Pages
Search This Blog
ushauri
Fay Pub
tangaza
Tuesday, March 19, 2013
MUIGIZAJI SNURA ANATANGAZA KUTAFUTA MUME ATAKAEMPA UHURU.
MSANII wa filamu na muziki mwenye mvuto wa aina yake Snura Mushi ‘Snura’, ameamua kutoa la moyoni kwa madai kuwa sasa anatafuta mwanaume wa kuweza kufunga naye pingu za maisha lakini kwanza kabisa akubali kumpa muda mrefu wa kutafuta pesa ili asiwe tegemezi baada ya kuingia ndani ya ndoa hiyo.
Akiongea kwa mbwembwe, Snura alidai si kwamba hataki kuolewa bali hataki kuishi ndani ya ndoa na kuwa tegemezi kwa mwanaume.
“Sitaki kuishi na mwanaume kabla hajakubali kunipa muda wa mimi kutafuta pesa...
Najua anaweza kuwa na uwezo wa kila kitu lakini hivyo vyote vitakuwa vya kwake na mimi natakiwa kuwa na mali zangu, lakini bila hivyo nitazeekea kwangu,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment