MWIMBAJI
wa Muziki wa Injili , Bahati Lusako Bukuku amefunguka kuwa amepata
mchumba lakini tatizo linabaki kuwa mume wake wa zamani, Daniel Basila
ambaye anasuasua kumpa talaka yake
Akizungumza jijini Dar juzikati, staa huyo anayetamba na wimbo wake wa Dunia Haina Huruma aliweka wazi kwamba hivi karibuni Mungu amemjalia kupata mchumba ambaye anahofia kumwanika kwa kuwa anabanwa na kifungo cha ndoa yake ya kwanza aliyofunga na Basila.

Bahati alisema kuwa kifuatacho inabidi adai talaka yake kwa nguvu zote
hata ikiwezekana kufikishana polisi ili aondokane na kifungo cha ndoa
hiyo na aanze mipango ya ndoa kwa kuwa hataki kumtendea Mungu dhambi.
Alisema kuwa, mara nyingi amekuwa akimkumbusha mumewe huyo wa zamani kuhusu talaka lakini amekuwa akimwambia asikonde talaka yake ipo hivyo avute subira.
Bukuku aliolewa na Daniel na kufanikiwa kupata mtoto mmoja ambaye alifariki dunia mwaka 2006 kabla staa huyo kutengana na mumewe.

No comments:
Post a Comment