Tukio lilitokea Ijumaa usiku
kwenye saa tatu kasoro Sinza Kumekucha Dar es salaam karibu na kanisa la
KKKT ambapo ilikua ghafla mlio wa risasi ukasikika ikiwa imelengwa kwa
dereva wa daladala.
Watu waliokuwepo karibu
wamesema dereva wa hii daladala anadaiwa kumkosea na kumkasirisha mtu wa
pikipiki alipokua kwenye foleni.
Ghafla mtu huyo wa pikipiki
ambae hakufahamika akiwa amebeba abiria inadaiwa alipita kwa mbele
akachomoa bastola na kupiga risasi na kuondoka.
Inadaiwa dereva wa daladala
aliepigwa risasi kichwani, alifariki muda mfupi baada ya tukio hilo huku
watu wakishuhudia abiria mbalimbali wakitokea madirishani na wengine
wakitoa vitu vyao kupitia madirishani.
millardayo.com
inaendelea kufatilia hii taarifa ili kupata taarifa za uhakika kutoka
kwa wahusika, wakiwemo polisi na taarifa zikipatikana utazipata kupitia
hapa HAPA.
No comments:
Post a Comment