Rapper Chidi Benz, amempiga CowBama a,k,a
Ngwea nje ya Ambassador Lounge ikiyoko
Mkapatower, posta, usiku wa kuamkia leo.ugomvi
huo ulitokea baada ya Chidi kumzingua Dully
alipokua akiingia, ambapo mwisho wake aliamua
kuondoka.
Baada ya Dully kuondoka, Ngwea aliamua
kumuuliza Chidi (ambae mara nyingi huitana Dogo
lao), inakuaje unamzingua kubwa lao, ndipo Chidi
alipopaniki na kuanza kutoa lugha chafu huku
akitaka kutokumsikiliza Ngwea, inasemekana
Ngwea aliamua kukaakimya lakini Chidi aliendelea
kungea kwa hasaira na kusema"ndio nimemzingua
kwani yeye nani" na kumbadilikia Ngwea ambae
pia aliamua kuachana nae na kurudi ndani kwenye
meza aliyokua amekaa na washkaji zake,
haikuishia hapo Chidi amkamfata kwenye meza
hiyo na kuanza kumuongelea mbaya Ngwea, na
ndipo Ngwea akaamua kushuka chini ya jengo kwa
nia ya kuondoka.
akiwa huko huko chini Chidi alimfata na kumpiga,
ikiwa ni pamoja na kumkata na chupa mkononi,na
kupelekwa hospitali ambapo alitibiwa.
nimeongea na Ngwea ambae anasema haoni
chochote kilichomfanya kupigwa na msanii huyo.
Ngwea kwa sasa yupo katika kituo cha polisi
Oystabay kwa ajili ya kumfungua mashtaka, licha
ya kuumizwa pia ni kutokana na vitisho
alivyopewa na Benzi.
Sio mara ya kwanza kwa Chidi kupiga wasanii
wenzake..
Pages
Search This Blog
ushauri
Fay Pub
tangaza
Monday, March 25, 2013
KAJALA KUWA HURU SOON.
HUKUMU ya kesi iliyokuwa inamkabili staa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja na mumewe imetolewa leo na Hakimu Sundi Fimbo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar. Katika hukumu hiyo Kajala amehukumiwa kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 13 na mumewe kwenda jela miaka saba au kulipa faini ya shilingi milioni 200.
Kajala alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya mumewe, Faraji Agustino kukumbwa na msala wa kutakatisha fedha haramu.
Sunday, March 24, 2013
LIL WAYNE SASA HIVI YUKO FIT.
Rapper Lil Wyne ambae ameingia
kwenye headlines wiki hii kutokana na taarifa za kuzidiwa kwake na
kulazwa hospitali ikidaiwa anaugua degedege, amejitokeza kwa mara ya
kwanza kwenye video akiongea kuhusu tour yake na T.I ambapo kabla ya
kuanza kuizungumzia aliwashukuru fans wake kwa maombi wakati akiwa
hospitali.
GRADES MPYA ZA O LEVEL ZATOLEWA
Serikali
kwa kupitia wizara ya elimu imefanya mabadiliko kwenye madaraja ya
alama za mitihani ya kidato cha nne. Hapo awali, madaraja yalikuwa ni
kama ifuatavyo:
A = 81%-100%
B = 61%-80%
C = 41%-60%
D = 21%-40%
F = 0%-20%
Mabadiliko mapya yamefanywa na sasa madaraja MAPYA ni kama ifuatavyo:
A = 80%-100%
B = 65%-79%
C = 50%-64%
D = 35%-49%
F = 0%-34%
Taarifa imetolewa mapema ili wanafunzi kwa kidato cha nne waanze kujiandaa vyema na mitihani ijayo.
BIFU LA NEY WA MITEGO NA NIKKI MBISHI LAIVA?!
Katika
kile kinachoonesha bifu ya Ney wa Mitego na Nikki Mbishi kufikia
pabaya, Ney amemmwagia matusi ya nguoni rapper huyo wa ‘Kill Yo Self’
kupitia BBM.
Bifu la wasanii hao lilianza baada ya Nikki kudaiwa
kurekodi wimbo uitwao Ney wa Mitego ambayo anamzungumzia msichana mwenye
jina hilo na ambaye ana tabia za ukicheche.
CHINUA ACHEBE MWANDISHI WA "THINGS FALL APART" AMEFARIKI DUNIA.
Mwandishi mashuhuri kutoka
Nigeria Afrika Chinua Achebe amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82
ambapo familia imekataa kuweka wazi sababu za kifo chake.
Chinua ambae amekua akitumia wheel chair toka mwaka 1990, amefariki dunia akiwa hospitali Boston Marekani jana asubuhi.
Kitabu cha kwanza cha Achebe
ambacho ni ‘Things fall apart’ inasemekana ndio kitabu kinaachoongoza
Afrika kwa kuchapishwa kwa lugha tofauti ambacho pia kilichapishwa kwa
mara ya kwanza mwaka 1958.
