Mungu akijalia 2013 utakua
mwaka ambao Tanzania itaingia kwenye headlines, Tanzania itapata mgeni
miongoni mwa wageni ambao wamepanga kuja kuishi hapa.
Pamoja na ustaa alionao na
utajiri alionao ambao umetokana na muziki anaoufanya, mkali ambae
alichaguliwa kuiwakilisha Congo DRC kwenye kolabo na R. Kelly, mkali
ambae alipenyeza mpaka kupata shavu la kufanya kolabo na staa Olivia wa G
unit time hizo, Fally Ipupa ametangaza kwamba katika sehemu ya makazi
yake Africa, anahitaji kuja kuishi Tanzania pia na mpango huo
ameufikiria kuanzia mwakani.
Fally Ipupa ambae ni staa kwenye muziki Africa
amesema mipango yake ya 2013 ni pamoja na kununua au kujenga nyumba na
kuishi Tanzania.
Kwa sasa anaishi Congo ambako
ndio kwao, ana miliki nyumba Paris Ufaransa pia ambako ameanza kuishi
miaka 7 iliyopita, na baada ya kuvutiwa na Tanzania, Fally ameamua
Tanzania iwe sehemu ya makazi yake.Source:millard Ayo
No comments:
Post a Comment