjini Rome. Baadaye Papa atafanya misa ya sherehe katika kanisa la
Sistine.
Uteuzi atakaofanya Papa Francis, utatizamiwa kama
ishara ya mageuzi katika uongozi uliozongwa na kashfa nyingi na pia
utaonyesha mwelekeo anaonuia kuchukua kwa kanisa hilo.
Baadaye wikendi ijayo, Papa mpya anatarajiwa kukutana na vyombo vya habari vya dunia katika mkutano maalum.
Na
Jumapili, ataongoza misa yake ya kwanza kama papa. Hata hivyo yeye
mwenyewe atatawazwa rasmi kuwa Papa Francis 1, siku ya Jumanne.
No comments:
Post a Comment