MASHABIKI WA SIMBA WAZICHAPA WAKATI WA MAPOKEZI YA RAGE
Mashabiki hao wa Simba walizichapa baada ya kugundua baadhi yao walikwenda uwanjani kwa lengo la kumfanyia vurugu mwenyekiti wao wakati wa mapokezi, kabla ya mashabiki kutwangana, mashabiki waliokuwa wakimuunga mkono mwenyekiti wao walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali na walionekana wenye matumaini makubwa na Rage huku wakisisitiza bado wanautambua uongozi wake na hakuna anayeweza kumuondoa zaidi yao wenyewe.
Hata hivyo, baadaye lilitokea kundi dogo la mashabiki wa Simba ambalo lilisadikiwa kuwa ni kundi la Mpira Pesa ambalo limekwenda uwanjani hapo kwa ajili ya kufanya fujo na hivyo kuanza kushambuliwa kwa makonde wakidaiwa kuhusika na mkutano uliotangaza kumwondoa Rage madarakani.
Tuesday, March 19, 2013
MUIGIZAJI SNURA ANATANGAZA KUTAFUTA MUME ATAKAEMPA UHURU.
MSANII wa filamu na muziki mwenye mvuto wa aina yake Snura Mushi ‘Snura’, ameamua kutoa la moyoni kwa madai kuwa sasa anatafuta mwanaume wa kuweza kufunga naye pingu za maisha lakini kwanza kabisa akubali kumpa muda mrefu wa kutafuta pesa ili asiwe tegemezi baada ya kuingia ndani ya ndoa hiyo.
Akiongea kwa mbwembwe, Snura alidai si kwamba hataki kuolewa bali hataki kuishi ndani ya ndoa na kuwa tegemezi kwa mwanaume.
“Sitaki kuishi na mwanaume kabla hajakubali kunipa muda wa mimi kutafuta pesa...
Najua anaweza kuwa na uwezo wa kila kitu lakini hivyo vyote vitakuwa vya kwake na mimi natakiwa kuwa na mali zangu, lakini bila hivyo nitazeekea kwangu,” alisema.
TIGER WOODS AVUTA MANZI MPYA.
Kibongobongo way back walikwishawahi kusema mapenzi ni kikohozi, na
haiwezekani kuyaficha na leo hili limethibitika baada ya Golfer wa
dunia, Tiger Woods kuamua kukiri kuwa katika mahusiano na bibie Lindsey
Vonn ambaye naye pia ni mwanamichezo.
Tiger ameamua kumwaga mchele kwenye kuku wengi lakini ameomba baada ya watu kufahamu kuwaacha wafanye yao na kuheshimu privacy yao.
Tiger ameamua kumwaga mchele kwenye kuku wengi lakini ameomba baada ya watu kufahamu kuwaacha wafanye yao na kuheshimu privacy yao.
Monday, March 18, 2013
WIZKID AMWAGA MKWANJA KWA MASHABIKI.
Kufuatia mafanikio makubwa kimuziki ambayo msanii wa muziki wa
Naijeria, Wizkid ama Weezy kama anavyojulikana sasa, mwishoni mwa wiki
aliamua kufanya kitu cha kipekee huko Lagos kwa kufanya onyesho la bure
kwaajili ya mashabiki wake.
Wizkid mwenyewe amesema kuwa ameamua kufanya hivi kutokana na ukweli kuwa kipaji cha kuimba amekipata bure bila kumpa Mungu kitu chochote.
USIISHI KWA HISTORIA.
Utamuacha wanamke fulani kwa kashfa zote na kejeli za kila namna kwamba hafai
na haoleki ILA Mwanaume yule atamchukua na kudate
nae na pengine atamuoa na wataishi
kwa furaha na kuzaa watoto,
atasahau hata kama
uliwahi kuwa Boy wake na kashfa
zako
Kapata Perfect Match yake....Mwanamke fulani
ataachwa na wewe utakutana nae
na kumpokea,na pengine utamuoa na kuishi kwa amani.
Umepata Perfect match yako..
Hii inaitwa Love Circle...
Hakuna Mwanaume wala Mwanamke 2nd hand/Used
kwamba hafai...
Kama hafai kwako kuna
mtu kwake huyo mdada ni
Malkia...
Kama hafai kwako,kuna
mdada
anamtamani amfanye awe
mfalme wake..
Binadamu hana Mshale wa
kuonyesha Kilomita ngapi
katembea au ana listi ya watu
mia
ngapi!
Kuna watu wametumika kwelikweli,wameshusha
engine mara6 na kumwaga oil nyeusi
ila wameolewa na kutulizwa ndani..
Wewe unayejiona mpya mpya unanukia Nylon bado
unamanga manga...Haijalishi ww ni Mpya au Used,
when ur perfect match arrives,
everything else about Past
will be history!
Subscribe to:
Posts (Atom)