ushauri

Fay Pub

Fay Pub
Fay Pub Sinza,We Rock,it is a good place to be cool and usalama wa kutosha!!Fay Pub ipo Sinza kumekucha,nyuma ya Seven Up kama unaelekea shamool Hotel,, kwa maelekezo piga namba 0715 556453

tangaza

Sunday, March 17, 2013

DEREVA WA DALADALA ACHAPWA RISASI AKIWA KWENYE FOLENI DAR.

Tukio lilitokea Ijumaa usiku kwenye saa tatu kasoro Sinza Kumekucha Dar es salaam karibu na kanisa la KKKT ambapo ilikua ghafla mlio wa risasi ukasikika ikiwa imelengwa kwa dereva wa daladala.
Watu waliokuwepo karibu wamesema dereva wa hii daladala anadaiwa kumkosea na kumkasirisha mtu wa pikipiki alipokua kwenye foleni.

Ghafla mtu huyo wa pikipiki ambae hakufahamika akiwa amebeba abiria inadaiwa alipita kwa mbele akachomoa bastola na kupiga risasi na kuondoka.
Inadaiwa dereva wa daladala aliepigwa risasi kichwani, alifariki muda mfupi baada ya tukio hilo huku watu wakishuhudia abiria mbalimbali wakitokea madirishani na wengine wakitoa vitu vyao kupitia madirishani.
millardayo.com inaendelea kufatilia hii taarifa ili kupata taarifa za uhakika kutoka kwa wahusika, wakiwemo polisi na taarifa zikipatikana utazipata kupitia hapa HAPA.

SOURCE:Millard Ayo

No comments:

Post a Comment